Monday, 12 October 2015


TAARIFA YA SERIKALI
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Vongozi wa Dini mbali mbali Nchi mara baada ya kufanya mazungumzo nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Kiongozi wa Timu ya Waislamu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Kabi na Kulia ya Balozi ni Kiongozi wa Wakristo Askofu Augustino Mweleli Shao.

 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakamilisha taratibu zilizobakia na tayari inajiandaa kuwachukulia hatua za Kisheria watu wote waliohusika kuharibu kwa makusudi zoezi zima la Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofanyika Tarehe 25 Mwezi Oktoba mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akizungumza na Viongozi wa Dini mbali mbali Nchini aliokutana nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kutafakari na kutafuta mbinu za kuendelea kujaribu kudumisha amani ya Nchi iliyotetereka  na kuleta mtafaruku katika kipindi hicho cha Uchaguzi.
Balozi Seif alisema ina uthibitisho kamili wa vielelezo vya ushahidi wa udanganyifu kwa maeneo yote ya Zanzibar hasa katika Majimbo ya Uchaguzi ya Kisiwa cha Pemba.
Alisema Afisa  wa Tume ya Uchaguzi au Mtu yoyote aliyehusika na udanganyifu huo aelewe kwamba mkondo  wa sheria utamkumba kwa vile vitendo walivyofanya wameisababishia hasara kubwa Serikali pamoja wa washirika wa maendeleo walioamua kusaidia uchaguzi huo.
Balozi Seif alibainisha kwamba  wakati wahusika hao wanapandishwa katika vyombo vya kisheria kujibu shutuma zinazowakabili Serikali kwa upande wake  itaweka hadharani uthibitisho kamili wa vielelezo vya ushahidi wa udanganyifu huo ili Wananchi wapate fursa ya kuelewa dhambi hiyo mbaya waliyofanyiwa na watu wachache kwa tamaa binafsi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia Viongozi hao wa Dini kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga vizuri kupitia vyombo vyake vya ulinzi kwa kupiga Doria maeneo yote katika kuona amani ya nchi inaendelea kudumu.
Aliwapongeza Viongozi hao wa Dini kwa jitihada zao wanazochukuwa za kutumia busara zao kwa kukutana na Viongozi  wa pande mbali mbali za Kisiasa wakilenga kusaidia kutuliza mumkari na machungu ya waumini wao ambao takriban wote ni  wafuasi wa vyama vya Kisiasa vilivyopo hapa Nchini.
Alivilaumu baadhi ya vyombo vya Habari hasa vile vya Nchi za Magharibi jinsi vilivyoonyesha wazi Taarifa zao nyingi  wanazotowa za zoezi zima la uchaguzi Mkuu wa Zanzibar zikionyesha  kuegemea upande mmoja tu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea masikitiko yake juu ya wangalizi wa Kimataifa walioamua kufuatilia uchaguzi Mkuu wa Zanzibar kwamba hawakwenda Kisiwani Pemba muda wote wa zoezi la kupiga kura kufuatilia changamoto zilizojitokeza katika majimbo ya Pemba.
" Nimesikitishwa na waangalizi wa Kimataifa waliokuwepo Zanzibar kwa karibu mwezi mmoja kufuatilia kampeni na uchaguzi wake wameshindwa kwenda Pemba wakati wa zoezi la kupiga kura na kuonekana  zaidi katika majimbo ya Kisiwa cha Unguja.
Balozi Seif aliishauri Idara ya Habari Maelezo kuendelea kufuatilia Taarifa zinazotolewa na vyombo mbali mbali vya Habari ndani na nje ya Nchini na kukemea au kutoa Taarifa dhidi ya uchochezi unaotolewa na vyombo hivyo.
Nao Viongozi hao wa Dini mbali mbali Nchini wameishukuru na kuipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua iliyochukuwa katika kusimamia amani ya Nchi.
Wananchi wa Zanzibar  wamerejea katika harakati zao za kawaida  za kimaisha  baada ya kutokea hitilafu tofauti ndani ya zoezi zima la upigaji kura kwenye  uchaguzi Mkuu wa Tarehe 25 Mwezi uliopita na kupelekea kuibuka kwa mtafaruku uliotikisa  amani ya Taifa.

 Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Nd. Vual Ali

TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR YAFUTA UCHAGUZI WA ZANZIBAR
 KWA SABABU ZILIZOMO KWENYE BARUA YA MWENYEKITI WA TUME.
 KAMA INAVYOSOMEKA HAPO CHINI.
 
ZEC: MAALIM SEIF ANAPASWA KUCHUULIWA HATUA ZA KISHERIA KWA KUTANGAZA MATOKEO.
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imesema imesikitishwa na kitendo cha mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF) kujitangazia ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili tarehe 25 Oktoba, 2015 na imevitaka vyombo vinavyosimamia utii wa sheria kumchukulia hatua kiongozi huyo wa CUF.
“kitendo cha Maalim Seif kujitangaza mshindi amevunja kifungu cha 42 (5) cha sheria ya mwaka 1984 ambacho kinaipa mamlaka Tume ya Uchaguzi kuwa chombo pekee chenye mamlaka hayo” Mwenyekiti huyo alifafanua.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari leo, Mweyekiti wa ZEC Jecha Salum Jecha alisema kuwa Maalim Seif ametenda kosa la jinai hivyo mamlaka zinazohusika zinapaswa kumchukulia hatua.
Kwa mujibu wa kifungu hicho, mtu akithibitika ametenda kosa hilo atahukumiwa kulipa faini ya Tzs laki tano au kwenda jela miaka mitano au adhabu zote.
“Tume haina mamlaka ya kumkamata wala kumhoji Maalim lakini viko vyombo vyenye mamlaka hayo hivyo itakuwa ni vyema vikatimiza wajibu wao kwa kumkamata na kumhoji mhusika hasa ukizingatiwa kuwa hii ni mara ya pili kwa Maalim Seif kutenda kosa kama hilo” Mwenyekiti wa Tume alieleza.
Alibainisha kuwa Tume yake imekijadili kitendo hicho kwa makini na uzito unaostahiki na kubainisha kuwa tangazo hilo linaweza kusababisha uvunjifu wa amani na utulivu uliopo nchini.
Bwana Jecha alibainisha kuwa Maalim Seif, kama walivyo wagombea wengine 13 wa nafasi ya urais wa Zanzibar wanaelewa fika sheria hiyo hivyo alitoa wito kwa wagombea wengine kuwa watulivu kama walivyo wananchi.
Kuhusu kasi ndogo ya Tumeyake kutangaza matokeo, Mwenyekiti huyo alisema hivi sasa kazi kubwa wanayoifanya ni kuhakiki kura kujua kama hakuna tofauti ya kura baina ya zile zilizoandikwa na hali halisi.
“Wanaoandika na kuhesabu kura wote ni binadamu hivyo wanaweza kuchanganya mahesabu na ndio maana kazi yetu hivi sasa ni kulinganisha kura”alisisitiza Mwenyekiti wa Tume.
Kuhusu kukamatwa kwa karatasi za kupigia kura huko katika jimbo la uchaguzi la Chonga, Wilaya ya Chake Chake, mkoa wa Kusini Pemba, Bwana Jecha alikiri kutokea kwa hilo na kwamba suala hilo sasa liko chini ya mikono ya Jeshi la Polisi.
Alitahadharisha juu vitendo vya baadhi ya wagombea kuchukua vyeti bandia vinavyoonesha kuwa  tayari wao wameshinda nafasi za ubunge au ujumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Bwana Jecha alitoa wito kwa wananchi kufanya subira wakati huu Tume yake ikifanya kazi ya kukusanya na kuhakiki kura na baadae kuwatangaza washindi.
PRESS RELEASE  
 CCM CONDEMNS MAALIM SEIF AND CUF.
Chama cha Mapinduzi (CCM) has condemned opposition Civic United Front (CUF) presidential candidate Maalim Seif Sharif Hamad for declaring himself a winner in the Zanzibar Presidential election.
Addressing local and international media at CCM offices here, CCM Deputy Secretary General Mr. Vuai Ali Vuai said what Mr. Hamad has done is against the law and urged an outright legal action against him.
Mr. Vuai, who was accompanied by some central committee members of his party, also accused Zanzibar Electoral Commission (ZEC) for not taking any action against Maalim.
“We don’t know the intention of Maalim Seif and his party to announce the results which is against the law of the land. He and CUF have violated section 42 (5) of the Election Act, 1984 which gives mandate only to ZEC to announce the elections results” He insisted.
Mr. Vuai was adamant that Mr. Hamad and CUF know what they are doing which was none than pressurizing ZEC and scare its members from fulfilling their duties according to the law.  
During the occasion, Mr. Vuai also expressed his party’s dissatisfaction over the way that ZEC handled some key issues during elections including conducting elections in many constituencies in Unguja and Pemba without CCM agents.
He questioned the wisdom of ZEC officials to let voting start in Magharibi ‘A’ & ‘B’ districts without CCM agents and posed a challenge to the media to think of what would be the situation if that could happen to CUF.
“We went to ZEC district office on the 24th October where we were assured of and we saw identity cards for agents of all parties including ours but next day we were told our agents IDs were nowhere to be seen” he elaborated and added that it was only after four hours some IDs were issued.
Responding to questions from reporters about his party’s confidence over ZEC, Mr. Vuai said that his party is confident that ZEC would continue to exercise its duties and responsibilities independently according its legal mandate.   
Meanwhile, CCM central committee member, Shamsi Vuai Nahodha has told Maalim Seif and CUF that it could be more logical and appropriate if ZEC members from CUF would resign the post before announcing the results as they have done.
“it would be understandable had ZEC members from CUF resigned otherwise what they have done is a sheer fear of defeat and a tactical measure to put pressure to ZEC” he said.
Central committee member Pandu Ameir Kificho said “the key issue here is that Maalim and CUF have violated the constitution and election law. We have come to the media to assist us to remind the citizenry that what Maalim has done is unconstitutional and deserves the action of law”

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimelaani vikali kitendo cha Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF) kujitangaza mshindi kinyume na sheria ya Uchaguzi huku ikiishangaa Tume ya Uchaguzi Zanzibar-ZEC kwa kukaa kimya dhidi ya kitendo hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari jioni hii, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai amesema kitendo cha Maalim Seif kujitangaza mshindi kimekiuka sheria ya uchaguzi na kuhoji dhamira ya kiongozi huyo kufanya hivyo. 
“Ni tukio la kushitusha sana na hatujui malengo ya kitendo hiki au anataka kuitia nchi katika mtafaruku?” Alihoji Vuai na kuitaka ZEC itekeleze majukumu yake kwa kuzingatia Katiba na Sheria.Katika mkutano huo, Vuai alieleza kusikitishwa kwake na baadhi ya matukio yaliyotawala uchaguzi huo ambayo aliyaeleza kuwa yalilenga kukihujumu chama hicho ili kuharibu ushindi wa wagombea wake.
“Huko Pemba katika jimbo la uchaguzi la Chonga wakala wa CUF alikamatwa na karatasi za kupigia kura akishirikiana na afisa wa Tume” alieleza Vuai na kuhoji ni kura ngapi zimepita bila ya kugunduliwa.
Aidha, chama hicho kilieleza kitendo cha wakala wake wote katika Wilaya za Magharibi ‘A’ & ‘B’ kutopewa vitambulisho kilikuwa na lengo la kuharibu ushindi wa chama hicho kwa kuwa ZEC iliruhusu uchaguzi kuendelea kwa muda mrefu bila ya kuwepo mawakala wake.
“Tulikwenda Tume tarehe 24 Oktoba, 2015 tukahakikishiwa na kwa kuviona vitambulisho vya mawakala wa vyama vyote, lakini siku iliyofuata tulipokwenda kuvichukua vyetu tukaambiwa havionekani” alifafanua Vuai na kuhoji kilichotokea baina ya upigaji wa kura ulipoanza saa moja hadi wakala wa kwanza kupata kitambulisho baada ya saa karibu nne ambapo sehemu nyingine wakala wao walifika saa saba hawajapata vitambulisho.
Alipoulizwa kuwa malalamiko hayo yanamaanisha chama chake hakina imani na ZEC, Naibu Katibu Mkuu huyo aliwaeleza waandishi wa habari kuwa chama chake bado kinaiamini Tume hiyo lakini inaikumbusha wajibu wake.
CCM ni chama kikubwa,tujiulize kama tukio hili lingewakuta wenzetu wa CUF ingekuwaje. Kwa nini vitambulisho vyetu vipotee katika eneo lenye wapiga kura wengi zaidi kuliko sehemu nyingie yeyote Zanzibar”alifafanua Vuai na kuongeza kuwa wajibu wa kutii sheria ni wa kila mtu na kila chombo hivyo isingekuwa busara kwa CCM kukaa kimya kwa yaliyotokea.
Wakati huo huo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Shamsi Vuai Nahodha amesema kitendo cha Maalim Seif kutangaza matokeo ni njama za kuishinikiza Tume ya Uchaguzi kufuata matakwa yao.
“Kitendo cha Maalim kujitangazia ushindi ni njama za kuishinikiza ZEC ifanye kile inachokitaka. Tungeelewa kama wajumbe wa ZEC kutoka chama cha CUF wangekuwa wamejizulu”alieleza Shamsi wakati wa kujibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari.
Akijibu swali kuhusu lawama kuwa serikali imeleta askari wengi vituoni, Shamsi ambaye ni Waziri Kiongozi mstaafu na pia amewahi kushika nafasi ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa alisema vyombo hivyo vinafanyakazi wakati wote si wakati wa uchaguzi tu na viko kuhakikisha ulinzi wa wananchi na mali zao.
Leo asubuhi Maalim Seif Sharif Hamad alitangaza ‘matokeo’ ya uchaguzi mkuu kinyume na sheria ambapo alijitangaza mshindi wa nafasi ya urais.
“Hoja ya msingi hapa yupo mtu amefanyakazi kinyume na Katiba na Sheria.Tumekuja kukumbushia wajibu wa kufuata Katiba na Sheria, tunataka muielimishe jamii kuwa kitendo cha Maalim kujitangazia ushindi ni cha uvunjifu wa Katiba na Sheria” Alieleza Mheshimiwa Haji Omar Heri.

Matukio ya uvunjaji sheria za uchaguzi yaliotokea Zanzibar.
Wazanzibari wagundua wizi mkubwa wa kura uliofanyika katika kisiwa cha Pemba pamoja na baadhi ya majimbo hasa katika majimbo ya mjini magharibi.Kumekuwepo pia ongezeko la kura katika baadhi ya vituo zaidi ya idadi ya wapiga kura.
Hali hiyo iliyosababisha baadhi ya wagombea kufungua kesi mahakamani.Chama tawala, CCM kimewakilisha malalamiko tume ya Uchaguzi Zanzibar. CCM imelalamikia mgombea wanafasi ya urais wa CUF kujitangazia ushindi kwa kutangaza matokeo kinyume cha sharia. Miongoni mwa shutuma dhidi ya tume ni pamoja na kutowapa mawakala wa CCM vitambulisho, hali iliyowazuia kutotekeleza majukumu yao vituon.Imeonekana pia baadhi ya matokeo kutofautiana na matokeo halisi yaliyopo tume.
  
ZANZIBAR WAENDELEA KUPIGA KURA KWA AMANI NA UTULIVU MKUBWA. HONGERA DR. SHEIN .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt.Idriss Muslim Hija (kushoto) wakati alipowasili katika kituo cha kupiga kura Skuli ya Bungi msingi wilaya ya Kati Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika foleni ya wapiga kura katika kituo cha kupiga kura Skuli ya Bungi wilaya ya Kati Unguja zoezi ambalo limefanyika leo,(wa pili kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt.Idriss Muslim Hija.

6968 ///// 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein  akipokea karatasi ya kupigia kura kutoka kwa Afisa  Sibira Ramadhan Iddi katika kituo cha kupiga kura Skuli ya Bungi wilaya ya Kati Unguja zoezi ambalo limefanyika leo.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein akitumbukiza kura katika kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Bungi msingi wilaya ya kati  Mkoa wa Kusini Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein akitumbukiza kura katika kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Bungi msingi wilaya ya kati  Mkoa wa Kusini Unguja.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein akitumbukiza kura katika kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Bungi msingi wilaya ya kati  Mkoa wa Kusini Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein akifanya mahojiano na waandishi wa habari baada ya kipiga kura leo katika kituo cha Skuli ya Msingi Bungi Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja.

DK.SHEIN APIGA KURA NA KUSEMA:NITASHINDA KWA KISHINDO
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. Ali Mohamed Shein amepiga kura na kueleza kuwa ana matumaini makubwa ya kushinda uchaguzi huo kwa kishindo kuliko uchaguzi uliopita.Akijibu maswali ya waandishi wa habari mara ya baada ya kupiga kura huko katika kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Msingi Bungi katika jimbo la uchaguzi la Tunguu, Wilaya ya Kati Unguja, Dk. Shein amesema atashinda uchaguzi huo na kuahidi mambo mazuri kwa wananchi wa Zanzibar. “Nimeongoza vyema serikali yenye Mfumo wa Umoja wa Kitaifa, tumetekeleza Ilani kwa asilimia 98, tumeimarisha maslahi ya watumishi na huduma za jamii zimeimarika yote hayo yananifanya niamani kuwa nitashinda kwa kishindo” Dk. Shein alieleza. Akijibu swali kuhusu mipango ya baadae endapo atachaguliwa, Dk. Shein alisema wananchi watarajie mambo makubwa zaidi ya mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya kipindi kilichopita kwani Ilani ya 2015-2020 imezingatia mambo mengi zaidi na makubwa zaidi.  Kuhusu suala la wananchi kulinda kura mgombea huyo wa CCM alieleza kuwa “si sahihi, kura hazilindwi na wapiga kura na katika hili wanasiasa wasiwababaishe wananchi” na kuwataka wananchi wakishapiga kura warudi majumbani kusubiri matokeo. Alipotakiwa kueleza kama atakubali matokeo aliweka wazi kuwa katika ushindani kuna kushinda na kushindwa hivyo suala la mtu kusema anakubali au hakubali halina msingi na wito kwa wapinzani wake atakapowashinda wakubali matokeo washirikiane kujenge nchi. Kuhusu malalamiko ya wapinzani kama yalivyonukuliwa katika swali la mwandishi wa habari ya kuwepo majina ya watu waliokufa katika daftari, Dk. Shein alisema suala hilo liko chini ya mamlaka ya Tume ya Uchaguzi ambayo inafanya kazi kwa uhuru bila ya kuingiliwa. Dk. Shein aliwaeleza waandishi wa habari kuwa ameridhishwa na maandalizi ya Tume ya Uchaguzi kuanzia mwanzo wa uandikishaji hadi kupiga kura na anaamini kuwa zoezi hilo litakweda vyema hadi mwisho. Kwa hivyo aliwataka wananchi kujihumu vituoni kupiga kura mapema huku wakifuata taratibu zote na maelekezo ya Tume ikiwemo kurejea majumbani mara baada yak kupiga kura. Akijibu swali kuhusu hatma ya serikali yenye Mfumo wa Umoja wa Kitaifa endapo wapinzani watakataa matokeo na kususia, Dk. Shein alijibu kwa kifupi kuwa “suala hilo liko wazi katika Katiba” hivyo kuwamtaka mwandishi akasome Katiba ili kupata jibu sahihi.
MAKAMO WA RAIS WA TANZANIA DR. MOHAMED GHARIB BILAL APIGA KURA .
   Makamo wa  Rais  Dr  Mohamed Gharib  Bilal  akipokea maelezo kutoka  afisa  wa tume ya      uchaguzi.

                           MAKAMO wa Rais  Dr Mohamed Gharib Bilal akiiingiza kura zake
                      katika   sanduku  la kura mara baada ya kumaliza kufanya kituoni
                      Kiembe Samaki. Wilaya ya Mjini Magharaibi/
MAKAMO WA PILI WA RAIS  BALOZI SEIF ALI IDDI AKIPIGA KURA KATIKA KIYUO CHA KITOPE .
  Mgombea nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa Tiketi ya CCM Jimbo la Mahonda ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika foleni ya kusubiri kupiga kura kwenye Kituo chake kiliopo Skuli ya sekondari ya Kitope.
 Balozi Seif akipiga kura ya Kumchagua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Bunge ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Kituo chake hapo Skuli ya Sekondari ya Kitope.

 Karani wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ambae jina lake halikupatikana akimueka alama Balozi Seif kuashiria kwamba ameshakamilisha zoezi la Kupiga kura ya kumchagua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, Mbunge, Mwakilishi na Diwani.
Balozi Seif akizungumza na vyombo vya Habari mara tuu bada ya kumaliza kutumia haki yake ya kupiga kura hapo Skuli ya Sekondari ya Kitope ambapo ndio kwenye kituo chake cha uchaguzi.

RAIS MSTAAFU AKIPIGA KURA DR. SALMIN AMOUR


Rais mstaafu wa  Zanzibar Dr Salmin  Amour  Juma  akipigakura katika kituo cha  skuli ya  Jangombe  Zanzibar.

TUNAMSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWA KUMALIZA KAMPENI KWA SALAMA NA AMANI.
ND.WANANCHI TUPIGE KU RA KWA AMANI NA UTULIVU AHSANTENI SANA.
TUNATOA SHUKRANI ZA DHANI KWA WANANCHI  KWA  UPENDO MLIOUNESHA KWA KUJA KWA  WINGI KATIKA UWANJA WA KIBANDA MAITI KUJA KUHITIMISHA KAMPENI ZETU NA KUWASIKILIZA MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR DR. ALI MOHAMED SHEIN NA MGOMBEA MWEZA WA URAIS WA TANZANIA MAMA SAMIA SULUHU HASSAN. NDUGU WANANCHI TUNAKUOMBENI OMBI HILI KAMA  LINAVYOJIONESHA HAPO  CHINI.
KWA KUTHAMINI MCHANGO WENU WANANCHI WAGOMBEA WETU WATAKUTUMIENI UJUMBE KWENYE SIMU ZENU NA KUKUPIGIENI SIMU KUKUOMBEANI MUWATILIE KURA. NDUGU WANANCHI HAWA NDIO VIONGOZI WALIO KARIBU NA NYIE NA NDIO WANAOJALI WANANCHI WAO.
CCM YAFUNGA KAMPENI NA KUWATIA HOMA WAPINZANI WAKE
Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimemaliza kampeni yake kwa kufanya mkutano mkubwa wa kampeni katika kiwanja cha Kibandamaiti mjini Unguja na kusisitiza ushindi kwa chama hicho ni lazima.
Katika kile kinachoonekana kuwa ni kufurahia ushindi wananchi waliohudhuria mkutano huo walionesha kujiamini, furaha na bashasha tangu mwanzo hadi mwisho huku wakiimba nyimbo mbalimbali zikiwemo za kusifu Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 na kuwakumbuka waasisi wake.
Nyimbo hizo kama ‘Abeid Nenda tunakutuma’ ambao unazungumzia wananchi wa Zanzibar walivyomuunga mkono Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Karume kufanya Mapinduzi mwaka 1964 kuwaondoa wakoloni na wimbo ‘sisi tumegomboka’ unaotoa ujumbe kuwa kuwepo kwao hapo wakiwa huru ni matokeo ya wanamapinduzi waliopoteza roho zao kutetea utu na heshima ya mzanzibari  zilivuta hisia za wazee kwa vijana.
Mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi wakuu wa chama hicho baadhi yao wakiwa wastaafu ambao wengi wao walipewa nafasi ya kuzungumza ambao ujumbe mkuu ulikuwa “chagua CCM kuijenga Zanzibar na Tanzania yenye amani, utulivu, upendo, mshikamano na maendeleo”
Mbali ya mgombea Urais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, wengine waliozungumza ni Mama Fatma Karume mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharaib Bilal, Rais Mtastaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muugano wa Tanzania Mzee Ali Haassna Mwinyi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Mji wa Zanzibar pamoja na sehemu nyingi za mashamba jana zilihamwa kwa muda kuhudhuria mkutano huo ambao kwa baadhi ya wachambuzi wa kisiasa hapa wanaeleza kuwa mahudhurio ya mikutano ya Kampeni ya CCM katika uchaguzi wa mwaka huu inatoa ishara mbaya kwa wapinzani wa chama hicho.
Baada ya kusimamisha shughuli za mji wa Zanzibar hadi majira ya saa 3 usiku wakati ilipozindua kampeni zake tarehe 13 Septemba, 2015, Jeshi la Polisi leo limezuia misafara ya magari ya chama hicho kutoka eneo la mkutano kwenda katikati ya mji hasa eneo la Michenzani ambako kuna wafuasi wengi wa CCM ambapo misafara kama hiyo kupokelewa kwa shangwe na wananchi wengi kujiunga nayo hivyo kuwa sherehe ya aina yake.
Wananchi waliohojiwa walieleza kuwa Jumapili tarehe 25 Oktoba, 2015 kazi itakuwa moja tu kuwachagua wagombea wa CCM nafasi zote kuanzia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na wabunge, wawakilishi na madiwani.  
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  amewahakikishia wanaCCM na wananchi wa Zanzibar kuwa ahadi zake zote alizoziahidi zitatekelezwa baada ya kupata ridhaa ya wananchi huku akisisitiza kuwa yoyote atakaevuruga amani siku ya uchaguzi atakiona.  
Dk. Shein ambaye ni Mgombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM aliyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye mkutano wa kufunga Kampeni ya chama hicho uliofanyika huko katika viwanja vya Demokrasia, Kibandamaiti Mjini Unguja, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi na wanaCCM.  
Dk. Shein alitoa shukurani kwa wanaCCM na wananchi kwa kuhudhuria kwa wingi katika mikutano yote tokea tarehe 13 mwezi huu zilipozinduliwa Kampeni za chama hicho huku akieleza kuwa ahadi zote zilizoahidiwa na chama chake kupitia Ilani ya CCM zitatekelezwa.  
Alisema kuwa sekta zote 23 zilizoahidiwa zitatekelzwa  zikiwemo za uchumi, uzalishaji, kilimo, mifugo, miundombinu, barabara, bandari, ujenzi wa barabara mpya na kongwe, huduma za afya, maji pamoja na mafanikio yalipatikana. Alielezea azma yake ya kuimarisha sekta ya elimu ikiwa  ni rejea kujenga skuli mbili kubwa za Sekondari, Chuo Kikuu, ambayo atayafanya kipindi kijacho na kuwaomba wanaCCM na wananchi kukiamini chama hicho kwa yale yote aliyoyanadi. Sifa nyengine kubwa ya CCM ni kuwa imetokana na TANU na ASP na baadae kuwa CCM huku akieleza kuwa nchi mbili nazo ziliungana na kufanya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo yote hayo aliyanadi nfdani ya mwezi mmoja na siku 9. Alisema kuwa akichaguliwa tena atatekeleza Ilani hiyo kama alivyotekeleza Ilani ya miaka mitano iliyopita. Dk. Shein alisisitiza suala zima la amani na utilinu na mshikamano ambayo yote amesimamiwa na Ilaini ya CCM na sera sahihi ya chama hicho kwani CCM inaamni kuwa hayo yote ndio msingi wa maendeleo na Tanzania. 
Alisema kuwa Zanzibar na Tanzaia nzima inaheshimika na kupewa heshima na Jumuiya ya Kimataifa kwa utulivu na umoja na ndio maana wataalii wengi wanakuja Zanzibar na Tanzania na wakubwa wengi wa duniani wanakuja kutembea Zanzibar na hayo yote yanatiokana na usimamizi wa CCM. Alisema kuwa Idara za SMZ zimekwua zikishiriki kikamilifu katika kulinda amani iliyopo na kuwahakikishia wananchi na wanaCCM kuwa uchaguzi wa mwaka huu utawakuwa huru na haki ambao utakuwa  wa amani.  
Aliwahakikishia kuwa ulinzi utakuwepo wa kutosha kw awananchi na mali zao kwani ulizni wa kutosha upo na kama yupo mtu atathubutu na afanye ataona. 
Alisema kuwa nchi hii inaamni  utawala wa Katiba na Utawala Bora, na kusema kuwa SMZ imeendeshwa kwa lengo la kuwatumikia Wazanzibari wote na hakuna aliyebaguliwa na kubezwa licha ya wale waliokuwemo Sertikali ambao walisema kuwa SMZ ina wadhulumu. "Serikali hii inawapenda watu wote na wanaosema hivyo na nitaendelea kusimamia Serikali yenye kusimamia maadili",alisema Dk. Shein.   
Aliwapomgeza vyombo vya Dola vya SMZ na vya SMT kwa kulinda amani na kusema kuwa ndio maana katika Kampeni aliahidi kuwaongezea mishahara Idara zote za SMZ ili walingane na vikosi vya SMT.  
Alieleza miongoni mwa azma yake ikiwa ni psamoja na Kupambana na umasikini, hasa kuwawezesha vijana, kupambana na kupamvana rushwa na kuimarisha uchumi huku akiwataka wananchi na wanaCCM kujenga imani kwa CCM pamoja na wagombea wake wote wa uongozi ili wasaidiane katika kuijenga nchi.  
Dk Shein alisema kuwa yeye yuko tayari kuwatumikia wananchi wa Zanzibar na kusisitiza kwua Zanzibar itajengwa kwa nguvu mpya na mipango mipya na kusisitiza kuwa uwezo wa kuijenga Zanzibar kwa mipango hatua kwa hatua upo.  
Alisema kuwa azma za kujenga miji ipo kama ilivyoahidiwa Mji wa Matembwe na Fumba na mipango mipya ya kujengwa mji mpya wa Kisiwandui, Kisimamajongoo na sehemu nyenginezo na baadae Mkokotoni na kueleza kuwa baada ya miaka mitano wananchi wataona mabadiliko hatua kwa hatua. 
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akitoa salamu za ndugu zao wa Tanzania Bara alisema kuwa  hiyo ni nafasi adhimu ambayo haijawahi kutokezea ndani ya Tanzania na hayo ndio mabadiliko. Alisema kuwa tokea kuanza kwa kampeni amefanya mikutano nchini ipatayo 343 amemaliza vyema na amerudi akiwa mzima wa afya na kuomba kupewa kura ili wawatumikie wananchi. Alisema kuwa Ilani ya CCM imetambua makundi yaliopo Tanzania yakiwemo vijana na wanawake na kusema kuwa jitihada za makusudi zimefanywa na SMZ na SMT kwa kujenga miundombinu Tanzania nzima pamoja na kuweka mitaji ili kujiendeleza kimaisha sambamba na kuleta tija kwa Taifa. Alisema kuwa imerahisisha usafiri wa watu na bidhaa kwa usafiri na mwasiliano ya barabara, fursa za biashara na kuwajenga vijana kimapato ili waweze kujitegemea na kwa CCM vijana ni rasilimali ambayo inahitaji kujenga nguvu kwa Taifa. Samia aliwatakaka vijana kuwa na tahadhari na wasikubali kufanywa daraja katika kutenda mambo maovu. Alisema kuwa CCM imejipanga inampango kazi na Ilani na kusisitiza kuwa  chama hicho kina mfumo unaoelekeweka kwani wagombea wake wamepatikana ndani ya CCM na wamechujwa na kupatikana wanaofaa.Alisema kuwa wapinzani bado hawajawa makini kupewa watanzania kuwaongoza na rasilimali zao na kutaka  wapuzwe. Alisema kuwa CCM kina dhamira ya dhati ya kutunza na kuezai Mapinduzi nakudumisha Mapinduzi na Muungano na wengine hawana imani na Mapinduzi na Muungano wa Tanzania. Mgombea Mwenza huyo wa CCM alisema kuwa CCM ndicho chama chenye uzoefu wa kuiongoza Tanzania kwani ina kila sababu ya kupewa uongozi. Samia aliwataka wanaCCM na wananchi kwenda kuchagua watumishi wa watu na sio watawala wa watu na kuomba kupewa kura ili kuleta maendeleo, na kusema kuwa aliopewa nafasi ni mwanamke wa Tanzania na sio Samia Suluhu hivyo kuna kila sababu ya kuichagua CCM. "Tupeni kura zote mimi kama mama sitawaangusha na tupeni kura ili kuonesha kuwa wanawake wakipewa nafasi wanaweza",alisema Samia.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal alisema kuwa kinachotakiwa ni kuhakikisha kuwa Chama Cha Mapinduzi kinaendelea kupata ushindi wa kishindo. Alisema kuwa CCM imeleta mabadiliko katika nyoyo na imani kwa kumuweka mgombea mwenza Mama Samia Suluhu Hassan.Bilal alisema kuwa kura za wanaCCM zitalindwa na Mawakala wa CCM pamoja na vyombo husika na kuwataka wanaCCM wasiwe na wasi wasi kwani ushindi hauepukiki kwa chama hicho huku akiwaeleza kuwa wataendelea kulindwa.
 Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd alisikitishwa na kauli za viongozi wa CUF za kusema kuwa watawaficha watoto wa wanaCCM ili wazazi wao wahangaike na wasiende kupiga kura. Alisema kuwa Ikulu ni ya wananchi wa Zanzibar hivyo wao ndio wanaoamua ni nani aende Ikulu kwani Ikulu watu hawendi kwa nguvu. 
Balozi Seif alisema kuwa mtu fitina hawezi kuongoza nchi pamoja na kueleza kuwa uongozi hauhitaji ushikina bali ni chaguo la Mwenyezi Mungu pamoja na wananchi.Aliwaeleza wanaCCM kuwa wakapige kura kwa salama na amani bila ya hofu yoyote kwani vyombo vya Dola viko macho.

          Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi alisisitiza 
    suala zima la amani nchini na kusema kuwa Watanzania hasa Wazanzibari  ni watu        wanaopenda amani.Serikali ya CCM imeleta maendeleo na kufanya mambo kuwa mepesi      kwa wawekezaji na kuendelea kuwa kivutio kwa watalii sambamba na  kuimarisha sekta        za  maendeleo.

Mama Fatma alisikitishwa na mambo yanayofanywa na chama cha CUF cha kumuweka Seif Sharif na Mzee Abeid Amani Karume kwenye picha ya pamoja katika bango la Kampeni la chama hicho. Mama Fatma alisema kuwa Kama Mansour anataka kupata kura kwa nini asiweke pisha ya Baba yake Yussuf Himid na Maalim Seif lakini alisema kuwa amefurahishwa kwa kusikia kwamba wenyewe waasisi wa Afro Shirazi  watalichukulia hatua suala hilo. Alisema kuwa Wazanzibari wana uwamuzi wao  ambao watautumia siku ya tarehe 25 mwezi huu kwa kuichagua CCM. Aidha, aliwatahadharisha wanaCCM kutokichagua chama cha CUF kwani kikiingia madarakani hakitokubali kutoka tena.


TUNATOA SHUKRANI ZA DHANI KWA WANANCHI WA KISIWA CHA PEMBA KWA  UPENDO MLIOUNESHA KWA WAGOMBEA UONGOZI WA RAIS WA MUUUNGANI DR  JOHN MAGUFULI, MGOMBEA MAMA SAMIA SULUHU NA MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR DR ALI MOHAMED SHEIN. KWA KUJA KWA WINGI KATIKA MIKUTANO YOTE YA KAMPENI ILIOFANYIKA KISIWANI HUMU NA HUU WA LEO WA KUFUNGA KAMPENI NA KUDHIHIRISHA UMMA KUWA KWELI MMEKUBALI KUONGOZWA NA VIONGOZI KUTOKA CHAMA CHA MAPINDUZI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza na Maelfu ya wanachama cha Mapinduzi CCM  na wananchi wa Kisiwani Pemba katika mkutano wa kufunga
 kampeni za Chama hicho katika uwanja wa Gombani yakale leo
   na kuwaombea kura wagombea wote wa CCM,

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete alisema kuwa CCM itaendelea kuongoza Jamhuri ya Tanzania na pamoja na Zanzibar na kuwaombea kura wagombea wote wa CCM. Aliwataka wananchi na wanaCCM kukichagua chama hicho kwani kimeongoza vizuri kwani nchi iko salama na imetulia na watu wanafanya shughuli zao bila ya bughuza na kueleza kuwa kama ingeongozwa vibaya hatua hiyo isingelifikia. Alisema kuwa kuna kila sababu ya kumchagua Dk. Shein kuwa Rais wa Zanzibar kwani Zanzibar iko salama na ameiongoza kwa umakini sana na kwa upande wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Dk. Shein amekuwa makini katika serikali hiyo na kama si umakini wake hata miaka mitano isingelimaliza. Alisema kuwa ameongoza kwa umakini Serikali hiyo na kusisitiza kuwa maendeleo yapo yanatyoonekana katika kila nyanja kwenye sekta zote na hata kwenye vipato vya watu. Rais Kikwete alisisitiza kuwa hakuna mbadala wa Dk. Shein, na Maalim Seif si mbadala wa Dk. Shein kwani Maalim Seif angezoza Serikali hiyo hata siku tatu zisingefika kwani si mstahamilivu. Alisema kuwa kiongozi huyo wa upinzania katika lugha zake anazozungumza haunganishi watu badala yake anawachonganisha na kusisitiza kuwa Dk. Shein ndio anaeweza kufanya kazi ya urais wa Zanzibar.  Rais Kikwete aliwataka wananchi na wanaCCM wamchague Dk. Shein pamoja na Wawakilishi, Wabunge na Madiwani wengi wa CCM ili aweze kuongoza vizuri, na wengine waendelee kuwa washiriki. Alisema kuwa kwa upande wa mgombe nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, John Pombe Magufuli,  hilo ndio chaguo la wengi na kueleza kuwa wapinzani wake hivi sasa wamekalia kuti kavu na kuwataka wananchi wakitaka mambo mazuri kwa kuitaka Zanzibar na Tanzania kwa jumla ziendelee kustawi na kuwa na maendeleo wawachague Dk. Shein na Magufuli.Alieleza kuwa CCM katika kumteua John Magufuli  haikufanya kosa kwani ni muadilifu kwani angekuwa na tatizo lolote la uadilifu asingelipata nafasi hiyo. Alisema kuwa Dk. Magufuli ni hodari, muaminifu, muadilifu na wanaomsema vibaya ni wale waliojaa hofu katika maisha yao ya ujanja ujanja. Alisema kuwa katika Wizara zote alizofanya kazi Magufuli,amethibitisha ukomavu wake pamoja na ujasiri na mvumilivu wake sambamba na hayo ni muumini wa  Muungano wa Tanzania na mpenda maendeleo kwani katika hotuba zake anaonesha jinsi anavyokereketwa na maendeleo na iwapo atapewa nafasi hiyo mafanikio makubwa yatapatikana Tanzania. Dk. Kikwete alisema kuwa Magufuli anaamini umoja na tokea ameanza Kampeni zake hajajinadi juu ya dini yake wala ukabila wake na kusema kuwa Tanzania inataka kiongozi anaesema mamenao yake akayaamini yeye mwenyewe.  
Alisisitiza kuwa uchaguzi utakuwa wa amani, na kueleza kuwa anaetayaarisha matayarisho ya Uchaguzi ni Tume ya Uchaguzi, na Serikali kazi yake ni kuwapa fedha kwa ajili ya shughuli zao lakini kuhakikisha kuna amani na utulivu siku ya kupiga kura ni jukumu la Serikali na yeye ndio amiri Jeshi Mkuu. "Tutahakikisha kuwa uchaguzi utakuwa wa amani na utulivu na anayetaka kufanya majaribio ya utayari wetu na ajaribu, natakata Watanzania wapate fursa ya kuwachagua viongozi wanaotaka",alisema Dk. Kikwete. "Tarehe 25 jitokezeni hakutatokea lolote...kuungana kwa vyama vinne ndio kuonesha dalili za kushindwa"alisema Rais Kikwete.Aliwataka wanaCCM na wananchi kujitokeza kwenda kupiga kura na hakutatokea lolote na atakae jaribu ataona na kutumia fursa hiyo kuwaombea kura kutaka kupewa kura Dk. Shein, Dk. Magufuli, Samia, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwahutubia maelfu ya wanachama cha Mapinduzi CCM  na wananchi wa Kisiwani Pemba katika mkutano wa kufunga kampeni za Chama hicho katika  uwanja wa Gombani yakale leo pamoja na kuwaomba kura wananchi
 pia na kuwaombea Kura wagombea wa Chama hicho.

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  amemuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungao Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuwathibitishia wananchi na wanaCCM kuondoa shaka na hofu kwani Serikali yao ipo na itaendelea kuwalinda siku ya uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. 
Dk. Shein ambaye ni Mgombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM aliyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye mkutano wa kufunga Kampeni ya chama hicho uliofanyika huko katika viwanja vya Gombani ya Kale, Chake Chake, Pemba uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi na wanaCCM. Dk. Shein alitoa shukurani kwa wanaCCM na wananchi kwa kuhudhuria kwa wingi katika mikutano yote tokea tarehe 13 mwezi huu zilipozinduliwa Kampeni za chama hicho. Alisema kuwa katika mikutano hiyo ahadi kwa kila Jimbo, Wilaya hadi Wadi zilitolewa kwa mujibu wa utekelezaji wa Ilani ya CCM pamoja na kuelezea mambo makubwa kwa Zanzibar. Alisema kuwa katika miaka mitano ijayo baada ya kuchaguliwa yeye na chama chake atayatekeleza yale yote yalioahidiwa na chama chake. Dk. Shein aliahidi kutokana na Ilani ya chama hicho kuendeleza kusimamia  amani, utulivu na umoja kwani ndio njia pekee ya kuleta maendeleo. "Anaezania ni zihaka na anataka kufanya fujo ajaribu aone",alisema Dk. Shein. Akilizungumzia suala la karafuu, Dk. Shein alisema kuwa Ilaini ya CCM kama iluvyoelekeza mwaka 2010, Serikali ya SMZ italiendeleza zao la karafuu na halitobinafsishwa na kuwataka wananchi wa Pemba wasikubali kurejeshwa nyuma kwani wanapata asilimia 80 ya soko la dunia la karafuu zao wanazoziuza na Serikali italiendeleza zao hilo. Alirejea ahadi yake ya kuwa endapo bei ya zao hilo itaendelea kuwa hivyo hivyo katika soko la dunia bei ya karafuu ataiongeza hadi kufikia kilo elfu 20,  badala ya elfu 14 ya bei ya sasa.Alisema kuwa alitangaza kuwa siku ya tarehe 12 Januari mwaka huu, kuwa atafuta michango yote ya elimu ya msingi kuanzia Julai mwaka huu na katika Kampeni hizi alisema kuwa mitihani ya kidatu cha nne na Sita nazo ameamua wazee wasichangie atakapoingia madarakani. Pia, arijea kauli yake kuwa mwaka wake wa mwanzo ataondoa michango ya Sekondari na kueleza kuwa  mwaka wa Pili katika uongozi wake atatangaza huduma za afya bure na kusema kuwa afya na elimu itakuwa bure kama alivyoasisi Mzee Karume kwani uwezo upo. Dk. Shein baada ya kusema hayo alishangazwa na vyama vya upinzani kuhemkwa na kuiga kwa kila analoliahidi. Alisema kuwa lengo la Serikali ni kuimarisha zaidi huduma za maji safi na salama ambazo kwa sasa ni alisilimia 87.7, kwa mijini na alisimia 70 vijiji, na kueleza lengo ni kufikia asilimia 97 mijini na  80 kwa vijiji na hilo linawezekana. Aidha, Dk. Shein alieleza jinsi alivyojiandaa na suala la ajira kwa vijana sambamba na mikakati ya ujenzi wa vyuo vya amali kikiwemo kitakachojengwa huko Mtambwe kwa Pemba na Makunduchi kwa Unguja. Pamoja na hayo, alisema kuwa Unguja na Pemba ni visiwa vilivyozungukwa na bahari na asilimia ya watu wake wengi ni wavuvi na kusema kuwa Serikali atakayoiongoza itaimarisha uvuvi wa bahari kuu kwa mashirikiano ya  Serikali mbili kwa nguvu zote ili kuitumia bahari kuu kwa kuweka miradi ikiwa ni pamoja na kuwakaribisha wawekezaji ili itoe tija ambapo Makao Makuu yake hivi sasa yapo Fumba Zanzibar. Dk. Shein, aliwataka wana CCM na wananchi kuwachagua viongozi wa CCM, Pia, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa shukurani kwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwa mashirikiano makubwa aliyompa tokea wakiwa wote Mawaziri sambamba na kuusimamia Muungano katika kipindi chake chote cha urais. Dk. Shein alisema kuwa Dk. Kikwete ametoa mchango mkubwa sana katika kuendeleza suala la mafuta na gesi kwa upande wa Zanzibar na kuwataka wananchi na WanaCCM kwenda kupiga kura kwa lengo la kuyalinda Mapinduzi pamoja na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Alisema kuwa yuko tayari kuiongoza Zanzibar na afya yake inamruhusu na kusisitiza kuwa mafanikio yote tokea 1964  yamefanywa kwa pamoja na kuwaeleza kuwa bila ya CCM yote hayo yasingelipatikana huku akiwaeleza wananchi kuwa  viongozi wa upinzani hawana vipaji vya kuongoza.
 Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Samia Suluhu Hassan akizungumza na Maelfu ya wanachama cha Mapinduzi CCM  na wananchi wa Kisiwani Pemba wakati alipokuwa akiomba kura pamoja na kuwaombea wagombea wengine wa CCM akiwemo Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano Dkt.John Pombe Magufuli katika mkutano wa kufunga kampeni za Chama hicho
 uliofanyika leo katika uwanja wa Gombani yakale.


Mgombe Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akitoa salamu za ndugu zao wa Tanzania Bara alisema kuwa wao wanasema kuwa CCM mbele kwa mbele na kusema kuwa Pemba ya 2010  si ya leo. Alisema kuwa CCM mwaka huu wameamua kutimiza nembo ya Serikali ya Adama na Hawa na kusema kuwa Adama na Hawa ni Magufuli na Samia na wako yatayari kukabidhiwa Tanzania na mali asili zake kwa lengo la kuitumikia. Aliwakataka akina mama bila ya kujali vyama vyao wapige kura CCM kwa sababu CCM imeamua mwaka huu kumpa heshima kubwa mwanamke kuwa Mgombea Mwenza. Aliwataka akina mama kukamatana na kuuonesha ulimwengu kuwa wanawake wakipewa nafasi wanaweza kuiongoza Tanzania. Aliishukuru amwamu ya nne ya Urais wa Dk. Kikwete kwa kujenga miundombinu kwa kutoa fursa kwa ajira na kusema kuwa Tanzania nzima imeunganishwa kwa barabara za lami na kueleza kuwa zikitoa huduma na kuwawezesha wananchi kusafirisha bidhaa zao, sambamba na kuinuka  kwa soko la ajira.  
Alisema kuwa Ilani ya CCM imeonesha jinsi vijana wa wanawake walivyopewa kipaumbele ili kuweza kupata fursa na kueleza kwa upande wa walemavu nao watapewa nafasi bila ya ubaguzi. Kwa upande wa wazee alisema kuwa, wazee wote ambao walikuwa wakulima na hawapati mafao watapewa sawa na wale waliokuwa wakifanya kazi Serikalini ambapo tayari kwa upande wa Zanzibar mchakato huo umeanza. Alisema mkuwa CCM ina mpango kazi kwa yale yote ambayo yatafanywa katika awamu na kuonesha kuwa rasilimali fedha za kuendeleza ahadi hizo zitapatikana. Alisema kuwa CCM ina mfumo na muuundo unaoelekewaka na kusisitiza kuwa mchakato ulioendeshwa katika chama hicho hadi kupatikanwa kwa wagombea na tofauti na jinsi walivyopatikana wagombea katika vyama vyengine vya siasa ambao ni wasanii na kusisitiza kuwa wapewe kura CCM wenye uzoefu wa kuongoza.Samia alisema kuwa katika kuendesha Serikali hawezi kupewa mtu ambae sifa zake hazina uwezo, alisema kuwa CCM ina lengo la kulinda na kudumisha Mapinduzi na Muuungano wa Jamhuri ya Tanzania. Mgombea huyo Mwenza wa CCM alisema kuwa ili walinde usalama wa Tanzania pamoja na kulinda Muungano na kwa umoja watu waweze kuishi kwa kusikilizana na kupendana. "Watanzania hawako tayari kuwapa kura wasanii"alisema Samia.



Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif  Ali Iddi akiwahutubia wananchi waliojaa katika uwanja 
wa  Gombani ya Kale katika ufungaji wa kampeni ya urais .

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd akitoa salamu kwa wananchi aliwataka wajiandae kwa ushindi wakiwemo akina mama kwa kupaka hina na kutia wanja kusubiri ushindi wa CCM. Alisema kuwa chama cha CUF katika uchaguzi wa mwaka huu kitashindwa na Katibu Mkuu wake utakuwa ndio mwaka wake wa mwisho wa siasa kama alivyoeleza mwenyewe aliposema kuwa hata Ukatibu Mkuu wa chama hicho anauwacha. 
Alisema kuwa viongozi wa CUF wamekuwa wakiwadanganya sana wananchi na kuendedelea kueleza kuwa wafuasi wa chama hicho wamejiandaa kuleta vurugu na wamejiandaa kuleta mamluki kutoka nchi jirani kwa lengo la kuja kufanya vurugu kisiwani humo. Kwa upande wa Unguja alisema kuwa tayari Serikali imeshapata taarifa kuwa kuna watu wamejificha kwenye nyumba ya kiongozi mmoja wa chama hicho huko Mombasa Unguja kwa lengo la kuja kufanya fujo siku ya uchaguzi na kusema kuwa hawatahi kufanya kwani taarifa zipo na watashughulikiwa na vyombo husika. Aliwataka wanaCCM na wananchi kutoogopa kwenda kupiga kura kwani ulinzi utawekwa kila mahala ili kuhakikisha kila mtu mwenye haki ya kupiga kura anapiga kura kwa kupata haki yake hiyo ya msingi.Balozi Seif alisema kuwa matusi anayotukanwa na viongozi wa CUF jibu lake ni siku ya tarehe 25 siku ya kupiga kura. Aidha, Balozi Seif alisema kuwa wenye familia ya Marehemu Mzee Karume hawataki kubandikwa picha zilizowekwa na CUF zinazomuonesha Maalim Seif na Marehemu Mzee Abeid Karume zikimuonesha Maalim Seif akisema kuwa atavaa viatu vya muasisi huyo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alitoa shukurani kwa washiriki na jamii yote waliotoa misaada yao mbali mbali katika Kampeni hiyo  kwa  chama hicho kutokana na mashirikiano makubwa waliyoyatoa wananchi, wanaCCM, wasanii, waandishi wa habari na wengineo. Vuai alisema kuwa Dk. Shein hana ubaguzi, hana choyo na muumini wa CCM ameweza kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar, huku akimpongeza Dk. Jakaya Marisho Kikwete alimpongeza kwa kusimamia vyema kuondokana na migogoro ya Zanzibar. Naibu Katibu Mkuu huyo, aliwataka wanaCCM kutochokozeka kwani wafuasi wa chama cha CUF wameamua kwa makusudi kufanya vurugu kwani wameshajua kuwa watashindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mberwa Hamad aliwaeleza wanaCCM kuwa ushindi kwa chama hicho hauepukiki katika uchaguzi wa mwaka huu hivyo aliwaondoa hofu na kuwataka kwenda kuwachagua viongozi wa CCM siku ya Jumaapili ya tarehe 25, Oktoba mwaka huu.
UZINDUZI WA UMEME KATIKA KIJIJI CHA KIJINI MATEMWE  KATIKA SHEREHE ZA  UFUNGUZI WA UMEME KATIKA KIJIJI  CHA MATEMWE MBUYUTENDE NA KIJINI,WILAYA YA KASKAZINI A MKOA WA  KASKAZINI UNGUJA. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kama ishara ya Ufunguzi wa Umeme katika kijiji cha Matemwe Mbuyutende na Kijini,Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa kaskazini Unguja leo (kushoto) Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar  (ZEC) Hassan Ali Mbarouk,
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiponyeza kitufe  kama ishara ya Uzinduzi  wa Umeme katika kijiji cha Matemwe Mbuyutende na Kijini,Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa kaskazini Unguja leo (kushoto) Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar  (ZEC) Hassan Ali Mbarouk,(kulia) Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi (wa pili kuli).

 WEKA ALAMA YAKO YA KURA KWA DR. ALI MOHAMED SHEIN. 
CHUMBA NAMBA SITA. ANGALIA KWA UANGALIFU.
 Baadhi ya wananchi wa Vijiji vya Matemwe Mbuyutende na Kijini wakimsikilizaRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipokuwa akitoa hutuba yake katika sherehe za uzinduzi wa Umeme katika vijiji hivyo leo katika Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa kaskazini Unguja, 

 MAMA MWANAMWEMA SHEIN AMBAE NI MKE WA MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KWA TIKET YA CCM DR.ALI MOHAMED SHEIN AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA UWT WILAYA YA MICHEWENII PEMBA.

MKE wa Rais wa wa Zanzibar mama Mwanamwema Shein akiwahutubiai viongozi wa UWT Pemba .






AHSANTENI WANANCHI WA JIMBO LA DIMANI 
KWA KUJA KWA WINGI KUHUDHURIA MKUTANO 
 NA KAMPENI NA KUMSIKILIZA MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KWA TIKET YA CHAM CHA MAPINDUZI
 DR. ALI MOHAMED SHEIN. TUNAKUOMBENI MJE KWA WINGI MNO SIKU YA UFUNGAJI WA KAMPENI.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwahutubia wananchi na WanaCCM katika Mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Jimbo la Dimani Mkoa wa Mjini Magharibi  Unguja  katika uwanja wa mpira wa Dimani leo,

VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamewaeleza wanaCCM na Wananchi kuwa hakuna chama chenye historia,kujali maslahi na maendeleo ya wananchi isipokuwa CCM hivyo kuna kila sababu ya wao kuwachagua viongozi wa chama hicho wanaogombania nafasi za uongozi. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano wa Kampeni ya uchaguzi wa CCM uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi na wanaCCM uliofanyika uwanja wa Mpira Dimani, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo mgeni rasmin alikuwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk. Ali Mohamed Shein.   
Nae Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mohammed Seif Khatib alisema kuwa hakuna chama hata kimoja chenye historia ya ukombozi isipokuwa chama cha CCM ambacho kinawajali na kinawathamini wananchi. 
Alisema kuwa CCM ina Sera thabiti kwani inayatambua na inayathamini Mapinduzi ya Januari 12, 1964 ambapo pia, chama hicho kimezaa Muungano ambao umeleta umoja na mshikamano hadi hivi leo.  
Alisema kuwa CCM ina kila sababu ya kuingia Ikulu kwani mgombea wake wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali Mohamed Shein ana kila sifa, elimu ya juu ya Sayansi, ana Digirii tatu, mtu wa watu, mpole na myenyekevu na anawapenda Wazanzibari, si mbaguzi.  
Nae Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Idd alisema kuwa uhuru wa Zanzibar umepatikana kutokana na wakulima na wakwezi hivyo hashangazwi na viongozi wa chama cha CUF kumwambia kuwa andapo watapa nchi akatafute jembe akalime. 
Balozi Seif pia, alishangazwa na chama cha CUF kusema kuwa Zanzibar hakuna maendeleo na kueleza kuwa maendeleo yaliopo hivi sasa hawayaoni. 
Balozi Seif alisema kuwa tayari kuna baadhi ya wafuasi wa chama cha CUF wameshadhamiria kufanya fujo na hivi sasa tayari wameshawahamisha watoto wao kuwapelekea Pemba ili wao wabakie kwa lengo la kufanya vurugu. 
Alisema kuwa Chama cha CUF kimejiandaa kuwadhibiti wafuasi wa CCM siku ya uchaguzi na kueleza kuwa CCM imeshapata habari na vyombo vinavyohusika katika kusimamia amani na utulivu vitawashughulikia wale wote watakao leta vurugu. 
Aidha, Balozi Seif alitumia fursa hiyo kuwaombea kura wagombea wote wa CCM. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alitoa pongezi kwa wanaCCM kwa kushiriki vyema katika mikutano ya chama hicho na kueleza kuwa kuna kila sababu ya ushindi wa CCM. 
Nae Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Magharibi, Yussuf Mohammed, alisema kuwa CCM itashinda kwa ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. 
Alisema kuwa uwanja wa mpira wa Bweleo umetengezwa na Serikali ya CCM na kushangazwa  na ahadi zilizotolewa na viongozi wa CUF kujenga uwanja huo ambapo ahadi hizo zote zilikuwa hewa na badala yake Serikali chini ya CCM umekijenga kiwanja hicho. 
Alisema kuwa Mapadri, Maaskofu na Wachunganyi amani yao iko kwa CCM na sio chama cha CUF kwani chama hicho hawana imani nzuri na watu wa dini ya Kikiristo kutokana na maovu mbali mbali waliowafanyia watu wa dini hiyo hapa nchini.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akiwaombea kura Viongozi wa CCM walioomba nafasi za Uongozi katika kamapeni za CCM zilizofanyika leo katika uwanja wa mpira Dimani Wilaya ya Magharibi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Jimbo la Dimani,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shei,
Nd. Wana CCM fateni maelekezo alioyaeleza Naibu Katibu Mkuu CCM , Nd. Vuai Ali Vuai. kuhusu kupiga kura. Fata  hatua  hizi  chini
 1. Unachukua
 2. Unaaangalia chumba namba 6 hakikisha mgombea awe Dr Ali Mohamed Shein 
 3. Unaweka.
 Ahsanteni sana. Kama inavyojionehsa hapo juu.


 Maelfu ya Wananchama wa CCM na Wananchi waliohudhuria katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM Jimbo la Dimani Wilaya ya Magharibi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakisikiliza sera zilizotolewa na Viongozi   katika mkutano huo mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.
 Maelfu ya Wananchama wa CCM na Wananchi waliohudhuria katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM Jimbo la Dimani Wilaya ya Magharibi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipozungumza nao leo.

Baadhi ya wanaCCM waliohudhuria katika Mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Jimbo la Dimani Mkoa wa Mjini Magharibi  Unguja wakimskiliza mgeni rasmi katika mkutano huo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza  nao leo katika uwanja wa mpira wa Dimani leo.




  

AHSANTENI WANANCHI WA JIMBO LA MAKUNDUCHI 
KWA KUJA KWA WINGI KUHUDHURIA MKUTANO 
 NA KAMPENI NA KUMSIKILIZA MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KWA TIKET YA CHAM CHA MAPINDUZI
 DR. ALI MOHAMED SHEIN.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwahutubia wananchi na WanaCCM katika Mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Mkoa wa Kusini Unguja Jimbo la Makunduchi katika uwanja wa mpira wa Jamhuri leo,
Mgombea nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wananchi wa Zanzibar kuzingatia na kuthamini historia ya ukombozi wao kwa kukichagua tena chama hicho na wagombea wake ili kukusanya nguvu kuendelea kuijenga Zanzibar na Tanzania.
“Tuzingatie historia yetu, tuangalie tulikotoka, tulipo na tunakokwenda kwa kukichagua Chama cha Mapinduzi kilicholeta ukombozi wetu” Dk. Shein alisema.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni huko Jang’ombe katika jimbo la uchgauzi la Mpendae, mjini Unguja, Dk. Shein aliwahakikishia wananchi hao kuwa dhamira yake ya kuwatumikia iko pale pale na kwa nguvu zote.
 “nichagueni mimi na wagombea wenzangu wa CCM na mimi nawaahidi nitaendelea kuwatumikia kwa nguvu zangu zote na mkinichagua nitahakikisha yote ninayowaeleza katika kampeni zangu nitayatekeleza” Dk. Shein aliongeza.
Aliwaambia mamia na wananchi waliohudhuria mkutano huo kuwa serikali atakayoingiza katika kipindi kijacho itaendelea na mipango ya kuimarisha huduma za jamii ikiwemo katika jimbo hilo ambapo kwa mujibu wa maelezo yake ahadi alizozitoa katika mkutano kama huo mwaka 2010 wakati akiomba kura asilimia kubwa amezishazitekeleza na baadhi utekelezaji wake ndio unaendelea au utaanza hivi punde.

“katika kipindi kilichopita tumeweza kuongeza kiwango cha upatikanaji maji katika mkoa mzima hadi kufikia asilimia 87 kutoka asilimia chini ya 67”alieleza Dk. Shein na kuongeza kuwa ahadi ya ujenzi wa skuli ya ghorofa na ya kisasa pamoja na kituo cha afya katika jimbo hilo umetekelezwa.
Alifafanua kuwa katika kipindi kijacho ataongeza kasi ya uimarishaji wa miundombinu ya barabara ambapo barabara zinazoingia mjini Unguja karibu zote zitajengwa upya kwa kiwango cha lami.
Alizitaja barabara hizo kuwa ni pamoja na kutoka Badarini (Malindi)-Kinazini hadi Bububu yenye urefu wa kilomita 11.2, Malindi (kupitia Darajani)-Mkunazini hadi Mnazi Mmoja yenye urefu wa kilomita 1.3,Tunguu-Fuoni-Magomeni-Kariakoo yenye urefu wa kilomita 16.3, Welezo hadi Ng’ambo kupitia Amani kilomita 2.9 na Uwanja wa Ndege-Kiembesamaki-Kilimani hadi Mnazi Mmoja yenye urefu wa kilomita 6.6.
Katika mkutano huo mgombea huyo wa CCM alieleza kuwa Ilani ya CCM katika kipindi kijacho imeielekeza Serikali kuimarisha karakana yake ili iwe ya kisasa hata kama ni kwa kushirikiana na sekta binafsi ili vyombo vya serikali viweze kufanyiwa matengenezo yote katika karakana hiyo.
Dk. Shein alifafanua kuhusu mradi wa usafi wa mazingira katika miji ya Unguja na Pemba ambao umegharimu serikali dola milioni 36. Alibainisha kuwa mradi huo utekelezaji wake umeanza sehemu zote 4 za mradi huo zimeanza kutekelezwa.
Alizitaja kazi hizo kuwa ni ujenzi wa ukuta wa Forodhani ambao unazuia maji ya bahari kuingia katika maeneo juu na ujenzi wa mtaro mkubwa wa kuondoa maji ya mvua kuhami maeneo ya Jang’ombe kujaaa maji na ujenzi wa mtaro wa Shaurimoyo hadi Gulioni-miadi ambayo itaanza kutekelezwa mwezi Disema.
Kazi nyingine ni kuingiza magari ya kusafisha mji na vifaa vya usafi pamoja na kujenga maeneo ya kukusanyia taka. Chini ya mradi huu alisema sehemu mpya ya kubwa ya kutupia taka katika eneo la Kibele limetengwa na kuandaliwa.
Dk. Shein ambaye anagombea tena nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka 5 aliwaeleza wananchi kuwa tatizo la kujaa maji katika viwanja vya Mnazi Mmoja linafanyiwa kazi ambapo mfumo mpya wa kuyatoa maji ya mvua na ya bahari umeanza kutekelezwa hivyo kuwahakikishia kuwa viwanja hivyo vitarejea katika hali yake ya zamani.
Aliwaomba wananchi kuwachagua wagombea wa CCM katika nafasi zote kuanzia ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, wabunge, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na madiwani.
Dk. Shein ataendelea na kampeni zake kesho ambapo atahutubia mkutano mkubwa wa kampeni huko Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja.

Maelfu ya wanaCCM waliohudhuria katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM uliofanyika leo katika uwanja wa mpira wa Jamhuri Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja Jimbo la Makunduchi wakimskiliza mgeni rasmi katika mkutano huo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza  nao.
 Baadhi ya wanaCCM waliohudhuria katika Mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM wakimskiliza mgeni rasmi katika mkutano huo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Sheinalipokuwa akizungumza  nao leo katika uwanja wa mpira wa Jamhuri MakunduchiMkoa wa Kusini Unguja Jimbo la Makunduchi ,




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi kombe la Mchezo wa fainali ya Zanzibar Cup 2015 Mpira wa Miguu Nahodha wa Timu ya Wilaya ya Mjini Abubakar  Ameir Omar uliochezwa katika uwanja wa Amaan Studiuam Mjini Unguja jana,Mchezo huo ulimalizika kwa Wilaya ya Mjini kuwafunga W/Magharibi kwa matuta 3-1.
AHSANTENI WANANCHI WA JIMBO LA MPENDAE 
KWA KUJA KWA WINGI KUHUDHURIA MKUTANO 
 NA KAMPENI NA KUMSIKILIZA MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KWA TIKET YA CHAM CHA MAPINDUZI
 DR. ALI MOHAMED SHEIN.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia  Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wana
CCM na Wananchi wa Jimbo la Mpendae  katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM uliofanyika leo katika uwanja wa Binti Amran  Mkoa wa Mjini Magharibi  Unguja.
WANACCM wametakiwa kuendelea na uvumilivu wa kisiasa  na kusikiliza maelekezo ya viongozi wao katika kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi Mkuu ambapo chama kikuu cha upinzani CUF kimedhamiria kufanya vitimbi mbali mbali vya kuvuruga amani na utulivu ili uchaguzi huo usifanyike jambo ambalo haliwezekani.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano wa Kampeni ya uchaguzi wa CCM uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi na wanaCCM uliofanyika katika viwanja vya Kwabitihamrani, mjini Zanzibar leo, viongozi wa CCM walisema mbinu hizo za upinzani kamwe haziwezi kufanikiwa kwani ushindi wa CCM umeonekana wazi katika maeneo yote ya Unguja na Pemba. 
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alisema kuwa CCM inatoa shukurani maalum kwa wanaCCM wa Zanzibar kwa kuhudhuria kwa wingi katika mkutano wa CCM ambapo Dk.Magufuli alikuwa mgeni rasmin. 
Alisema kuwa mahudhurio ya wanaCCM kwenye mkutano huo yamewafanya wanaCUF kuitisha mkutano wa dharura katika makao makuu yao Mtendeni na kumueleza Maalim Seif kuwa ni nani atakuwa Makamu wa Kwanza wa Rais kwani tayari wameshaonesha dalili za kushindwa nafasi ya urais. Naibu katibu Mkuu wa CCM amewataka wanaCCM kuhakikisha kuwa wanahifadhi kadi zao za kupigia kura kwani alisema ushindi wa chama hicho utakamilika kwa kura na siyo vyenginevyo. Alisema kuwa ajenda nyengine iliyozungumzwa kwenye kikao hicho ni kuwazuia wanaCCM kutopiga kura siku ya tarehe 25 mwezi huu lakini hilo halitowekana  wani vyombo vya dola vipo kwa kazi ya kuhakikisha amani na utulivu unaimarika.  
Vuai alisema kuwa visa vitakuwa vingi katika kipindi hichi kilichobaki ikiwa ni pamoja na kufanya vurugu za kila aina kwa lengo la kutaka kusifanyike kwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu lakini hilo haliwezekani.  
Alisema kuwa kuna kila sababu za kuchaguliwa kwa Dk. Shein kwani ametekeleza ilani kwa azaidi ya salimia 90, ni muungwana, mkweli ni mtendaji na muadilifu wa hali ya juu. 
Alisema kuwa Dk. Shein ameinua kiwango cha elimu, barabara, biashara na uwekezaji, umeme, maji na pia, hivi karibuni aliahidi ndani ya mwaka mmoja wa madaraka yake baada ya kuchaguliwa ataongeza mshahara kwa kima cha chini laki3, azma ya kwasaidia wazee sambamba na kuiweka Zanzibar kuwa ya amani na utulivu.  
Nae Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Idd alieleza kuwa Maalim Seif alikwenda Afrika ya kusini kuomba fedha kwa ajili ya kukisaidia chama chake  na baada ya kurudi Zanzibar alianza kuwadanganya wafuasi wake kuwa kaonana wa wawekezaji ambao wameahidi kuja kuekeza na kuifanya Zanzibar kuwa Singapore.

Alisema kuwa hivi karibuni, Maalim Seif alikwenda kufanya mkutano na wakristo na kuwaomba radhi kwa yote yaliofanywa na CUF ikiwa ni pamoja na matukio kadhaa ya mauaji yaliyofanywa na chama hicho. 
Alisema kuwa kinachotafutwa na wananchi ni Rais na sio ushenga kwani Maalim Seif huwa anapita akisema katika mikutano yake kuwa wajane wote wa kiume atawapa wake iwapo atashinda uchaguzi na kuwa Rais wa Zanzibar.   
Balozi Seif aliwasisitiza wanaCCM kuhakikisha wanawapigia kura za ndio viongozi wote wa CCM kwa lengo la kuendelea kuwaletea maendeleo. 
Mama Fatma Karume mjane wa Rais wa  Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume nae akiwasilimia wanaCCM na wananchi waliohuduria katika mkutano huo  na kuwataka kuwapigia kura zote za ndio wagombea wa CCM kwani chama hicho kina historia kubwa ya ukombozi wa Zanzibar. 
Aliwataka wanaCCM kuwa wamoja na kushikamana baina yao huku wakihakikisha kuwa chama cha CUF kinakosa ushindi kabisa kwa kuwapigia kura viongozi wote wa CCM.
Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mjini, Borafya Ame Silima alisema kuwa anamatumaini makubwa kuwa viongozi wa CCM wanaogombania nafasi za uongozi watashinda kwani imani zao zipo kwa ajili ya kuwasaidia wananchi.
Borafya alisikitishwa na tabia ya kuzichana picha za wagombea wa CCM hasa katika maeneo ya Malindi na Chukwani na kueleza kuwa hiyo ni dalili ya kuonesha wazi kuwa  chama cha CUF kimeshashindwa.
AHSANTENI SANA WANANCHI WA UNGUJA KWA
 KUJA  KWA WINGI SANA KATIKA UWANJA WA MANZI MMOJA  KUWASIKILIZA  WAGOMBEA WA CCM, 
DR JOHN P. MAGUFULI AMBAE NI MGOMBEA 
URAIS WA TANZANIA NA DR ALI MOHAMED SHEIN MGOMBEA  URAIS WA ZANZIBAR.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia 
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein 
akizungumza na maelfu ya anachama wa CCM na wananchi waliohudhuria 
katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM mkutano wa aina yake uliofanyika leo katika uwanja wa Mnazi Mmoja Mjini Unguja.

MAGUFULI AFUNIKA ZANZIBAR
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli amemaliza ziara ya kampeni hapa Zanzibar na kuweka historia kuwa kiongozi aliyekusanya wananchi wengi hadi sasa katika kampeni za mwaka huu.
Mkutano wa mgombea huyo ambao ulifanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja mjini hapa, ulihudhuriwa na umati wa wananchi wa Zanzibar bila ya kujali vyama vyao vya siasa.
Dk. Magufuli ambaye juzi alifanya mkutano kama huo huko Pemba amekuwa kivutio kwa wananchi wa Zanzibar ambapo kabla ya kuja kwake wananchi wengi walikuwa wakiulizia mara kwa mara ratiba ya kampeni ya kiongozi huyo Zanzibar.
Viwanja vya Mnazi Mmoja vilianza kujaa watu tangu majira ya saa sita na kufanya barabara za eneo hilo kufungwa mapema tangu majira ya saa tano.
Katika hotuba yake kwa wananchi Dk. Magufuli aliwahakikishia wa Zanzibar kuwa akichaguliwa atakuwa Rais wa watazania wote na kwamba amepata imani kubwa kutoka kuwa wananchi wa Zanzibar watamchagua kutokana na mapokezi yao makubwa.
“Nimesimama hapa kuomba kura nina imani na nyinyi kwa kuwa mimi nimedhamiria kuwatumikia wananchi wa Tanzania bila ubaguzi” Dk. Magufuli alieleza.
Aliwaeleza hao ambao walikuwa wakikatisha hotuba yake mara kwa mara kuwa alifurahishwa na namna walivyompokea tangu kuwasilisi kwake Zanzibar na namna watu wa vyama vyote walivykuwa na hamu ya kumuona na kumsikiliza.
Dk. Magufuli aliahidi kupambana na rushwa na vitendo vya kiharamia kama vya uvunaji maliasili mfano uvuvi haramu katika bahari kuu kwa kuimarisha ulinzi wa bahari.
“Hapa ni kazi tu, nitawashughulikia mafisadi wote nikiingia madarakani na ndio maana nilipopitishwa tu na chama kugombea nafasi hii mafisadi wote waliondoka CCM wenyewe” Dk. Magufuli
Mgombea huyo wa CCM alisisitiza umuhimu wa kuendeleza mani na utlivu nchini taznania iendelee kuwa tulivu na kukaribisha wageni zaidi wakiwemo watalii ambao wanaingiza pato kubwa kwa taifa.
“pasipo amani hakuna anayeweza kufungua duka, hakuna mtalii atakayekuja kutembelea Tanzania wala Zanzibar, hakuna mtu atakayekuja kujifunza historia ya Zanzibar ambayo inatajika ulimwenguni kote” Dk. Magufuli aliongeza.
Aliahidi kushirikiana na Dk. Shein kuhakikishia kuwa amani na utulivu wan chi unaendelea kuwepo nchini ili wananchi waweze kuendekla na shughuliza za kujiletea maendeleo.

AHSANTENI SANA WANANCHI WA PEMBA KWA KUJA  KWA WINGI SANA KATIKA UWANJA WA GOMBANI YA KALE  KUWASIKILIZA  WAGOMBEA WA CCM, DR JOHN P. MAGUFULI AMBAE NI MGOMBEA URAIS WA TANZANIA NA DR ALI MOHAMED SHEIN MGOMBEA
 URAIS WA ZANZIBAR.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia akamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Wanachama wa CCM na Wananchi wa Kisiwani Pemba leo katika mkutano wa hadhara wa kampeni za kumnadi Mgombe Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli  katika uwanja wa Gombani ya kale Wilkaya ya Chake chake Pemba


Mgombe Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufulu akizumgumza na Wananchi na WanaCCM wa Kisiwani Pemba leo katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM zilizofanyika katika uwanja wa Gombani ya kale Wilkaya ya Chake chake Pemba
Mgombe Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufulu akimuombea kura Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibad Dk.Ali Mohamed Shein kwa  Wananchi na WanaCCM wa Kisiwani Pemba leo katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM zilizofanyika katika uwanja wa Gombani ya kale Wilkaya ya Chake chake Pemba.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wananchi wa Zanzibar kumchagua Dk. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu ndie mgombea anayefaa kushika wadhifa huo.
Dk. Shein aliueleza umati wa wananchi uliohudhuria mkutano mkubwa wa kampeni huko Gombani Chake Chake Pemba kuwa uamuzi wa kumteua Dk. Magufuli kugombea nafasi hiyo ni uamuzi sahihi kwa kuwa Dk. Magufuli ni mtu makini, mchapakazi, anayeiependa nchi yake na watanzania wenzanke.
“Chama cha Mapinduzi kilimteua Dk. Mafuguli kutokana na sifa zake na tukishirikiana sote tutaijenga Tanzania kwa mafanikio makubwa zaidi” alisema Dk. Shein.
Katika mkutano huo aliwasuta wanaohubiri kuvunja Muungano kwa kueleza kuwa hakuna mtu wala kikundi cha watu wanaoweza kuvunja Muungano huo ambao umedumu kwa miaka zaidi ya hamsini sasa.
“Tulishirikiana katika kutafuta Uhuru wetu, tukafanikiwa na baadae tukaamua kuungana wananchi wa Tanganyika na Zanzibar na leo ni nchi moja” Dk. Shein alieleza.
Kwa hivyo aliwataka wananchi kuwachagua wagombea wa CCM kwa nafasi za Urais, wabunge, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na madiwani ili kujenga timu kabambe ya kuleta maendeleo.
Katika mkutano huo Dk. Shein aliwatahadharisha baadhi ya watu ambao wamedhamiria kufanya vurugu wakati wa uchaguzi na kuonya kuwa wasithubutu kufanya hivyo kwani serikali haitawavumilia.
Alisisitiza kuwa baadhi ya watu hao wanafahamika kwa majina na wanakoishi hivyo waelewe kuwa wanachokifanya ni kinyume na malengo ya Mapinduzi yaliyoleta umoja na mshikamano wetu.
“Nimewahakikishia mara kwa mara wananchi wote na hata washirika wetu wa maendeleo kuwa tutafanya uchaguzi huru na wa haki hivyo sitarajii mtu au kikundio cha watu kuuchafua uachaguzi kwa kufanya vurugu” Dk. Shein alionya.
Aliwaeleza wananchi kuwa amani, umoja na mshikamao kuwa miongoni wao masuala muhimu kwa kuwa ndio misingi muhimu ya maendeleo ya nchi hivyo hawana budi kuhakikisha kuwa wajiepusha na vitendo vya kuhatarisha amani.
Alibainisha kuwa nguzo kuu ya amani na mshikamano wa wananchi wa pande mbili hizo iliwekwa katika Muungano wa vyama vyetu vya Afro Shirazi na TANU hivyo wananchi hawana budi kuyaenzi Mapinduzi ya mwaka 1964 kwani kufanya hivyo ndio watakuwa wameimarisha umoja wetu, uhuru wetu na Muungano wetu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akiteta jambo naMgombe Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli leo katika mkutano wa hadhara wa kampeni za kumnadi   katika uwanja wa Gombani ya kale Wilaya ya Chake chake Pemba,
 Miongoni mwa maelfu ya wanaCCM wakimsikiliza Mgombe Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli alipokuwa akitoa sera za Chama cha Mapinduzi CCM leo katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM kuomba Ridhaa ya kuchaguliwa katika nafasi ya kuiongoza Tanzania.


  
 Mwenyekiti wa Jumuiya yaWazazi Taifa  Abdalla Bulembo pia akiwa Kiongozi wa Msafara wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli  akiwasalimia wanaCCM katika mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyikaleo katika uwanja wa Gombaniyakale wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba

 


 AHSANTENI SANA WANANCHI WA JIMBO LA 
CHWAKA KWA KUJA  KWA WINGI SANA KATIKA UWANJA WA  MISUKA  KUMSIKILIZA  MGOMBEA
 URAIS WA ZANZIBAR  KUPITIA CCM  DR ALI MOHAMED SHEIN.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar
 Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wanaCCM na Wananchi wa Jimbo la Chwaka katika
 mkutano wa hadhara  wa Kampeni za CCM uliofanyika leo katika uwanja wa mpira Kijiji cha Chwakawilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Ali Mohammed Shein ameeleza azma yake ya kuendelea kuwainua wasanii hapa nchini kwa kutekeleza ahadi yake ya ujenzi wa studio za kisasa ambazo tayari zimekamilika na kuwekwa vifaa vyenye sifa na ubora wa pekee kwa shughuli za kurikodia.
Dk. Shein aliwataka wasanii hao kukaa mkao wa kula kwani lengo lake la kuwainua wasanii limefikiwa ambapo tayari ujenzi wa studio hizo za kisasa za kurikodi nyimbo na michezo ya kuigiza umekamilika na wakati wowote shughuli za kurikodi zitaanza.
Hayo aliyasema wakati alipokuwa akizungumza na wananchi pamoja na WanaCCM waliohudhuria katika mkutano wa Kampeni za uchaguzi kwa upande wa CCM uliofanyika katika uwanja wa mpira Chwaka, Jimbo la Chwaka, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Katika maelezo yake, Dk. Shein alisema kuwa studio hizo zimejengwa kwenye jengo jipya la zamani la Utangazaji la Sauti ya Tanzania Zanzibar, baada ya kufayiwa matengenezo makubwa na kuwekewa vifaa  hivyo vya kisasa.
Alisema kuwa lengo na madhumuni ya ujenzi wa studio hizo ni kuhakikisha wasanii wanaimarisha kazi zao za sanaa zao na kwenda na wakati uliopo kutokana na vifaa vya kisasa vilivyomo ndani ya studio hizo.
Dk. Shein alisisitiza kuwa wasanii watafaidika na huduma zitakazotolewa na studio hizo ambazo zitawasaidia kuondokana na usumbufu wanaoupata hivi sasa katika kurikodi kazi zao.Studio hizo ni za kisasa ambazo ni za pekee kwa nchi za Afrika Mashariki ambapo vifaa vyake vinatoka nchini Uingereza na tayari vifaa hivyo vimeshafanyiwa majaribio na wakati wowote shughuli za kurikodi kazi za wasanii zinatarajiwa kuanza.







Mgombea  urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein
 akiwatambulisha wagombea uongozi wa ngazi mbali kwenye uchaguzi mkuu ujao wa
  Jimbo la  Chwaka.











AHSANTENI SANA WANANCHI WA JIMBO LA MAHONDA  KWA KUJA  KWA WINGI KATIKA
 UWANJA WA MISUKA KUMSIKILIZA  MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KUPITIA CCM DR ALI MOHAMED SHEIN.
         MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR LUPITIA CHAMA CHA MAPINDUZI DR      ALI MOHAMED SHEIN AKIWAHUTUBIA WANANCHI WALIOFURIKA KWENYE         UWANJA WA MISUKA MAHONDA KWENYE MKUTANO WA HADHARA WA                                        KAMPENI YA UCHAGUZI.

  •      DK. SHEIN AWASUTA CUF NA KUSEMA SEMA:
  •               TUNAJENGA ZANZIBAR SIO SINGAPORE WALA MAURITIOUS. 
  •             CUF ELEZENI MAFANIKIO YA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA.
  •         AWATAKA WASINUNE AKIWAELEZA MAFANIKIO YA SERIKALI  NA           CHAMA CHA MAPINDUZI.
  •   ASEMA KUTEKELEZA ILANI YA CCM NDIO MAKUBALIANO.

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi-CCM Dk. Ali Mohamed Shein amesema chama chake na Serikali atakayoiunda endapo atachaguliwa tena amedhamiria kuongeza kasi ya kuijenga Zanzibar ili iweze kufikia malengo yaliyomo katika mipango mbalimbali ya maendeleo ya nchi.

“Tumelenga kuendelea kuijenga Zanzibar kwa kasi zaidi sio Singapore wala Mauritius kwani kazi hiyo tumeianza kipindi kilichopita na tumeonesha kuwa tuna uwezo huo”Dk. Shein ameuambia mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika leo huko Mahonda katika jimbo la Uchaguzi la Donge, Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja.
Amesema katika kipindi kilichopita Serikali aliyoingoza ambayo ilikuwa chini ya Mfumo wa Umoja wa Kitaifa imefanya kazi nzuri ya kuitekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM lakini bahati mbaya wapinzani wanasita kueleza mafanikio katika mikutano yao ya kampeni.
“Tumetekeleza pamoja Ilani ya CCM na baadhi ya wizara zimeongozwa na mawaziri kutoka upinzani lakini katika mikutano yao ya kuomba kura hawataki kuwaeleza wananchi mafanikio tuliyoyapata badala yake wanasema hatujafanya lolote” Dk. Shein alieleza.
Hivyo aliwataka wapinzani kuwa waungwana kwa kutangaza mafanikio ya uongozi wa kipindi cha miaka mitano iliyopita kwa kuwa na wao walishiriki kuyafakisha na kwamba kutekelezwa kwa Ilani ya CCM ndio makubaliano katika kuendesha serikali katika mfumo wa Umoja wa Kitaifa.
Alifafanua kuwa utaratibu tulikubalika ni kuwa Ilani itakayotekelezwa ni ya chama kinachoshinda na hivyo ndivyo ilivyofanyika.
Aliwaeleza maelfu ya wananchi waliokuwa wakikatisha hotuba yake kwa vifijo na vigelegele kuwa Chama cha Mapinduzi kitashinda uchaguzi ujao kwa kuwa kimeonesho weledi na umakini mkubwa katika kupanga na kutekeleza Ilani na kuongeza kuwa katika kampeni zake ni lazima kutangaza mafanikio ya serikali yeke na kunadi Ilani.
Alieleza kuwa wakati katika kipindi kilichopita Serikali imeweza kutekeleza ahadi alizozitoa wakati wa kampeni mwaka 2010, katika kipindi kijacho aliahidi kuongesa kasi ya kuimarisha huduma za jamii.
“Katika miaka mitano ijayo tutazijenga kwa kiwango cha lami barabara za Matemwe-Muyuni, Kichwele-Pangeni, Kinduni-Kichungwani, Mkwajuni-Kijini na Pale -Kiongole” Dk. Shein alizitaja barabara hizo.
Kwa upande wa umeme aliahidi kuvipatia umeme vijiji vya Chechele na Mwmwembe Maji katika jimbo hilo na kususitiza kuwa katika awamu ijayo serikali itaongeza kasi ya usambazaji huduma hiyo vijijini.
Dk. Shein  ataendelea na mikutano yake ya kampeni kisiwani humu kesho ambako atahutubia mkutano mkubwa wa kampeni huko Chwaka. 
                                
 







No comments:

Post a Comment