WAHI MAPEMA KUMTILIA KURA DR. ALI MOHAMED SHEIN
TAREHE 25/10/2015 ==(READY 2 GO)==
Ahsanteni wananchi wa Mahonda
kwa kuja kwa wingi sana na kuujaza uwanja wa Misuka kwenye mkutano wa hadhara kumsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.Dr Ali Mohamed Shein.
DK. SHEIN AWASUTA CUF NA KUSEMA SEMA:
· TUNAJENGA ZANZIBAR SIO SINGAPORE WALA MAURITIOUS .
· CUF ELEZENI MAFANIKIO YA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA
· AWATAKA WASINUNE AKIWAELEZA MAFANIKIO YA SERIKALI NA CHAMA CHAKE
· ASEMA KUTEKELEZA ILANI YA CCM NDIO MAKUBALIANO
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi-CCM Dk. Ali Mohamed Shein amesema chama chake na Serikali atakayoiunda endapo atachaguliwa tena amedhamiria kuongeza kasi ya kuijenga Zanzibar ili iweze kufikia malengo yaliyomo katika mipango mbalimbali ya maendeleo ya nchi.
“Tumelenga kuendelea kuijenga Zanzibar kwa kasi zaidi sio Singapore wala Mauritius kwani kazi hiyo tumeianza kipindi kilichopita na tumeonesha kuwa tuna uwezo huo”Dk. Shein ameuambia mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika leo huko Mahonda katika jimbo la Uchaguzi la Donge, Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja.
Amesema katika kipindi kilichopita Serikali aliyoingoza ambayo ilikuwa chini ya Mfumo wa Umoja wa Kitaifa imefanya kazi nzuri ya kuitekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM lakini bahati mbaya wapinzani wanasita kueleza mafanikio katika mikutano yao ya kampeni.
“Tumetekeleza pamoja Ilani ya CCM na baadhi ya wizara zimeongozwa na mawaziri kutoka upinzani lakini katika mikutano yao ya kuomba kura hawataki kuwaeleza wananchi mafanikio tuliyoyapata badala yake wanasema hatujafanya lolote” Dk. Shein alieleza.
Hivyo aliwataka wapinzani kuwa waungwana kwa kutangaza mafanikio ya uongozi wa kipindi cha miaka mitano iliyopita kwa kuwa na wao walishiriki kuyafakisha na kwamba kutekelezwa kwa Ilani ya CCM ndio makubaliano katika kuendesha serikali katika mfumo wa Umoja wa Kitaifa.
Alifafanua kuwa utaratibu tulikubalika ni kuwa Ilani itakayotekelezwa ni ya chama kinachoshinda na hivyo ndivyo ilivyofanyika.
Aliwaeleza maelfu ya wananchi waliokuwa wakikatisha hotuba yake kwa vifijo na vigelegele kuwa Chama cha Mapinduzi kitashinda uchaguzi ujao kwa kuwa kimeonesho weledi na umakini mkubwa katika kupanga na kutekeleza Ilani na kuongeza kuwa katika kampeni zake ni lazima kutangaza mafanikio ya serikali yeke na kunadi Ilani.
Alieleza kuwa wakati katika kipindi kilichopita Serikali imeweza kutekeleza ahadi alizozitoa wakati wa kampeni mwaka 2010, katika kipindi kijacho aliahidi kuongesa kasi ya kuimarisha huduma za jamii.
“Katika miaka mitano ijayo tutazijenga kwa kiwango cha lami barabara za Matemwe-Muyuni, Kichwele-Pangeni, Kinduni-Kichungwani, Mkwajuni-Kijini na Pale -Kiongole” Dk. Shein alizitaja barabara hizo.
Kwa upande wa umeme aliahidi kuvipatia umeme vijiji vya Chechele na Mwmwembe Maji katika jimbo hilo na kususitiza kuwa katika awamu ijayo serikali itaongeza kasi ya usambazaji huduma hiyo vijijini.
Dk. Shein ataendelea na mikutano yake ya kampeni kisiwani humu kesho ambako atahutubia mkutano mkubwa wa kampeni huko Chwaka.
VIONGOZI WA CCM Zanzibar wameeleza kuwa CCM ina kila sababu ya ushindi
kutokana na kuungwa mkono na wananchi walio wengi nchini hali ambayo inatokana
na utekelezaji wake wa Ilani, Sera na ahadi zake kwa vitendo huku wakiwataka
wananchi wa Zanzibar kutokubali kurejeshwa walikotoka.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika
mkutano wa Kampeni ya uchaguzi wa CCM uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi na
wanaCCM uliofanyika uwanja wa Misuka, Jimbo la Donge, Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa
wa Kaskazini Unguja, viongozi wa CCM waliohudhuria mkutano huo kwa nyakati
tofauti walisema kuna CCM ndio chama pekee kinachojali maslahi wa wananchi.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamo wa
Pili wa Rais ambaye pia, ni mgombea wa nafasi ya Uwakilishi Jimbo la Mahonda Balozi
Seif Ali Iddi alisema kuwa katika chama cha CUF hakuna viongozi wa kuhubiri
siasa na badala yake wapo viongozi wasanii.
Alisema kuwa usanii huo unatokana na
kubadilisha maneno kwa kila siku wanapokutana na wafuasi wao ambapo hutumia
lugha za kuwadanganya ili wachaguliwe.
Balozi Seif alishangazwa na hatua
zilizochukuliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad kwenda
Tume ya uchaguzi ambapo kutokana na cheo chake haruhusiki kuziingia kazi za
Tume hiyo.
Waziri wa Maji, Ardhi na Nishati ambaye pia, ni Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya Taifa, Ramadhan Abdalla Shaaban nae aliendelea kulielezea suala la
mafuta na kuwasisitiza wananchi kutodanganyika juu ya suala hilo.
Waziri Shaaban alisema kuwa CCM na
viongozi wake wanahistoria kubwa ya kulifuatialia suala hilo na kueleza kuwa
tayari Dk. Shein ameanza kulifanyia kazi kwa mashirikiano na Rais Jakaya Mrisho
Kikwete.
Nae Balozi Amina Salum Ali alisema kuwa
mwaka huu ushindi wa CCM hauepukiki kutokana na hamasa kubwa waliyoipata vijana
wa Unguja na Pemba hatua ambayo inakihakikisha
ushindi chama hicho.
Alisema kuwa CCM kila baada ya miaka
mitano huchagua viongozi kwa lengo la kutangaza Sera zinazotekelezeka.
Aidha, alieleza kuwa viongozi wa CCM
wamefanya mambo mengi ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar na kuwataka vijana
na wananchi kwa jumla kuwachagua viongozi wa CCM pamoja na kufahamu azma ya
Mapinduzi hatua ambayo matunda yake yanaonekana.
Nae Mjumbe wa Halmashauri Kuu wa Taifa
ambaye pia ni Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za
SMZ Haji Omar Kheir, alisema kuwa viongozi
wa CCM wanachaguliwa kwa sababu wanatekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo na ndio
maana wataendelea kuchaguliwa na mwaka huu wataendelea kushinda.
Alisema kuwa wanaogawa pikaka ya Majimbo
ni Tume ya Uchaguzi hivyo si haki kukaa kwenye viriri vya mikutano na kuanza
kuwalaumu viongozi wa CCM huku akishangazwa na viongozi wa CUF kupita kueleza
maneno yasio na msingi.
Aliwataka wananchi na wanaCCM kuwachagua
viongozi watakaowaletea maendeleo huku akisisitiza kuwa Dk. Shein ndie
atakaepelekwa Ikulu kutokana na busara yake, hekima na anaejua kazi zake za
urais.
Alisema kuwa tayari Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar chini ya uongozi wa CCM una mpango madhubuti wa wa kujenga Soko jipya
la ghorofa litakalojengwa katika Mkoa huo kupitia mradi wa MIVAP.
Nae aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo la
Kitope, Makame Mshimba Mbarouk aliwaeleza wananchi na wanaCCM kuwa CCM ni chuo
na kueleza kuwa wale wote waliosema kenda UKAWA na wengine kusema kajiunga na
chama cha CUF ni maneno yakiupuzi na yasio na maana.
Mshimba alishangazwa na wale wanaosema
kuwa CCM haijafanya kitu na kueleza kuwa CCM imefanya mambo mengi huku akisema
kuwa amefuatwa sana na wapinzani ili aihame CCM jambo ambalo alisema hawezi
kulifanya wala hawezi kukisaliti chama hicho kutokana na kufanya mambo mengi na
ataendelea kubaki kwenye chama chake cha CCM, na kuwaombea kura viongozi wote
wa CCM.
Nae mama Fatma Karume akiwasalimia
wananchi na wanaCCM waliohudhuria katika Mkutano huo na kuwataka wananchi wa
Zanzibar kuwa makini na kujua wanatoka wapi na wanakwenda wapi na vijana
wakumbuke walikotoka wazee wao na kutokubali kurejeshwa nyuma.
Aliwaambia Wazanzibar kuwa makini katika
kuilinda amani iliyokuwepo na kuichagua CCM ili kuepuka yasije kutokezea
yanayowakumba wananchi waliokosa amani katika nchi mbali mbali duniani.
Aliwataka wananchi wa jinsia zote na hali
zote kuichagua CCM kwani ndicho chama kinachopigania maendeleo yao na
kinachowajali.
Nae Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,
Vuai Ali Vuai aliwaombea kura viongozi wote wa CCM akiwemo Rais wa Zanzibar Dk.
Shein, Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dk. John Magufuli pamoja na Wabunge,
Wawakilishi na Madiwani.
Nao viongozi wa Mkoa wa Kaskazini kwa
nyakati tofauti walisisitiza haja ya kuendelea kusimamia amani na utulivu na kumpongeza
Dk. Ali Mohamed Shein kwa kutekeleza vyama Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Waliwataka vijana kutohadaika na maneno ya
wapinzani na kuwataka wawachague viongozi wa CCM kwani ndio wanaojali maslahi
ya wananchi.
Viongozi hao walimueleza Dk. Shein kuwa
asiwe na wasi wasi kwa Mkoa wa Kaskazini kwani walifuata maneno ya Mwalimu Nyerere
kuwa amani ya Tanzania inatengemea sana kwa kuwepo kwa CCM.
Ahsanteni wananchi wa Pujini
Pemba kwa kuja kwa wingi sana na kuujaza uwanja wa Pujini kwenye mkutano wa hadhara kumsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.Dr Ali Mohamed Shein.
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. Ali Mohamed Shein ameahidi katika kipindi kijacho cha uongozi wake kiwanja cha ndege cha Karume Pemba kitaimarishwa ili kuwezesha ndege za kimataifa kutua moja kwa moja kutoka nje hivyo kuongeza biashara ya utalii nchin.
Ametaja hatua zinazochukuliwa kuwa ni pamoja na ujenzi wa njia ya ndege na kuongeza urefu na kuweka taa za katika njia ya kurukia na kutua ndege, kuimarisha miundombinu ya huduma za abiria na mizigo kwa kujenga jengo jipya, huduma za umeme na kukamilisha ujenzi wa uzio.
Mgombea huyo wa CCM ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Pujini katika jimbo la uchaguzi la Chonga, wilaya ya Chake Chake, mkoa wa Kusini Pemba.
Dk. Shein aliwaeleza mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano huo kuwa katika kuimarisha uvuvi nchini Serikali itajenga kiwanda cha kutotolea vifaranga vya samaki huko Beit el Ras Unguja ili kuimarisha ufugaji wa samaki ambao umeanza kushika kasi visiwani humo.
“Tutajenga chuo cha mafunzo ya uvuvi, viwanda vya kusindika samaki na bandari maalum kwa ajili ya uvuvi Unguja na Pemba” Dk. Shein alifafanua.
Katika mkutano huo Dk. Shein aliwahakikishia wananchi kuwa uchaguzi utakuwa huru na salama na kwamba wasiwe na hofu yeyote ulinzi na usalama utaimarishwa na kuwaonya wale ambao wamedhamiria kufanya fujo wakati wa uchaguzi.
“ Tunawahakikishia wananchi kuwa uchaguzi utakuwa huru na wa haki kwani uchaguzi ni utaratibu wa kidemokrasia ambao kila mshiriki anapaswa kuuheshimu” Dk. Shein alisisitiza na kuwatahadharisha wale wote wenye dhamira ya kufanya fujo na kuharibu uchaguzi
Aliwapongeza wananchi wa Pujini kwa kuwa mstari wa mbele katika ufugaji wa samaki na kubainisha kuwa serikali iligharimia kuanzisha bwawa darasa ili kuwapatia mafunzo ya ufugaji huo.
Dk. Shein aliwaeleza wafugaji wa samaki wa Pujini kuwa ahadi yake ya kuwapelekea umeme alioitoa wakati alipowatembelea Julai mwaka jana imeanza kutekelezwa ambapo hatua ya awali imeanza kwa kupeleka nguzo.
Alisema serikali atakayoiongoza katika awamu ijayo itaendelea na mikakati yake ya kuimarisha elimu katika ngazi zote na kuahidi kujenga skuli za msingi kumi za kisasa na za ghorofa kati ya hizo sita zitajengwa Unguja na nne zitajengwa Pemba.
Katika kipindi kijacho serikali yake itajenga barabara kuu ya kutoka Chake Chake hadi Mkoani na barabara ya Ole hadi Kengeja yenye urefu wa kilomita 35 ambayo maandalizi ya ujenzi yameanza.
Alizitaja barabara ndogondogo zitakazojengwa kuwa ni Matangini-Kilindi na Kipapo –Mgelema. Kwa upande wa utekelezaji alisema barabara za Chanjamjawiri- Pujini na Kuyuni –Ngomeni kwa kiwango cha kifusi zilikamishwa sambamba na barabara ya Chanjaani-Pujini yenye urefu wa kilomita 5 ambayo ilijengwa kwa kiwango cha lami.
Kwa upande wa umeme katika kipindi kijacho akichaguliwa tena aliahidi kuvipatia umeme vijiji vya Limani, Ngomeni, Kitundwini, Chanoni, Mwachawa, Hauraha, Limanda Pujini na Tuunguuni Kilindi.
Katika kipindi kilichopita aliwaeleza wananchi hao kuwa vijiji vya Kilindi, Banaani, Mtimbu, Kijini na Kibaridi katika jimbo hilo vilipatiwa huduma hiyo. Mgombea huyo wa CCM ataondoka Pemba kesho kurejea Unguja ambako ataendelea na kampeni zake kwa kuhutubia mkutano mkubwa wa kampeni huko katika viwanja vya Misuka katika jimbo la Uchaguzi la Donge wilaya Kaskazini ‘B’.
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM Dr AliMohamed Shein akiwatambulisha wagombea uongozi wa ngazi mbali mbalin za uongozi katika uchaguzi ujao.
Ahsanteni wananchi wa Mtambwe Kaskazini
Pemba kwa kuja kwa wingi sana na kuujaza uwanja wa Mkoongeni kwenye mkutano wa hadhara kumsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.Dr Ali Mohamed Shein.
DK. SHEIN: USHINDI WA CCM MWAKA HUU NI KIFO CHA CUF
- Wananchi wameamua kuipa kisogo CUF
- Bei ya soko la dunia ikipanda hatutasita kuongeza bei ya karafuu
- Nitaendelea kuimarisha mindombinu na huduma za jamii
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. Ali Mohamed Shein amesema chama chake kitashinda tena uchaguzi wa mwaka huu na kushika dola na kwamba huo utakuwa mwisho wa Chama cha Wananchi-CUF kwa kuwa chama hicho kimezoea kudanganya wananchi ambao sasa wameamua kukipa kisogo. Katika mkutano wa mkubwa wa kampeni wa chama hicho uliofanyika huko Makoongeni Mtambwe, Dk. Shein aliwaambia wananchi hao kuwa kauli za chama hicho na Katibu Mkuu wake cha kuleta Zanzibar yenye mamlaka kamili ni upotoshaji na ghiliba za kuwafanya wakipigie kura chama hicho lakini kadri muda unavyokwenda wananchi wamekuwa wakizigundua ghiliba hizo.
“tafsiri ya mamlaka kamili ni kuwa sote tunaukataa Muungano jambo ambalo si kweli na lisilowezekana kwa watanzania wote, Bunge na Baraza la Wawakilishi kuukataa Muungano”alieleza Dk. Shein.
Mgombea huyo wa CCM aliwataka wananchi wa Mtambwe kufanya uamuzi sasa wa kuwapigia kura wagombea wa CCM na kuahidi kuongeza kasi ya maendeleo katika kipindi kijacho pindi akichaguliwa tena.
“Tutapiga hatua zaidi ya maendeleo katika kipindi kijacho kwa kuwa katika kipindi kilichopita tumedhihirisha kuwa uwezo wa kufanya hivyo tunao na zaidi washirika wetu wa maendeleo wazidi kuonesha imani kubwa na uongozi wangu hivyo wameahidi kuendelea kushirikiana nasi katika harakati zetu za kujiletea maendeleo” Dk. Shein alieleza.
Mgombea huyo wa CCM aliwaahidi wapiga kura na wananchi wote kuwa endapo watamchagua tena ndani ya miaka miwili ya mwanzo ya uongozi wake ataondosha michango yote katika sekta ya afya huku akisisitiza kuwa katika kipindi cha mwaka wa kwanza wa uongozi wake kipindi kijacho elimu ya sekondari itakuwa bure.
“dhamira ya serikali ni kuhakikisha malengo ya Mapinduzi ya kutoa afya na elimu bure linatimizwa kadri uwezo wa serikali unavyoimarika.Katika kipindi kijacho tutaendelea kuimarisha huduma za jamii na kwa kuendeleza miundombinu yake na kuzipatia vifaa vya kisasa na wataalamu” Dk. Shein alisema.
Aliwataka wananchi kuendelea kuimarisha kilimo cha karafuu na kuwataka wasibweteke na kauli za baadhi ya viongozi wa upinzani kuwa mafuta yatachimbwa ndani ya siku 100.
“Mafuta si jambo la leo wala kesho itatuchukua muda mrefu kuchimba mafuta na kufaidika nayo lakini hata kama yatakuwepo bado Zanzibar rasilimali yake kuwa ni zao la karafuu na hatuna budi kulithamini na kulienzi” Dk. Shein alisisitiza.
Aliwahakikishia tena wakulima wa zao la karafuu kuwa serikali itaendelea kulipa uzito zao hilo na kusisitiza kuwa serikali haitasita kuongeza bei sio tu kuhakikisha wakulima wanafaidika zaidi na zao lakini pia kuhakikisha kuwa zao hilo linaendelea kuwa zao muhimu la uchumi na nembo ya Zanzibar.
Katika kipindi cha miaka mitano ijayo akichaguliwa Dk. Shein aliahidi kuimarisha miundombinu ya barabara katika jimbo la uchaguzi la Mtamwe na wilaya ya Wete kwa kuzijenga kwa kiwango cha lami barabara za Miembe Mazizi-Chanjaani, Uondwe-Nyali, Mkanjuni-Kivumoni, Mokoongeni-Kinazini na Mkarafuu Mmoja- Mnazi Mmoja.
“Tulitoa ahadi mwaka 2010 ya kuijenga barabara ya Bahanasa –Mtambwe na nyingine nne zote tumetekeleza.Vituo vya afya vimeimarishwa na kati yao vituo vitatu kati ya hivyo vimepandishwa daraja kuwa daraja la pili hivyo kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kutoa huduma zaidi kwa wananchi” Dk. Shein aliongeza.
Kuhusu usambazaji umeme katika jimbo hilo alieleza kuwa ni vijiji vichache tu ndio bado havijapata umeme lakini viwili miongoni mwao vya Chekea kitapata umeme hivi karibuni na mipango itafanywa kukipatia kijiji cha Mtambwe Mkuu huduma hiyo mara tu baada ya kuingia madarakani.
Mgombea huyo urais kwa tiketi ya CCM ataendelea na kampeni zake kesho kisiwani Pemba kwa kuhutubia mkutano wa kampeni utakaofanyika huko Pujini katika jimbo la uchaguzi la Chonga.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akiwatambulisha wagombe Ubunge katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo kijiji cha Makoongeni Wilaya ya Wete Pemba katika Jimbo la Mtambwe pia kuwaombea Kura Rais wa Jamhuri ya Muungano na Mgombea Mwenza,
WANACCM na wananchi kisiwani Pemba wametakiwa kutotishika na vitisho vinavyotolewa
na viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani vya kuwafanyia hujuma siku ya uchaguzi
mkuu Oktoba 25 mwaka huu kwani vyombo vya ulinzi na usalama vimejiapanga
kuwalinda katika kutekeleza haki yao hiyo ya kikatiba.
Wakizungumza katika nyakati tofauti
katika mkutano wa Kampeni ya uchaguzi wa CCM uliofanyika Mtambwe leo, Mkoa wa
Kaskazini Pemba, viongozi wa CCM waliohudhuria mkutano huo walisema vyama vya
upinzani vimeshajua kuwa kuna kila dalili kwa CCCM kushinda kwa kishindo katika
uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi huu na kwamba njia pekee inayokusudiwa
kufanywa na upinzani ni kutumia vitisho kwa lengo la kuwazuia wapiga kura wa
CCM.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ambaye pia ni
Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi amesema Serikali imegundua mbinu
zinazokusudiwa kufanywa na vyama vya upinzani na amewahakikishia wanaCCM na
wananchi kwamba Serikali imejidhatiti kukabiliana na hali yoyote
itakayojitokeza kwa kuweka ulinzi imara ili wananchi wote waweze kuitumia haki
yao ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Balozi Seif Ali Iddi aliwataka wananchi
wa Mtambwe kuwa makini kusikiliza sera za wagombea kutoka vyama mbali mbali vya
siasa lakini kuwachagua wagombea wa CCM ambao ahadi zao zinatekelezeka.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Idd, alishangazwa na kauli za baadhi ya wagombea wenye kunadi
maendeleo kwa wapiga kura wakati wao wenyewe wameshindwa kuonesha mfano kwenye
vijiji walivyotoka licha ya kuweko madarakani kwa muda mrefu.
Viongozi wa CCM waliopata fursa ya
kusalimiana na wananchi pamoja na WanaCCM waliohudhuria katika mkutano huo walielezea
kuridhishwa kwao na hali ya mabadiliko na ukuaji wa demokrasia na maendeleo
katika jimbo la Mtambwe ambako wananchi wameonesha kuwa huru kuchagua sera za
chama wakipendacho wakionesha mabango yanayosomeka "kubadili chama siyo
kurtadi".
Alieleza kuwa wimbi kubwa limekuwa
linaikimbia CUF na kuipongeza wanaMtambe walio wengi kujiunga na CCM na
kuendelea kukiunga mkono kwa nguvu zao zote chama hicho cha CCM.
Akizungumzia maendeleo ya Mtambwe na
Pemba kwa jumla, Balozi Seif Ali Iddi alisema kuwa miongoni mwa juhudi
zilozofanywa na serikali ndani ya miaka mitano chini ya uongozi wa Dk. Shein ni
hatua yake ya kulirejeshea hadhi yake zao la karafuu na kuwapa pencheni wazee
waliotimia miaka 70.
Alisema kuwa Dk. Shein ameondosha gharama
zilizokuwa zikilipwa na wazazi kaondosha na hivi sasa akina mama watakuwa
wakipata huduma hizo bure ambapo pia hivi karibuni aliahidi kuwa akipewa ridhaa
atatoa mshahara kima cha chini laki tatu kwani Dk. Shein hadanganyi na anatenda
alichoahidi.
Aliwataka wananchi na wanaCCM kuangalia
chama kinachotekeleza ahadi zake kwa wananchi huku akisisitiza kuwa ataendelea
kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda kwani anauhakika na ushindi hadi pale
atakapoamua kupumzika.
Alisema kuwa mbinu zinafanywa ikiwa ni pamoja na kununua vitambulisho vya
CCM, na kuwaambia kuwa hivi sasa
viongozi wa upinzani wanawatisha wananchi kuwa CUF wakishindwa nyumba za wafiasi
wa CCM watazichoma moto na kuwataka wananchi kutotishika. na kutokubali
kutishwa.
Alisema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama
viko macho na kusisitiza kuwa ushindi wa CCM ni lazima mwaka huu, na kuwataka
wanaCCM wa Pemba kupamba maskani zao, nyumba zao kwani ushindi kwa CCM
hauepukiki.
Aliwataka wananchi kuamka mapema kwenda
kupiga kura, na baadae kurudi nyumbani na kuwahakikishia wananchi kuwa kutakuwa
na ulizni wa kutosha ili kila mwananchi apige kura kwa amani na utulivu.
Balozi Seif alitoa salamu kwa wananchi wa
Kinyikani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Jimbo la Kojani ambao wameamua
kujitoa katika chama cha CUF na kujiunga na CCM kwa kuomba kujengewa barabara
yao kutoka Mzambarauni hadi Mchangamdogo.
Nae Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa
Pili wa Rais Mohammed Aboud alisema kuwa katika kipindi cha miaka mitano Djk.
Shein amefanya kazia mkubwa ya kuleta maelndeleo, na mfamo ni barabara kutoka
Bahanasa kuja Mtambwe.
Alisema kuwa sio tu ujenzi wa barabara,
bali ni kuhakikisha wananchi wa Unguja na Pemba wanapata mambo ya msingi
ikiwa ni pamoja na huduma za afya,
elimu, maji, umeme, biashara na nyengine kwani amefanya kazi za maendeleo nchini
hivyo kuna kila sababu ya kumpa kura za ndio Dk. Ali Mohamed Shein.
Waziri Mohammed alisema kuwa Dk. Shein ni
hidaya kwa Zanzibar kwani ni mkweli, mchapa kazi, hana makuu, mwenye subira na
mfano wa kuonesha kuwa ameweza kuhimili vituko vingi ambavyo vimefanywa na wapinzani
ili kuvuruga amani ambapo Dk. Shein amejitahidi kuhakikisha hilo halitokei.
Alisema kuwa Dk. Shein ameshajenga
misingi imarana na amejitahidi katika miaka mitano kwa kuijenga Zanzibar mpya
sambamba na kufungua milango ya kuimarisha uwekezaji ili kuhakikisha uchumi
unaimarika kwani nia yake ni kuondoa umasikini.
Alisema kuwa uchaguzi sio shwangwe na
matusi bali uchaguzi ni takwimu, na tayari kwa upande wa takwimu CCM imejipanga
vizru hivyo shangwe hizo ni kazi bure.
Alisema kuwa mara hii CCM haikubali
kuibiwa kura zake kisiwani humo kama ilivyozoeleka na kusema kuwa mara hii CCM
imejipanga kuhakikisha uporaji wa kura zao unadhibitiwa.
Wapo wafusi wa CUF ambao wameshajua kuwa
CUF imeuzwa na wamesema hawakubali kwani chama hicho hakina Mgombea Mwenza.
Aidha, alieleza kuwa chama cha CUF
kinajisifu kuwa tayari kimeshawapata ma PO na ma PC ambao watawasaidia katika
kufanya vile watakavyowaamuru na kusema kuwa atakaejaribu kuiba kura hatua za
kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Waziri Aboud alisema kuwa wafusi wa chama
hicho cha upinzani wamekuwa wakijisifu kuwa mara hii watahakikisha wanaiba kura
na kuitaka Tume ya Uchaguzi kulitambua jambo hilo ambalo ni njia moja wapo ya
kuvuruga amani.
Alisema kuwa chama hicho kimejipanga kwa
lengo la kuwa wamejipanga kuwa na Mawakala wengi ili kufanya uharibifu mara hii
hakuna kugaiwa juisi, maji, pilau kwani mara hii CCM imejipanga vizuri kwa
Mawakala wake.
Nae Balozi Amina Salum Ali alisema kuwa CCM
itaendelea kuuonesha ulimwengu kuwa iko hai na itaendelea kuongoza taifa la
Tanzania na kuwataka wanaCCM kuendelea kukiunga mkono chama chao hicho.
Alisema kuwa CUF haina itikadi wala Sera
na kushangwazwa kama kweli hayo yapo basi maendeleo makubwa yangeweza
kupatikana na kueleza kuwa kinachofanyika ni hadaa.
Alisema kuwa upinzani hawaelewi Utaifa
kwani viongozi wa vyma vya upinzani hawawaelezi wananchi na wafuasi wao umuhimu
wa Utaifa na badala yake huwatia kasumba kwa lengo la kuichukia Serikali yao.
Alisema kuwa maendeleo yanayotekelezwa na
Dk. Shein ni kwa ajili ya wananchi wote na kuwaeleza kuwa hata viongozi wa
upinzania wanajua kuwa hakuna maendeleo kama hakuna Sera.
CCM ndio chama pekee kinachoimarisha
maendeleo, na kusema kuwa CCM inawajali wananachi wote wa Tanzania na Serikali
zote mbili zimekuwa zikileta maendeleo kwa wananchi wote bila ya kuwabagua.
Kwa upande wa akina mama, Balozi amina
alisema kuwa akina mama wa Mtambwe wana nguvu ya kuwashawishi akina baba
kuiunga mkono CCM ili baadae wasije kujutia na kusisitiza kuwa Dk. Shein
amekuwa akihakikisha kuwa maendeleo yanafikiwa na wananchi wote hapa Zanzibar.
Waziri wa Kilimo na Maliasili, Dk. Sira
Ubwa Mwamboya alisema kuwa Mtambwe ya leo sio ile ya miaka mitano iliyopita
kwani huduma zote muhimu zipo na kushangwazwa na kiongozi wao mkuu Edward
KLowasa kudai kuwa akipata uongozi atapeleka elimu, afya na Mamlaka Kamili na
kueleza kuwa hayao yote yapo yameshaletwa na CCM.
Aliwataka wananchi kuwapigia kura
viongozi wote wanaogombania nafasi kwa upande wa CCM.
Nae Balozi Ali Karume ambaye pia ni
Mjumbe wa Halmahsuri Kuu ya CCM aliwataka wanaCCM na wananchi wa Mtambwe kuwapa kura viongozi wa
CCM akiwemo Dk. Ali Mohamed Shein, Dk. Magufuli, Wabunge, Wawakilishi na
Madiwani wa CCM.
Hakuna kitu ambacho unaweza kukitetea
kama hukiamini hivyo alisisitiza kuwa ipo haja ya kumchagua Dk. Shein huku
akieleza kuwa CCM ina historia kuwa tokea ASP katika suala la ushindi na mwaka
huu CCM itaendelea kushinda.
Aliwataka wananchi wa Pemba kutoregeza
kamba katika zao la karafuu kwa kudanganyika kuwa kuna mafuta yatakayochimbwa
kwa siku mia moja na kueleza kuwa anauhakika na anaamini kuwa Dk. Shein atapandisha
tena bei zao la karafuu baada ya kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Zanzibar.
Nao viongozi wa CCM Mkoa wa Kaskazini
Pemba chini ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo Hamad Mberwa walipongeza juhuddi
zinazochukuliwa na viongozi wa CCM katika kuimarisha chama hicho huko katika
Mkoa wa Kaskaziani Pemba.
Aidha, viongozi hao walitumia futrsa hiyo
kuwaeleza historia ya Mtambwe ilivyokuwa hapo kabla na hivi sasa ilivyo kwani
maendeleo makubwa yamepatikanwa huko Mtambwe.
Katibu wa CCM Mkoa wa Kaskazini
Pemba, alisema kuwa Mtambwe ya sasa ni
Mtambwe ya Dijitali na sio ile iliyozoeleka kwani tayari wameshatambua ukweli
uko wapi na chama kipi cha kukiunga mkono ili kiwaletee maendeleo.
Baadhi ya Wananchama wa CCM wakiwa wameshikilia mabango yanayotoa ujumbe "KUBADILI CHAMA SIO KURTADI NA VYAMA HAVIMTII MTU PEPONI YUSEMANE"katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi uliofanyika leo katika kijiji cha Makoongeni Jimbo la Mtambwe Kaskazini Pemba.
Ahsanteni wananchi wa Jimbo la Shaurimoyo Mkoa
wa Mjini Unguja kwa kuja kwa wingi sana kwenye mkutano wa hadhara kumsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM katika uwanja wa Urafiki,jimbo la Shaurimoyo katika wilaya ya mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mgombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. Ali Mohamed Shein ameahidi katika kipindi kijacho akichaguliwa tena atahakikisha kuwa jitihada zaidi zinaelekezwa katika kuimarisha sekta binafsi nchini.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la uchaguzi la Shaurimoyo leo huko katika uwanja wa urafiki Unguja Mjini, Dk. Shein amesema serikali inatambua kuwa haiwezi kufanya kazi pekee hivyo ushirikiano kati ya sekta umma na binafsi ni wa lazima.
“sekta binafsi ni injini ya maendeleo hivyo katika kipindi kijacho mkinichagua tena nitahakikisha sekta hiyo inaimarishwa na ushirikiano kati ya sekta hiyo na sekta ya umma unapewa kipaumbele” Dk. Shein alieleza.
Aidha alibainisha kuwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya sekta hizo ni miongoni mwa mikakati ya Serikali atakayoingoza kuongeza ajira hasa kwa vijana kwa kuwa ushirikiano huo utasaidia katika kuweka na kuimarisha mazingira mazuri zaidi ya kuvutia uwekezaji hivyo kuzalisha nafasi nyingi zaidi za ajira.
Katika mnasaba huo amewataka vijana wasihadaike na ‘porojo’ za baadhi ya wanasiasa wanaowaahidi ajira bila ya kuwa na mpango maalum wa kuzalisha ajira hizo.
“Hawana mpango wowote wanatumia lugha za kuwahadaa ili muwape kura na lakini Ilani ya CCM inaonesha wazi mipango yake ya kuzalisha ajira na tayari imeonesha kwa vitendo katika kipindi kinachomalizika sasa” Dk. Shein alisisitiza.
Sambamba na ahadi hiyo mgombea huyo wa CCM alisema kupitia Ilani ya chama chake kuwa akichaguliwa tena ataendelea na jitihada za kuimarisha usihirikika kwa kuwapatia mafunzo ya uongozi na uendeshaji wanachama 15,000 wakiwemo viongozi 3,000.
Katika kutatua tatizo la kujaa kwa maji katika baadhi ya maeneo ya jimbo hilo pamoja na maeneo ya jimbo la Kwahani, Dk. Shein aliahidi kuujenga upya mtaro wa maji machafu na mvua katika maeneo hayo ili kuepusha maeneo hayo kujaa maji na hata kusababisha magonjwa ya miripuko.
Kuhusu utekelezaji wa Ilani kwa kipindi cha mwaka 2010-2015, Dk, Shein alibanisha kuwa ahadi katika jimbo hilo zimetekelezwa ikiwemo uimarishaji wa hospitali ya Mikunguni ambayo pamoja na kutoa matibabu mengine sasa imekuwa kituo kikuu cha matitabu ya macho katika eneo la mjini Unguja.
Katika awamu ijayo ameahidi kutekeleza ombi la wananchi wa jimbo hilo la kupanua hospitali hiyo kwa kuongeza gorofa nyingine lakini hilo aliahidi kulifanyia kazi baada ya wataalamu kuruhusu upanuzi huo.
Katika mkutano huo ambao ulivutia wananchi wengi wa jimbo hilo na maeneo mengine ya mji wa Zanzibar Dk. Shein aliahidi akichaguliwa tena ataendelea na mpango wa kumarisha huduma za jamii ikiwemo maji, afya, elimu na miundombinu ya kiuchumi.
Mjumbe wa Kamati kuuya CCM na Makamo wa Pili wa Rais balozi Seif Ali Iddi akiwasalimia wananchi na wanaCCM katika Mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi katika uwanja wa mpira Urafiki jimbo la Shaurimoyo Mjini Unguja leo.
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya Kitaifa ya CCM Balozi Amina Salim Ali akitoa salam zake kwa wanachama wa CCM na wananchi wengine waliohudhuria katika Mkutano wa Kampeni za Uchaguzi zilizofanyika katika kiwanja cha mpira cha Urafiki jimbo la Shauri Moyo kilichopo Wilaya ya Mjini Unguja
Ahsanteni wananchi wa Jimbo la Nungwi Kaskazini Unguja kwa kuja kwa wingi sana kwenye mkutano wa hadhara kumsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed shein akizungumza na Wanachama wa CCM na Wananchi wapenda amani katika uwaja wa mpira Nungwi Wialaya ya Kaskazini A mkoa wa kaskazini Unguja leo katika mkuatno wa hadhara wa kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika hivi karibuni.
KAMPENI YA UCHAGUZI NUNGWI
Mgombea Urais wa
Zanzibar kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amehutubia
mkutano mkubwa wa aina yake wa kampeni katika mji mdogo wa Nungwi katika mkoa
wa Kaskazini Unguja na kuwataka wananchi kukichagua chama hicho kwa kuwa ndicho
kinachothamini na kinachotekeleza malengo ya Mapinduzi ya mwaka 1964.
Aliwaambia maelfu ya
wananchi waliohudhuria mkutano huo kuwa wanapaswa kuichagua CCM kwani ndicho
chama chenye uwezo na kimeonesha mfano wa utekelezaji wa malengo ya Mapinduzi
na ahadi za Rais wa kwanza wa Zanzibar hayati Mzee Abeid Amani Karume.
“Mapinduzi ndiyo
yaliyoweka msingi wa usawa na kuondosha ubaguzi ambao uliwanyima haki na
kuwakandamiza wananchi walio wengi wa Zanzibar” Dk. Shein alieleza.
Katika mnasaba huo alisema
kuwa Mapinduzi yalileta usawa na kujenga mazingira ya kuijenga nchi yetu kwa
ushirikiano na kwa umoja wetu na kwa maslahi yetu wote.
Mgombea huyo wa CCM
alisema Zanzibar ni maarufu ulimwenguni kote tokea karme nyingi zilizopita
lakini umaarufu huo hautakuwa na manufaa kwetu endapo hatutaweza kulinda na
kuienzi amani na utulivu uliopo.
Katika kipindi
kijacho aliahidi kuimarisha huduma za jamii ikiwemo elimu, afya, umeme na maji pamoja
na miundombinu ya barabara ili kukidhi mahitaji makubwa ya huduma hizo kutokana
na mji huo kupanuka sana kutokana na shughuli za biashara ya utalii.
“Tutaimarisha huduma
za umeme kwa kuweka transfoma kubwa yenye KVA 200 katika mji mpya ulioko Ras
Nungwi itakayoweza kuhudumia wateja wengi na kwa uhakika zaidi” Dk. Shein
alisema na kuongeza kuwa mji huo mdogo utawekewa taa za barabarani hadi
Kivunge.
Dk.Shein aliwaeleza
wananchi hao kuwa biashara ya utalii ndio inayoipatia Zanzibar fedha nyingi za
kigeni hivyo lengo la Serikali katika miaka mitano ijayo ni kuongeza idadi ya
watalii wanoitembelea Zanzibar ifikie 500,000 ifikapo 2020 kutoka 300,000 hivi
sasa huku jitihada zikielekezwa katika kuimarisha uwezo wa wananchi kitaaluma wa
kuweza kuhudumia sekta hiyo.
Aliwaeleza wananchi
hao kuwa kupanua haraka kwa mji Nungwi ni uthibitisho kuwa Nungwi inaendelea kusonga
mbele kwa kujenga majengo mengi na hoteli nyingi za kitalii.
Dk. Shein aliahidi
atakapochaguliwa tena Serikali yake itawajengea uwezo wavuvi nchini kwa
kuwapatia boti zenye ukubwa wa kati na kubwa ili waweze kuvua kwa uhakika na
kupata mapato makubwa zaidi.
Kwa upande wa kilimo
cha mwani, dk. Shein alisema ataiamarisha masoko la mwani kwa kutafuta masoko
mapya ya zao hilo ili wakulima waweze kupata bei nzuri na kufaidi jasho lao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed shein akiteta jambo na Naibu katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar Vuai Ali Vuai wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika uwanja wa mpira Nungwi Wilaya
ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM NEC na Waziri wa ardhi,maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban akielezea wananchi na wanaCCM kuhusu suala zima la Uchimbaji wa mfuta katika mkutano wa hadhara wa
kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika uwanja wa mpira Nungwi Wilaya ya Kaskazini A Unguja leo.
Wanachama wa CCM na Wapenda amani wakinyoosha mikono yao juu kuashiria kuunga mkono maneno na sera zilizotolewa na mjumhe wa Kamati Kuu ya CCM Khadija Hassan Aboud leo wakati wa Mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika Nungwi Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa kaskazini Unguja katika uwanja wa mpira.
Ahsanteni wananchi wa Jimbo la Bumbwini kwa kuja kwa wingi sana kwenye mkutano wa hadhara umsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wananchi na wanachama wa CCM Jimbo la Bumbwini wilaya ya Kaskazini B Mkoa wa kaskazini Unguja leo, katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM ulifanyika uwanja wa Skuli ya Bumbwini Makoba ikiwa ni mfulilizo wa mikutano inayoendelea.
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia
Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. Ali Mohamed Shein ameahidi kuwa moja ya mambo
muhimu atakayasimamia endapo atachaguliwa tena kuiongoza Zanzibar ni kuendelea
kuimarisha mazingira ya kuaminiana, kuvumiliana, kupendana na kushirikiana
miongoni mwa wananchi wake.
“katika kipindi kilichopita tumefanya
kazi kubwa ya kuwaunganisha wananchi kwa kujenga mazingira ya uvumilivu,
kuaminiana, kuvumiliana na kushirikiana” Dk. Shein aliuambia mkutano mkubwa wa
kamperni huko Bumbwini Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja.
Alisema kuwa serikali yake
atakayoiunda itahakikisha kuwa amani na utulivu Zanzibar inaendelea kuimarika
siku hadi siku, miezi hadi na miezi na mwaka hadi mwaka na kusisitiza kuwa
hatafanya ajizi katika kuwashughulikia watu wanaotishia amani na utulivu.
“Mimi ni Rais ninayejiamini, wananchi
mlinipa kura kuwaongoza na nimekuwa nikitekeleza majukumu yangu ya Urais kwa
mujibu wa Katiba na Sheria hivyo hakuna haja ya kutishana katika kuongoza” Dk.
Shein alieleza.
Alifafanua kuwa serikali si ya
vingozi iwe Rais, Makamu wa Rais, Mawaziri au Makatibu Wakuu bali ni ya
wananchi hivyo asitokee kiongozi mmoja kumtisha mwingine kwani kufanya hivyo ni
kujidanganya.
“wananchi amueni wenyewe msitishike
chagueni viongozi mnaowataka wala msitishike kwani hiyo ni haki yenu ya
kikatiba kufanya hivyo” Dk. Shein aliwaambia maelfu ya wananchi hao waliokuwa
wakikatisha hotuba yake mara kwa mara.
Katika Mkutano huo uliohutubiwa na
makada mbali mbali wa chama hicho,Dk. Shein alieleza hatua kwa hatua
utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi katika jimbo hilo na kuanisha kuwa katika
kipindi kilichopita aliahidi kujenga kituo cha afya Kiongwe ambacho tayari
kimejengwa pamoja na kujenga skuli ya Pangatupu.
Alibasisha kuwa katika kio0jdi
kijacho serikali itajenga kitilo cha afya Pangatupu ili kuziweka huduma za afya
karibu na wananchi.
Mgombea huyo wa CCM aliahidi
kuendelea kuimarisha huduma za jamii katika wilaya hiyo pamoja na miundombinu
ya barabara.
Aliwataka wananchi kumchagua tena
kushika nafasi ya urais wa Zanzibar na kumchagua Dk John Pombe Magufuli kwa
nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wagombea wengine wa chama
hicho katika nafasi za ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Dk. Shein ataendelea na kampeni zake
kesho kwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara huko Nungwi katika mkoa Wilaya ya
Kaskazini ‘A’.
Ahsanteni wananchi wa Jimbo la Mkoani kwa kuja kwa
wingi sana kwenye mkutano wa hadhara kumsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na
Wananchi na wanachama wa CCM Jimbo la Mkoani Mkoa wa kusini Pemba, katika uwanja wa mpira wa Makombeni, mkutano huo wa hadhara wa
kampeni za CCM ulifanyika leo ikiwa ni mfulilizo wa mikutano inayoendelea.
Mgombea nafasi ya
urais kupitia Chama cha Mapinduzi-CCM Dk. Ali Mohamed Shein amesema endapo
atachaguliwa tena kuongoza Zanzibar atahakikisha Shirika la Meli na Mamlaka ya
Bandari yanaimarishwa kwa kufanyiwa marekebisho makubwa ili kuyawezesha
kujiendesha kibiashara kama ilivyofanyika kwa Shirika la Biashara la Taifa
(ZSTC).
Akizngumza katika
mkutano wa kampeni huko Makombeni wilaya ya Mkoani, mkoa wa Kusini Pemba leo,
Dk. Shein alisema taasisi hizo mbili za serikali ni lazima zijiendeshe
kibiashara na kuacha kupokea ruzuku serikalini.
“Baada ya kununua
meli kubwa itakayowasili hivi karibuni tutanunua meli nyingine mpya yenye
ukubwa kama MV Maendeleo na pia meli nyingine ya mafuta kuchukua nafasi ya MV
Ukombozi ambayo pamoja na meli ya MV Maendeleo ya sasa zitauzwa kwa kuwa zimeshapitwa
na wakati” alifafanua Dk. Shein.
Kwa upande wa Mamlaka
ya Bandari aliwaeleza maelfu ya wananchi waliofika katika mkutano huo kuwa
katika kipindi kijacho Serikali itaendelea kuimarisha Mamlaka hiyo kwa
kuiwezesha na kuifanya itekeleze majukumu yake kwa ufanisi na kutengeneza
faida.
Mgombea huyo wa CCM
alisema kuwa ahadi zake kwa majimbo ya wilaya ya Mkoani alizozitoa katika
mkutano wa kampeni kama huo tarehe 3 Oktoba 2010 zimetimizwa na kueleza kuwa
matengenezo makubwa ya bandari ya Mkoani aliyoahidi yamekamilika.
“Matengenezo ya
bandari tumekamilisha na kipindi kijacho tutaiimarisha zaidi kwa kuiwekea vifaa
bora” alieleza Dk. Shein na kuonesha kukerwa na kauli za baadhi ya wanasiasa wa
upinzani kukejeli bandari hiyo.
“bandari yetu sasa
ina uwezo wa kupokea mizigo mingi na lazima tutukuze chetu badala ya kutuza vya
wengine,kukejeli jitihada zetu si uungwan” alisema Dk. Shein na kuongeza kwa
methali isemayo “usitukane wakunga na uzazi ungaliko”
Alitaja kukamilika
kwa ujenzi wa barabara za mkoa wa Kusini Pemba kuonesha utekelezaji wa Ilani ya
mwaka 2010-2015 zikiwemo barabara za Mizingani-Wambaa, Mtambile-Kangani,
Mtambile-Mwambe,Chajaani– Pujini, Chanjamjawiri-Tundauwa na
Mtuhaliwa-Mkanyageni.
Katika mkutano huo
uliojaa shamrashamra za wana CCM na wananchi na kuonesha kujiamini kupata
ushindi, Dk. Shein aliwaeleza wananchi hao kuwa katika kipindi kijacho jitihada
zaidi zitaelekezwa katika kuimarisha ubora wa elimu pamoja na kuendelea
kuimarisha miundombinu katika sekta ya elimu.
“Baada ya mafanikio
makubwa katika kuimarisha miundombinu katika sekta ya elimu katika kipindi
kijacho mazingatio sasa yatawekwa katika kuhakikisha kiwango cha elimu yetu
kinaimarika ili watoto wetu wengi zaidi waweze kufaulu kwa madaraja ya juu
katika mitihani ya kidato cha nne na cha sita na hatimae kuwawezesha kujiunga
na vyuo vikuu kwa wingi” Dk. Shein alifafanua.
Aidha katika kipindi
hicho alibainisha kuwa serikali itaimarisha elimu ya watu wazima ili kuongeza
kiwango cha wananchi wanaojua kusoma na kuandika kutoka 85 hivi sasa hadi
asilimia 95 mwaka 2020.
Kwa upande wa skuli
za maandalizi aliendelea kubainisha kuwa katika wilaya ya Mkoani hivi sasa
tayari vimejengwa vituo 26 kama alivyoahidi mwaka 2010 na miaka mitano ijayo
serikali itajenga vituo vingine 34.
Dk. Shein aliwaeleza
kuwa kwa upande wa afya serikali katika kipindi kijacho itavipandisha vituo 38
vya afya kuwa daraja la pili ikiwa ni miongoni mwa hatua za kuimarisha huduma
za afya katika wilaya hiyo.
Aliwaeleza wananchi
kuwa ujenzi mpya wa hospitali ya Abdalla Mzee unaendelea na hospitali hiyo
itakuwa kubwa na ya kisasa. Aitumia fursa ya mkutano huo kumshukuru Rais wa
Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping kwa msaada wa ujenzi wa hopsitali hiyo
pamoja na kuwezesha ujenzi wa bandari mpya ya Mpigaduri.
Dk.Shein anatarajiwa
kuondoka hapa kesho asubuhi kuendelea na kampeni zake kisiwani Uguja ambapo
kesho hiyo jionia atahubia mkutanowa kampeni huko Nungwi mkoa wa Kaskazini
Unguja.
Mjumbe wa Sekretarieti ya kamati Maalum ya
Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar Haji Mkema alipokuwa akiwaombea kura Wagombea
nafasi za
Uongozi katika Chama cha Mapinduzi CCM wakati wa Uchaguzi Mkuu
ukifika,katika jimbo la Mkoani katika mkutano wa hadhara wa kampeni
zilizofanyikaleo uwanja wa Makombeni Wilaya ya Mkoani Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Zanzibar pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein
akiwatambulisha wagombea Udiwani wa CCM kwa Wananchi na wanachama wa CCM Jimbo
la Mkoani Mkoa wa kusini Pemba, katika uwanja wa mpira wa Makombeni, wakati wa
mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM ulifanyika leo ikiwa ni mfulilizo wa
mikutano inayoendelea.
Ahsanteni sana wananchi wa Jimbo la Kojani kwa kuja kwa wingi katika Kiwanja cha Kiuongoni kuja kumsikiliza Dr Ali Mohamed Shein kwenye kampeni zinazoendelea Tarehe 3/10/2015.
Mgombea Urais Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza
nawanachama wa CCM,Wananchi wapenda amani waliohudhuria katika mkutano wa hadhara wa
kampeni za CCM za kuombe kura wagombea nafazi za Uongozi katika Chama
hicho,uliofanyika leo uwanja wa Mpira Kijiji cha Kiungoni Jimbo la Kojani Wilaya ya
Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa NEC pia Waziri wa rdhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban alipokuwa akizungumza na
wananchi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Kojani Wilaya ya wete
Mkoa wa Kaskazini Pemba katika kijiji cha Kiungoni wakati wa
mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM uliofanyika leo uwanja wa Mpira Kijijini
hapo, mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein
Aliyekuwa Balozi Jumuiya ya Nchi za Afrika Nchini Marekeni Bi. Amina
Salum Ali alipokuwa akizungumza na wananchi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi
Jimbo la Kojani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba,wakati alipokuwa akiwaombea
Kura wagombea nafasi mbali mbali wa CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika
leo uwanja wa Mpira Kijiji cha Kiungoni.
READY 2 GO. Hakuna kurudi nyuma , hakuna kuchelewa.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa NEC Balozi Ali Abeid Amani
Karume allipokuwa akizungumza na wananchi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi
Jimbo la Kojani Wilaya ya wete Mkoa wa Kaskazini Pemba katika kijiji cha
Kiungoni wakati wa mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM uliofanyika
leo uwanja wa Mpira Kijijini hapo, mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali
Mohamed Shein.
Vijana waliojitoa katika Chama cha CUF na kuingia CCM wakinyoosha mikono
juu kuonesha ishara ya kuunga mkono chama cha Mapinduzi kwa uwezo wake
wakuelezea sera zake kwa Wanachama katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika
Uwanja wa Kiungoni jimbo la Kojani Wilaya ya Wete Pemba leo,yake mbali mbali
inayofanyika Unguja na Pemba
Ahsanteni wananchi wa Jimbo la Gando kwa kuja kwa wingi kumsikiliza mgombea Urais wa Zanzibar kupitia
Chama Cha Mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein leo hii tarehe 02/10/2015.
WANANCHI kisiwani Pemba wametakiwa kuwachagua viongozi wa CCM ambao watakaa
pamoja na wao na sio wale viongozi wanaowachagua kutoka vyama vya upinzani ambao
wakishapata nafasi za uongozi huwakimbia na kutojali matatizo yao.Hayo yalielezwa leo na baadhi ya Viongozi
wa CCM Zanzibar, katika Mkutano wa
Kampeni ya uchaguzi wa CCM uliofanyika katika Jimbo la Gando, Mkoa wa Kaskazini Pemba uliohudhuria na
maelfu ya wanaCCM na wananchi ambapo mgeni rasmi alikuwa mgombea Urais wa
Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali Mohamed Shein.Viongozi hao walieleza kuwa viongozi wa
vyama vya upinzani wanaochaguliwa na wananchi kisiwani Pemba mara baada ya
kupata nafasi za uongozi huhamisha makaazi yao kisiwani humo na kuwasahau
waliowachagua.
Katika mkutano huo Balozi Seif alisema kuwa amekuwa akipata amaelezo kutoka kwa
wanachama wa CUF kuwa hivi sasa wamechoka kudanganywa na kuwaambia kuwa umefika
wakati wa wao kujiunga na CCM."CUF imekuwa sawa na timu ya mpira
kila siku ikiingia uwanjani inapigwa mabao hiyo si timu kwa nini wewe ubaki
huko njooni CCM Sera zake zinatelezeka tizameni ndani ya miaka mitano
ilivyofanya... na karibu tunatengeneza barabara ya Wete- Chake"alisema
Balozi.Alisema kuwa Dk. Ali Mohamed Shein
amefanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kutekeleza ahadi ya kununua meli mpaa
ambayo itaingia nchi wakati wowote na Dk. Shein ndie atakae izindua.Aidha, alisema kuwa CCM haitaki fujo wala
shari huku akishangwaza na mgombea urais wa CUF ambaye ameanza kugombea nafasi
hiyo tokea ujana wake.Aliwataka wananchi kujiunga na CCM kwani
ni chama ambacho hakijawahi kushindwa.
Nae Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho alitumia fursa hiyo
kueleza kuwa miundombinu ya barabara Pemba imeimarika na kutoa shukurani kwa
Dk. Shein kwa maendeleo yaliopatikana kisiwa humo. Kificho alisema kuwa Zanzibar imeimarika
kutokana na amani iliyopo hatua ambayo imepelekea kukua kwa sekta za maendeleo
ikiwemo sekta ya utalii.Aidha, alisema kuwa chama vyama vya
upinzani vimekuwa havina hoja kutokana na maendeleo makubwa yaliofikiwa
kisiwani humo na ndio maana vimekuwa
havizungumzii kuhusu maji, barabara, umeme, afya, elimu na sekta
nyenginezo hiyo ni kutokana na kuwa vyote hivyo vimetekelezwa na Serikali ya
CCM.Alieleza kuwa kinachofanywa na vyama
hivyo hivi sasa ni kudandia hoja ambazo tayari zimekuwa zikifanyiwa kazi na
Serikali kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM chini ya uongozi wa Dk. Shein huku
akieleza haja ya Dk. Shein kupewa kura za ndio ili maendeleo zaidi yaweze
kupatikana Unguja na Pemba.Aliwataka wananchi hao wa Pemba
kutowachagua viongozi ambao mchezo wao ni kukimbia katika vyombo vya kutunga
sheria kama walivyofanya katika Baraza la Wawakilishi, Bunge la Katiba na Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nae Waziri Kiongozi Mstaafu Shamsi Vuai Nahodha aliwaomba wananchi
wa Pemba kujua kuwa viongozi waa CUF wameshindwa kufanya kazi za siasa na
kuwaauliza viongozi wa chama hicho hata kujenga madarasa wanasubiri mamlaka
kamili.
Aliwataka wananchi wa
kisiwa cha Pemba kufanya mabadiliko na kuwachagua viongozi wa CCM kwani
viongozi wote waliowachagua katika uchaguzi uliopita
Ahsanteni wananchi wa Jimbo la Kiwani kwa kuja kwa wingi kumsikiliza mgombea Urais wa Zanzibar kupitia
Chama Cha Mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein leo hii tarehe 01/10/2015.
Ahsanteni wananchi wa Jimbo la Paje kwa kuja kwa wingi kumsikiliza mgombea Urais wa Zanzibar kupitia
Chama Cha Mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein leo hii tarehe 29/9/2015.
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
DK.SHEIN
SUALA LA MAFUTA LISIPOTOSHWE KWA MANUFAA YA KISASA.
Mgombea Urais wa
Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema suala la
mafuta kutolewa katika mambo ya muungano ni matokeo ya jitihada za pamoja kati
ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja
na viongozi wake hivyo asitokee mtu au chama kikalitumia suala hilo kama lake
binafsi.
“Hakuna haja ya
mbwembwe wala kujisifu wote katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano tulishirikiana na kushauriana pamoja kwa muda
mrefu hadi kufikia hatua ya kupitisha sheria ya mafuta katika kikao cha Bunge
cha mwezi Julai 2015” Dk. Shein alisema.
Akizungumza katika
mkutano wa kampeni huko Paje leo katika jimbo la uchaguzi la Paje, Mkoa wa
Kusini Unguja, Dk. Shein amesema wako baadhi ya wanasiasa Zanzibar wanalitumia
suala hilo kama mtaji wa kisiasa kwa kuwaeleza wananchi kuwa hatua iliyofikia
sasa ni jitihada zao binafsi.
Katika mkutano huo
ambao ulivunja rekodi za mahudhurio tangu kufanyika mkutano wa uzinduzi wa
kamepeni, Dk. Shein amesema suala hilo limekuwa likipotoshwa kwa makusudi kwa
manufaa ya kisiasa hasa wakati huu wa kampeni.
“ningewaelewa
wenzangu hawa kama wangewaeleza wananchi kuwa hatua iliyofikiwa ni jitihada za
serikali yetu ambao wao ni washirika katika serikali lakini kusema wao ndio
waliofanikisha jambo hili inasikitisha na si jambo la kiungwana” Dk. Shein
alieleza na kuongeza kuwa kama ni sifa angeweza kujisifu yeye kwani ndie
aliyekuwa msimamizi mkuu pamoja na Rais Kikwete.
Alisema yeye amefanya
ziara katika nchi za Uholanzi na Ras El Khaima ambako alifanya mazungumzo na
kutia saini makubaliano ya awali ya ushirikiano katika kuendeleza sekta hiyo
pamoja na kufanya mazungumzo na makampuni mengi yenye azma ya kuja kushiriki
katika kuendeleza sekta ya mafuta na gesi.
Dk. Shein alibainisha
kuwa baada ya kuwepo makampuni ya kutafuta mafuta Tanzania mwaka 2002 wakati
huo akiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alimtuma aliyekuwa
Waziri wa Nishati wakati huo Edgar Maokola Majogo kuzungumza na Waziri mwenzake
wa Zanzibar wakati huo Burhan Saadat kuhusu suala hilo uchimbaji wa mafuta.
“Majibu ya
mashauriano hayo yalikuwa ni kuwa suala hilo lisiharakishwe kwa kuwa linahitaji
mashauriano zaidi” Dk. Shein alisimulia na ndipo mazungumzo yalipoanza.
Mgombea huyo wa CCM
aliwaeleza wananchi kuwa jitihada za kuliondoa suala la mafuta katika mambo ya
muungano lilijadiliwa katika Bunge la Katiba lakini baada ya kuwa mchakato huo
haukukamilika yeye na Rais wa Jamhuri ya Muungano walilipeleka suala hilo kwa
wanasheria wakuu ili kutumia bunge kulikamilisha na ndivyo lilivyofanyika.
“Ilikuwa ni busara
yetu viongozi kulipelekea suala hili kwa wanasheria wetu wakuu baadae
tukalijadili katika vikao vyetu hadi sheria kupitishwa bungeni” Dk. Shein
alisisitiza.
Hata hivyo aliongeza
kuwa ni jambo la kushangaza watu hao wanaojinasibu kuwa wamefanikisha suala
hilo ndio hao hao waliopinga suala hilo na kukimbia bungeni wakati sheria ya
mafuta ilipokuwa ikipitishwa.
Akibainisha zaidi Dk.
Shein kuwa wakati hayo yakiendelea huku Serikali ya Zanzibar ilikuwa
ikitayarisha sera yake na kudokeza kuwa imekamilika pamoja na kwamba rasimu ya
sheria iko tayari ikisubiri kupitishwa katika Baraza la Wawakilishi ili kazi ya
kuendeleza sekta ya mafuta na gesi ianze kwa kasi.
Aliwataka wananchi
wasihadaike na maneno ya viongozi hao kuwa uchimbaji huo utaanza mara moja na
kuwatahadharisha kuwa hadi kuyachimba mafuta itachukua sio chini ya miaka
mitano.
DK.
SHEIN: NICHAGUENI TENA TUENDELEE KUSHIRIKIANA KWA KUONGEZA KASI YA KUIJENGA
ZANZIBAR.
Mgombea wa nafasi ya
urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewataka
wananchi kumpa tena fursa ya kuongoza ili waendelee kushirikiana kuijenga
Zanzibar.
Amesema katika
kipindi cha miaka mitano kinachomalizika sasa Zanzibar imepiga hatua kubwa
kimaendeleo kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM hivyo
kumchagua tena yeye na chama chake kuongoza ni fursa nyingine kwa wananchi wa
Zanzibar kuendeleza kasi ya maendeleo ya nchi yao.
Katika mkutano wa
kampeni uliofanyika huko Paje katika jimbo la uchaguzi la Paje,Mkoa wa Kusini
Unguja, mgombea huyo wa CCM aliueleza umati mkubwa wa wananchi ambao haujawahi
kutokea kuwa ahadi alizozitoa kwa jimbo hilo katika mkutano wa kampeni kama huo
mwaka 2010 zimetekelezwa na kuahidi kuongeza kasi ya utekelezaji wa Ilani mpya
ya chama hicho ya mwaka 2015-2020.
“Tumetekeleza Ilani
yetu kama tulivyopanga katika sekta ya afya, elimu, maji, umeme na sekta ya
utalii”na kuongeza kuwa kwa sekta ya barabara utekelezaji umeanza na
utakamilishwa katika kipindi kijacho.
Alifafanua kuwa baada
ya kukamilisha kuifanya hospitali ya Makunduchi kuwa ya wilaya, Serikali
itaendelea kuimarisha huduma za afya katika mkoa huo kwa kuiimarisha hospitali
ya Kivunge na kituo cha afya cha Paje kwa kivipatia vifaa na wataalamu wa afya.
“Kazi ya kuipandisha
hospitali ya Makunduchi kuwa ya wilaya imekamilika kwa kuiwekea vifaa vipya na
kuwapatia madaktari wakiwemo kutoka nje ya nchi na tunatarajia kuongeza majengo
mengine mapya kuiwezesha hospitali hiyo kuwahudumia watu wengi zaidi” alieleza Dk.
Shein na kuongeza kuwa hivi sasa hata wananchi wa mjini wanafika katika
hospitali hiyo kufuata huduma.
Aliongeza kuwa Serikali
hivi karibuni ilifungua kituo kipya cha afya huko Kajengwa Makunduchi ikiwa ni
sehemu utekelezaji wa mpango wa Serikali wa uimarishaji wa huduma za afya
nchini.
Dk. Shein aliwaeleza
wananchi hao kuwa katika kipindi kijacho Serikali itajenga dakhalia katika
skuli ya sekondari Paje Mtule ambayo ni skuli mpya ya kisasa ambayo imejengwa
ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya mwaka 2010 -2015 ya kuimarisha elimu nchini.
Katika kuendelea
kuimarisha elimu, Dk. Shein ameahidi katika kipindi cha miaka mitano ijayo
kuzipatia skuli zote za sekondari kompyuta ili ziweze kwenda na mabadiliko ya
sayansi na tekinolojia.
Kuhusu ahadi ya
kusambaza umeme vijijini, Dk. Shein alieleza kuwa utekelezaji wake umezidi asilimia mia na kwa
upande wa Paje ni maeneo machache yaliyobaki na kuahidi kukamilishwa muda mfupi
ujao baada Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) kwa kuweka transfoma mpya.Mgombea huyo wa CCM
anatarajiwa kwenda Pemba kuendelea na kampeni zake kesho.
Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia wananchi katika mkutano huo. |
Mzee Kwacha akiwahutubia wananchi waliojaa sana kupita kiasi katika Uwanja wa Paje. |
Baadhi ya wananchi na wanachama cha Mapinduzi CCM wakiwangalia kikundi
cha sarakasi kikitoa burudani wakati wa mkutano wa CCM uliofanyika leo jimbo la Paje uwanja wa
mpira Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja katika kampeni zinazoendelea
Ahsanteni wananchi wa Jimbo la Mtopepo katika Uwanja wa Garagara kwa kuja kwa wingi kumsikiliza mgombea Urais wa Zanzibar kupitia
Chama Cha Mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein leo hii tarehe 28/9/2015.
VIONGOZI wa CCM Zanzibar wamewataka wananchi wa Zanzibar kuendeleza amani,
utulivu na mshikamano uliopo na kuwaonya wale wote wanaokusudia kufanya vurugu
wakati wa uchaguzi mkuu wajue kuwa Serikali pamoja na vyombo vyake vya Dola viko macho. Viongozi hao waliyasema hayo leo katika
Mkutano wa Kampeni ya uchaguzi wa CCM
uliofanyika katika uwanja wa Garagara, Jimbo la Mtopepo, Mkoa wa Mjini Magharibi uliohudhuria na maelfu ya wanaCCM na
wananchi ambapo mgeni rasmi alikuwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya
CCM, Dk. Ali Mohamed Shein.
Nae Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd alisema kuwa vyama vya upinzani hawana Sera na hoja na hivi sasa wamebaki kubwabwaja.
Balozi Seif alisisitiza haja ya
kuimarishwa kwa umoja na mshikamano kwa wananchi na wanaCCM kwa jumla na kusema
kuwa umoja ndio silaha ya kushinda kwa CCM.
Alisema kuwa kuwepo kwa amani na utulivu ni
jambo la lazima na kuwaonya wale wote waliodhamiria kufanya fujo wakati wa
uchaguzi kuachana na azma yao hiyo na kuwaonya wanachama wa CUF wasije kujaribu
kufanya fujo huku akiwataka wazee wa Darajabovu kutowaachia vijana wao kufanya
fujo.
Aidha, Balozi Seif aliwataka wazee wasije
kuilaumu Serikali iwapo watoto wao watafanya fujo kwani Dola haijaribiwi wala
haichezewi na kueleza kuwa anaetaka kujaribu akale muhogo ajue kama ni mtamu
ama mchungu lakini sio serikali.
Alisema kuwa Serikali iko macho kwa
kuwadhibiti wale wote walio na lengo la kufanya vurugu siku ya tarehe 25 na 26. Alisema kuwa huu si wakati wa kuwasemea
wananchi, na hakuna serikali ya mkataba kwani serikali ya mkataba lengo lake ni kuvunja Muungano, na CCM haiko tayari
kuwepo kwa serikali ya Mkataba na kueleza kuwa CCM wanachokijua wao ni serikali
mbili.
Nae Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu
Ameir Kificho alitumia fursa hiyo kwa kusema kuwa Dk. Shein ni mtu muadilifu,
makini, muangalifu na katika maamuzi yake hakurupuki na kwa mwenendo na tabia
hizo hakuna mgombea wa urais wa kumpa kura nyingi za ndio isipokuwa Dk. Shein.Kificho aliwaomba wananchi kuwapeleka Wawakilishi
wa CCM na Wabunge wa CCM kwani wao ndio wanaofanya kazi vizuri kwa maendeleo ya
Watanzania na wananchi wa Zanzibar kwa jumla na hawana mtindo wa kutoka toka
katika nyumba hizo za kutunga sheria.
Nae Waziri wa Maji,Ardhi na Nishati
Ramadhani Abdalla Shaaban alishangazwa
na kauli za CUF zinazosema kuwa ndani ya
miaka 50 Zanzibar haina maendeleo na kusema kuwa mbali ya miaka hiyo wanayosema
wapinzani tayari ndani ya miaka mitano tu ya Dk. Shein maendeleo yaliopatikana
Unguja na Pemba ni makubwa. Alieleza kuwa tayari wanaCCM na wananchi wameshaamua tarehe 25 kummiminia kura zote Dk. Shein na kusema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya CCM uchumi umeimarika.
Pamoja na hayo, alieleza kuwa angalau CUF wanakiri kuwa kifungu cha Katiba mpya inayopendekezwa cha 23 na 26 kimeelezea kwamba ardhi, mafuta na gesi yatashughulikiwa na Zanzibar, na kusema kuwa kinachosubiriwa ni wakati wa kuipigia kura Katiba inayopendekezwa ifanye kazi.
Alisema kuwa tayari Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Dk. Shein wameshakubaliana juu ya Sheria ya mafuta na gesi, na tayari sheria hiyo imeshakwenda kwenye Bunge la Muungano kwa lengo la kuwa Zanzibar ishughulikie wenyewe rasilimali hizo.
Ahsanteni wananchi wa Mkokotoni kwa kuja kwa wingi kumsikiliza mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi
Dr Ali Mohamed Shein.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dr Ali Mohamed Shein akiwahutumia wana CCM waliofika kwenye kiwanja cha Mkokotoni kwenye mkutano wa kampeni ya uchaguzi mkuu tarehe 27/9/2015. |
VIONGOZI wa CCM Zanzibar wameeleza kuwa hoja inayotolewa na chama cha CUF ya
kutaka kuleta Mamlaka Kamili ni dhamira ya kumrejesha Sultan kuja kuiongoza
Zanzibar kwa njia ya mlango wa nyuma.
Viongozi hao waliyasema hayo leo katika
Mkutano wa Kampeni ya uchaguzi wa CCM
uliofanyika katika uwanja wa Sun Rise, Mkokotoni, Mkoa wa Kaskazini Unguja
uliohudhuria na maelfu ya wanaCCM na wananchi ambapo mgeni rasmi alikuwa
mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali Mohamed Shein.
Alisema kuwa CUF hawana hoja na
kushangazwa na kauli inayotoa kuwa Zanzibar haina Mamlaka kamili wakati tayari
Zanzibar inayo mamlaka Kamili ila nia ya chama hicho ni kurudisha uongozi wa
Kifalme.
Alisema kuwa viongozi wa CUF wameishiwa
hoja na hawana la kuwaambia wafuasi wao na hivi sasa wamekuwa wakitumia jina
lake kwa kunokesha mikutano yao. "labda kwa kwa sababu mimi mweusi na siwezi
kujifanya mweupe kama Jusa",alisema Balozi Seif.
"Kama mimi mweusi ndio alivyoniumba
Mungu sasa na wale waliokuwa na vilema visivyoonekana inakuwaje",alisema
Balozi na kueleza mwaka huu CUF wanaanguka
huku akisisitiza kuwa Serikali inatolewa kwa nguvu za kura.
Aidha, Balozi Seif Ali Idd, alisema kuwa
CUF hawana ajenda na liliopo hivi sasa ni kubwabwaja na kuwaeleza wanaCCM
kilichobaki ni kwenda kupiga kura tarehe 25 mwezi huu, na CCM kupata ushindi na
kueleza kuwa CUF haina ubavu wa kuishinda CCM.
Balozi Seif alisema kuwa tayari chama cha
CUF wanajua kuwa mara hii wanashindwa na
ndio maana wamekuwa wakipita kununua vitambulisho vya kupigia kura kwa
wanaCCM.
Alieleza kuwa mikakati wanayopaka ya
kufanya vurugu Oktoba 24, 25 na 26, tayari imeshajulikanwa na kutumia fursa
hiyo kuwata wazee wa CUF wa Mkoa wa Kaskazini kutowaachia watoto wao kufanya
vurugu na kusema kuwa vyombo vya dola havichezewi na kuwataka wasije wakailaumu
Serikali na kutowaachia watoto wao kuingia mtegoni, wasije kufanya vuru, wala
maandamano.
Alisema kuwa mambo mengi ya vurugu wanayokusudia
kufanya CUF wanayajua na wana ushahidi nayo na huku akieleza kuwa ipo siku
watayatoa. "Chokochoko kachokoe pweza...CCM haichokolewi iko imara na
ukifanya mchezo itakushughulikia",alisema Balozi Seif.
Alisema kuwa Oktoba 25 mwaka huu ni siku ya ushindi wa CCM hivyo kila
mmoja aende mapema kupiga kura na kuwahakikishia wananchi kuwa siku ya uchaguzi
ulinzi wa kutosha utakuwepo kwa ajili yao na watalindwa wakati wote.
Nae Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri
Kiongozi Mstaafu Shamsi Vuai Nahodha alisema kuwa Mamlaka kamili ya Zanzinar yalipatikanwa
tokea mwaka 1964 chini ya Marehemu Mzee Abeid Karume na hakuna mtu yeyote wala
kikundi chochote cha watu ambacho kina uwezo wa kufanya hivyo hivi leo.
Alisema kuwa wanachokusudia kukifanya
chama hicho kwa kutaka Zanzibar iwe mwanachama wa Umoja wa Mataifa, iwe na safaru
yake, Wizara yake ya mambo ya nje yake ni jambo la kushangazwa kwani taifa
lolote duniani haliwezi kuwa na viti viwili katika umoja wa Mataifa wala
haiwezekani kuwa na sarafu mbili wala Wizara mbili za Mambo ya nje ndani ya
taifa moja.
Shamsi aliendelea kuwashangazwa na CUF kutaka
kuanzisha Mamlaka kamili na kueleza kuwa chama hicho na kile cha CHADEMA msiimamo wao unafanana
lakini dhamira zinatofautiana kwani lengo lao ni kuvunja Muungano kwa kutumia
lugha ya ulaghai.
Alisema kuwa dhamira ya CHADEMA ni
kuwarubuni CUF ili kuwaunga mkono na kuwa na mgombea mmoja wa Jamhuri ya
Muungano na la kusikitisha zaidi ni kuwa CHADEMA kimefanikiwa, kuvidhoofisha vyama
vya CUF na NSSR MAGEUZI. Pia alieleza kuwa CCM itaendelea kuunga mkono sera ya
Serikali mbili.
Alieleza kuwa CCM inaamini kuwa Sera ya
Serikali mbili ndio yenye uwezo wa kuongoza serikali, na kusisitiza kuwa Sera
ya Serikali tatu haina uwezo wa kuulinda Muungano wala kuyalinda Mapinduzi ya
Januari 12, 1964.
Kwa upande wa Muungano alisema kuwa
Wazanzibari wamekuwa wakinufaika na Muungano na kueleza kuwa Tanzania Bara wapo
Wazanzibari wanaopata huduma kadhaa za maisha ya mwanaadamu ikiwemo ardhi, maji
safi na salama na huduma nyenginezo bila
ya bughudha.
Shamsi alishangazwa na wale wote
wanaosema kuwa Muungano hauna maana na kueleza kuwa ipo haja ya kutafuta mada
nyengine na sio hiyo.
Akieleza juu ya vitendo vinavyofanywa na
viongozi wa CUF, alisema kuwa wapo wanachama na viongozi wanapita kwenye
Majimbo kununua vitambulisho vya kupigia kura na kueleza kuwa Sheria ya
uchaguzi inasema kuwa mwananchi yeyote wa Zanzibar aliesajiliwa kwenye Daftari,
haijalishi kuwa shahada yake, imepotea ama imenunuliwa au imeibiwa, ana haki ya
kupiga kura.
Hivyo aliiomba Tume ya Uchaguzi
kuhakikisha kila Mzanzibari mwenye Shahada na asie na shahada wakati jina lake
limo kwenye Daftari la kupiga kura ipewe fursa hiyo.
Nae Bi Amina Salum Ali aliwataka wananchi
wa Kaskaznini kutobabaishwa na maneno ya wapinzani huku akieleza miongoni mwa
mafanikio yaliopatikana katika Mkoa huo ikiwa ni pamoja na uimarishwaji wa
miundombinu ya barabara pamoja na huduma nyengine za kijamii.
Aidha, aliendelea kueleza kufarajika
kwake na mipango ya Dk. Shein ya kuimarisha sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha Zanzibar inalima na kuzalisha mchele wake wenyewe.
Nae Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheir ambaye pia ni mgombea
Uwakilisgi Jimbo la Tumbatu,alisema kuwa WanaCCM wanasubiri siku ya tarehe 25
Oktoba mwaka huu kukirejesha madarakani chama hicho.
Mapema Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Kaskazini Unguja Haji Juma Haji, alisikitishwa na kauli za chama cha CUF
zinazoelezwa katika mikutano yao kuwa Zanzibar itaongozwa na wale walioondoshwa
mwaka 1964 pamoja na kuwahakikishia wananchi kuwa Serikali hiyo itaingia madarakani
na wale wote waliochukuliwa mashamba yao wanawarudishiwa mashamba yao kwani
yamechukuliwa kwa dhulma.
Alieleza kuwa wanaCCM wanaamini kuwa
uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa huru, haki na amani, na kusema kuwa vitendo vinavyofanywa
na CUF katika Mkoa huo hawaridhiki kwani wameanza kuchana picha za wagombea wa
CCM na kuwataka vijana wa Mkoa wa Kaskazini wasikubali kutumiwa na CUF kufanya
hivyo.
Alisisitiza kuwa Mkoa wa Kaskazini
ushindi hauna mbadala, huku akishangazwa wale wanaoparamia miti na kuanza
kuchana picha za wagombea wa CCM"Waanaparamia
miti kwaru kwaru utazani kima wanagombana na picha zisizosema waje kugombana na
mimi Haji Juma nnosema',alisema Haji.
Ahsanteni wananchi kwa kuwa pamoja kwenye sala ya Eid na Baraza la eid hapo Mkokotoni. Mungu atujaalie Zanzibar yenye kuendelea na amani na baraka tele. Kesho tarehe 27 tunakuja tena Mkokotoni tuwe pamoja kumsikiliza mgombea urais urais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein katika kampeni za uchaguzi mkuu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dr Ali Mohamed Shein akiwahutumia wananchi katika Baraza la Eid katika sikukuu hii ya mfungo tatu iliofanyika Mkokotoni Kaskazini Zanzibar. |
HOTUBA YA
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI, MHE. AL-HAJJ DK. ALI
MOHAMED SHEIN, KATIKA
BARAZA LA
IDD- EL-HAJJ: 24 SEPTEMBA, 2015
SAWA NA
MWEZI 10 MFUNGUO TATU, 1436 HIJRIA
BISMILLAH
RAHMAN RAHIM
Naanza kwa kushuhudia kuwa hapana Mola
anayestahiki kuabudiwa kwa haki na viumbe vyote isipokuwa Mwenyezi Mungu
Mtukufu Subhana Wataala. Yeye ndiye
Muumba wa Dunia na Akhera na kwake Yeye ndiyo marejeo ya viumbe vyote. Tunakiri kwa kauli na kuitakidi kwa moyo kuwa
Mtume Muhammad (S.A.W) ni Mtume wake wa haki na kigezo chema cha uchamungu kwa
waumini sote.
Rehema na amani ya Mwenyezi Mungu
zimshukie Mtukufu wa daraja na mbora wa viumbe; Sayyidna Muhammad (S.A.W), Aali
na Sahaba zake pamoja na waumini wote waliofuata njia yake ya uongofu hadi siku
ya kiama. Tumuombe Mola wetu (SW)
atujaalie na sisi tulio hai, ndugu, jamaa na wale wote waliokwishatangulia
mbele ya haki tuwe miongoni mwao. Atupe
ubainifu wa kuyafanya mambo ya kheri na tuyaepuke
mambo ya shari na maovu, ili tuweze kufanikiwa hapa Duniani na huko Akhera
tuendako. Amin!
Mheshimiwa
Sheikh Khamis Haji Khamis;
Kadhi
Mkuu wa Zanzibar.
Mheshimiwa
Maalim Seif Sharif Hamad;
Makamu wa
Kwanza wa Rais,
Mheshimiwa
Balozi Seif Ali Iddi;
Makamu wa
Pili wa Rais,
Mheshimiwa
Dk. Amani Abeid Karume,
Rais
Mstaafu wa Zanzibar;
Mheshimiwa
Pandu Ameir Kificho;
Spika wa
Baraza la Wawakilishi,
Mheshimiwa
Omar Othman Makungu;
Jaji Mkuu
wa Zanzibar,
Waheshimiwa
Mawaziri,
Waheshimiwa
Mabalozi,
Wageni
Waalikwa,
Ndugu Wananchi,
Mabibi na
Mabwana,
Assalamu
Aleikum Warahmatullahi Wabarakatuh
IDDI
MUBARAK
Ndugu Wananchi,
Nimeanza hotuba yangu kwa kumtukuza
Mola wetu (SW) na kukiri kuwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) ni Mtume wa haki wa
Mwenyezi Mungu ambaye ni wajibu wetu kumsalia, kuyazingatia na kuyafuata
mafundisho yake ili tuweze kufanikiwa katika kuyatekeleza maamrisho ya Mwenyezi
Mungu na tujiepushe na yale yote tunayokatazwa kuyafanya. Kupitia mafundisho ya Mtume (S.A.W)
kutoka kwa Mwenyezi Mungu, tumetakiwa tuitekeleze ibada ya Hijja kwa kila
mwenye uwezo katika nyumba tukufu iliyopo Makka huko Saud Arabia. Mwenyezi Mungu katika aya ya 97 ya Surat Aali
Imran anatufahamisha uzito na umuhimu wa kuitekeleza ibada ya Hijja kwa kusema:
“Na kwa ajili ya Mwenyezi
Mungu imewawajibikia watu wafanye Hijja katika nyumba hiyo, kwa yule awezaye
kwenda huko. Na atakayekufuru
(atakayekanusha) basi Mwenyezi Mungu si muhitaji kuwahitaji walimwengu”.
Ndugu
Wananchi,
Leo tunaungana katika furaha ya sikukuu
ya Idd el Hajj na waislamu wenzetu kwa maelfu kutoka mataifa mbali mbali, wa
rangi na hadhi mbali mbali walioitikia wito wa Mola wetu kwenda kuitekeleza
Ibada ya Hijja katika mji Mtukufu wa Makka.
Kwa hakika, hii ni neema kubwa kwetu kwani wapo wenzetu wengi miongoni
mwetu ambao hawakuweza kuifikia siku hii.
Kwa hivyo, ni wajibu wetu kumshukuru Mola wetu kwa kuturuzuku neema hii
ya kuifikia siku hii, ambapo ni miezi
michache tu iliyopita, tulijaaliwa kuisherehekea sikukuu ya Idd-el-Fitri kwa
amani na salama. Tunamshukuru Mwenyezi
Mungu kwa kutujaaliya siku hizi za furaha na kuwa pamoja katika kuzisherehekea.
Ndugu
Wananchi,
Ni jambo la kutia moyo na kumshukuru
Mwenyezi Mungu kuona kwamba idadi ya mahujaji wa Zanzibar imekuwa ikiongezeka
kila mwaka. Katika mwaka huu wa 2015, taasisi zinazosafirisha mahujaji hapa
Zanzibar kutokana na uongozi bora na uzoefu wa kuzifanya shughuli za Hijja za
Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana zimeweza kusafirisha mahujaji 1,502, kati
ya mahujaji 3,000 waliosafirishwa kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Idadi hii ni ziada ya mahujaji 222
ikilinganishwa na idadi ya mwaka jana ambapo taasisi za Zanzibar zilisafirisha
mahujaji 1,280 kati ya 2,500 kwa Tanzania nzima. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewekewa
fursa ya kupeleka katika Hijja, mahujaji
25,000 kwa mujibu wa makubaliano ya OIC.
Ni dhahiri kuwa idadi ya mahujaji wetu kwa sasa ni ndogo ikilinganishwa
na nchi nyingine za Afrika ya Mashariki.
Aidha, imebainika kuwa mahujaji wetu wengi wanaokwenda Hijja ni watu wa
hali za kati na hali za chini kiuchumi. Wengi wao huifanya ibada hii baada ya
kupata fedha zao za kiinua mgongo.
Kwa lengo la kuwasaidia wananchi wengi
zaidi waweze kupata fursa ya kuitekeleza ibada ya Hijja kwa wepesi na mapema
zaidi, tayari Serikali imeanza kazi ya kufanya upembuzi yakinifu ili kuanzisha
Mfuko wa Hijja Zanzibar. Mfuko huo utakapoanzishwa, watu wengi zaidi watapata
nafasi na uwezo wa kuweka fedha kidogo kidogo kwa mujibu wa uwezo wao. Hatimae,
watamudu kutekeleza ibada za Hijja na Umra kwa mujibu wa makubaliano na taratibu
zitakazowekwa na mfuko. Nchi nyingi
ambazo zimeanzisha mifuko ya aina hii ikiwemo Malaysia, wanamudu kumaliza idadi
yote ya nafasi za mahujaji walizowekewa.
Bila ya shaka, kwa kupitia utaratibu wa
mfuko huu, mahujaji wetu watapata uwezo wa kufanya maandalizi mazuri ya
misafara ya Hijja. Kadhalika, kwa miezi yote Waumini wengi watapata nafasi ya kwenda
kutekeleza ibada za Umra na ziara.
Mifuko hii pamoja na kuwawezesha Waislamu kuhiji husaidia sana shughuli
za kidini na kijamii. Tayari Kamisheni
ya Wakfu ya Mali ya Amana kwa kushirikiana na Benki ya Kiislamu ya PBZ, Mfuko
wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF), Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC), Umoja wa Taasisi
za Hijja Zanzibar na wataalamu wa Uchumi na Utawala kutoka taasisi za kiislamu
wanalifanyia kazi suala hili na
matarajio ni kuanza kufanya kazi kabla ya Hijja ijayo. Tumuombe Mwenyezi
Mungu atufanyie wepesi katika kulitekeleza jambo hili la kheri.
Ndugu
Wananchi,
Ibada ya Hijja waliyoitekeleza ndugu
zetu mahujaji huko Makka ina mchango muhimu wa kukuza imani ya mja na uchamungu
wake kutokana na mafunzo muhimu yanayotokana na ibada hiyo yenye historia ndefu
tangu kwa baba wa Mitume Nabii Ibrahim (AS).
Miongoni mwa mafunzo muhimu ya ibada ya
Hijja ni kudhihirika kwa umoja wa Waislamu duniani ambao wanakutanika katika Mji
wa Makka kwa kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu. Umoja wa waislamu umebainishwa
katika aya mbali mbali za Kurani ambapo katika aya 92 ya Surat Al-Anbiyaa,
Mwenyezi Mungu ametuthibitishia hilo na kututaka tumuabudu Yeye kwa kusema,
“Hakika umma wenu huu ni
umma mmoja tu, na mimi ni Mola wenu, basi niabuduni”.
Hali hii ya umoja, tunapaswa tuione
umuhimu wake na tuiendeleze katika maisha yetu ya kila siku hasa sisi tunaoishi
katika nchi moja na watu wa nasabu moja.
Sote tuna wajibu wa kuimarisha umoja wetu na kuepukana na masuala yote
yanayohatarisha umoja na mshikamano wetu kwa lengo la kutafuta radhi za Mwenyezi
Mungu na kupiga hatua kubwa zaidi za maendeleo.
Ndugu
Wananchi,
Jambo jengine muhimu linalotokea katika
kipindi cha ibada ya Hijja ni Waislamu kutoka sehemu mbali mbali duniani kupata
fursa ya kukutana na kujadili masuala yanayohusu maendeleo ya jamii ya kiislamu
katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na ustawi wa jamii. Katika hali kama hii, masuala mengi ya msingi
huzungumzwa na Waislamu wenye taaluma, maarifa, uzoefu na kubadilishana mawazo
kwa njia ya majadiliano na kupata njia za kukabiliana na changamoto za
maendeleo zilizopo. Fatwa zinazotolewa
miongoni mwa maulamaa wa kiislamu, huwa ni dira muhimu katika kuleta ustawi wa
jamii zetu.
Hili nalo ni jambo la kuliendeleza
katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbali mbali zilizomo katika jamii
yetu. Majadiliano ni njia nzuri na ya
pekee katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto zetu za maendeleo ndani ya jamii
yetu. Ni wazi kwamba, jamii haiwezi
kupata maendeleo kama watu watakosa kushirikiana na kuaminiana. Kwa hivyo, kwa kutumia maarifa yanayotokana
na mafunzo ya Ibada ya Hijja ni miongoni mwa faida tunazozipata katika
utekelezaji wa Ibada hii na ni wajibu wetu tuyatumie mafunzo hayo katika maisha
yetu ya kila siku.
Ndugu
Wananchi,
Vile vile, katika ibada ya Hijja tunajifunza umuhimu wa mahujaji kuwa na subira na kwa wale tunaobaki nasi huwa tunawasubiri
ndugu, jamaa na marafiki zetu waliokwenda kuitekeleza ibada hii kwa lengo la
kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu. Ibada
ya Hijja inajumuisha taratibu nyingi pamoja na ugumu wa safari, gharama na haja
ya kuwa na uzima wa afya na ustahamilivu.
Yote haya yanahitaji kuwa na subira ambayo ni sifa muhimu ya Mitume yote
na Masahaba. Kwa wale wanaoondokewa na
ndugu na jamaa zao kwa ajili ya kwenda kuitikia wito huo wa Mwenyezi Mungu nao
hulazimika kuwa na subira.
Kuwa na subira ni jambo lililosisitizwa
sana katika Kurani na Sunnah kupitia visa vya Mitume wa Mwenyezi Mungu na
Masahaba ili iwe ni mafunzo kwetu.
Katika kusisitiza faida ya kuwa na subira kwa muumini, Bwana Mtume
(S.A.W) katika hadithi iliyopokelewa na Al-Bukhaariy na Ahmad amesema:
“Kubakia katika subira kwa
siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu ni bora zaidi kuliko dunia na vyote
vilivyomo ndani yake”
Ni dhahiri kuwa kuna fadhila kubwa
katika kusubiri kwa siku hizi ambazo wenzetu wanatekeleza ibada ya Hijja huko
Makka na sisi tunaowasubiri tukiwaombea dua ili ibada zao zikubaliwe. Aidha, masheikh wetu wanatuelekeza kuwa
subira yenye malipo zaidi ni ile ya kusubiri kwa kujizuwia kutekeleza mambo
mabaya kwa kutegemea malipo mema kutoka kwa Mola wetu Subhana Wataala. Tumuombe Mwenyezi Mungu atupe subira kwa
kutegemea fadhila na kufuata maamrisho ya Mola wetu.
Ndugu
Wananchi,
Miongoni mwa masuala muhimu
tuliyosuniwa katika sikukuu hii ya Idd el Hajj ni kuchinja mnyama. Uchinjaji huu unatupa funzo la utiifu wa
Nabii Ibrahim (AS) na kutawakali kwake pamoja na mwanawe Ismail (AS) katika
kutekeleza amri ya Allah kupitia ndoto aliyooteshwa. Utiifu wao wa kweli kwa Mwenyezi Mungu
uliwawezesha kufuzu, jambo ambalo la mazingatio kwetu sote na kujifunza ili
tuweze kufanikiwa katika masuala yetu mbali mbali ya kimaisha.
Mafundisho ya uislamu yanasisitiza
umuhimu wa kuitekeleza suna hii ambayo ni ibada na hatua ya kumkurubisha mja na
Mola wake. Siku hii ya leo imesuniwa
kuchinja mnyama baada ya sala ya Idd na kutumia sehemu ya nyama na nyengine
kuwapa marafiki na wahitaji wengine waliokuwa hawana uwezo katika jamii.
Ni wajibu wetu kuyaendeleza mambo kama
haya ya kheri na uchamungu ili iwe ni sababu ya kukuza mapenzi mema baina yetu
na kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu kwa kufanya anayoyaridhia na kujiepusha na
makatazo yake. Kadhalika, tuendelee
kuyatumia mafunzo yanayotokana na ibada zetu kwa vitendo ili iwe ndiyo dira ya
kuleta ufanisi katika maisha yetu ya kila siku.
Ndugu
Wananchi,
Tuna wajibu mkubwa wa kumshukuru
Mwenyezi Mungu Mtukufu kutuwezesha kuungana na waislamu wenzetu duniani katika
kuisherehekea sikukuu hii ya Idd el Hajj katika hali ya amani na salama. Nimepata faraja kubwa kuweza kushirikiana na
waislamu wenzetu wa Mkoa huu wa Kaskazini Unguja kwa kusali pamoja sala ya Iddi
leo asubuhi katika kiwanja cha mpira cha Polisi Mkokotoni na hivi sasa kwa
pamoja tumejumuika katika kituo hiki cha Mafunzo ya Amali kwa ajili ya Baraza
la Iddi.
Natoa shukurani zangu na naipongeza
Kamati ya Maandalizi kwa kushirikiana vyema na uongozi wa Mkoa wa Kaskazini
Unguja pamoja na Wilaya zake katika kuifanikisha shughuli hii. Kadhalika, nawapongeza kwa dhati wananchi
wote wa Mkoa huu kwa kujitokeza kwa wingi katika sala ya Idd na kwa
mashirikiano yenu mnayoendelea kutupa. Tumuombe Mwenyezi Mungu azidishe
ushirikiano huu katika kuifanikisha mipango yetu ya maendeleo na kuimarisha
ustawi wa wananchi wote.
Ndugu
Wananchi,
Nimefarajika na hatua kubwa ya
maendeleo tuliyoyafikia katika Mkoa huu wa Kaskazini Unguja katika sekta za
kiuchumi, huduma za jamii na muamko wa wananchi katika kuzitumia fursa mbali
mbali za kujiendeleza kiuchumi kwa kushirikiana na Serikali. Napenda nikupongezeni sana kwa mafanikio
hayo.
Katika kuhakikisha kuwa, Mikoa yetu
inazidi kuimarika kiuchumi, kuongeza fursa za ajira hasa kwa vijana na
kuimarisha upatikanaji mzuri wa huduma za jamii, Serikali imeazimia kujenga mji
wa kisasa katika Mkoa huu wa Kaskazini kwenye vijiji vya Kijini na
Matemwe. Ujenzi wa barabara wenye urefu
wa kilomita 20.2 kutoka Matemwe kupitia Kijini hadi Kidoti umekwishaanza.
Wananchi wa Mkoa huu wananufaika na kuwepo kwa idadi kubwa ya hoteli za kitalii
kwa kuzingatia kauli mbiu ya utalii kwa wote.
Ndugu
Wananchi,
Inatia moyo kuona vijana na kinamama wa
Mkoa huu walivyojidhatiti kujiendeleza kiuchumi kwa kutengeneza bidhaa mbali
mbali na kuzalisha mazao kwa ajili ya kuuza katika Hoteli za kitalii. Aidha, wananchi wengi wa maeneo ya Bumbwini,
Mkokotoni, Bwekunduni, Fungurefu na vijiji nyengine vya Mkoa huu wameimarisha
uchumi wao kwa kujishughulisha na biashara ya madagaa ambayo nimearifiwa kuwa
husafirishwa hadi Kongo na nchi nyengine za jirani.
Wito wangu kwenu ni kuwa muendelee kushirikiana
na Serikali yenu katika kuziimarisha shughuli zetu hizi ili ziweze kutoa tija
zaidi. Kadhalika, vijana wanaokosa fursa
ya kuendelea na masomo wakitumie kituo cha Mafunzo ya Amali cha Mkokotoni ili
wajiendeleze kupata ujuzi wa kazi mbali mbali za amali unaotolewa na kituo
hicho. Kazi hizo ni pamoja na useremala,
ushoni, uchoraji, uwashi, ufundi bomba, magari, mafriji, mapishi ya aina mbali
mbali na huduma za mahoteli. Vile vile,
katika mwezi wa Agosti, 2015 tulifungua kituo cha ujasiriamali “Bare-foot
College” kama kiliopo huko India, kituo kinachotengeneza vifaa vya umeme wa jua
ndani ya Mkoa huu ambacho ni cha aina yake na maalum kwa kinamama. Hizo ni fursa ambazo mnapaswa kuzitumia vyema
katika kupiga hatua zaidi za maendeleo.
Ndugu
Wananchi,
Serikali kwa kushirikiana na washirika
wetu wa maendeleo pamoja na ushirikiano wa wananchi tumeweza kupiga hatua kubwa
katika kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika Mkoa huu
kwa kutekeleza miradi mbali mbali. Hali
ya upatikanaji wa maji safi katika Mkoa huu imefikia asilimia 71.68. Mafanikio hayo yamefikiwa baada ya kutekeleza
miradi mikuu mitatu ya maji safi na salama katika Mkoa huu. Miradi hiyo ni mradi wa Serikali kupitia
Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Mradi wa Maji wa Ras-al-Khaimah na Mradi wa
Maji wa ADB ambayo kwa pamoja imewanufaisha wananchi mbali mbali wa Mkoa huu
kupata huduma za maji safi na salama.
Kadhalika, Serikali imeimarisha huduma
za hospitali ya Koteji ya Kivunge pamoja na vituo vya afya vyengine katika Mkoa
huo ili kuziimarisha afya za wananchi.
Wajibu wa wananchi ni kuzitumia huduma hizi pamoja na wazazi na walezi
kuhakikisha watoto wetu wanapelekwa kupata chanjo ili kuwakinga na maradhi
mbali mbali na kinamama wajawazito wawe wanajifungulia hospitali katika azma ya
kuziimarisha afya zao.
Ndugu
Wananchi,
Pamoja na mafanikio hayo katika
kuziimarisha huduma za jamii, napenda nitumie fursa hii, kuutaka uongozi wa
Mkoa wa Kaskazini; Unguja kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na taasisi
zinazowasimamia madereva wachukue hatua madhubuti katika kukabiliana na tatizo
la ajali za barabarani katika Mkoa huu. Taarifa kutoka Jeshi la Polisi zinabainisha
kazi kubwa tuliyo nayo katika kukabiliana na tatizo la ajali za
barabarani. Kwa mujibu wa taarifa hiyo,
katika kipindi cha kuanzia mwezi wa Januari hadi Agosti mwaka 2014, jumla ya
ajali za barabarani 391 zimetokea Unguja na Pemba. Ajali hizo zilizosababisha vifo vya watu 104
na watu 728 wamejeruhiwa. Katika Mkoa
huu wa Kaskazini Unguja zilitokea ajali 64 zilizosababisha vifo vya watu 16 na
jumla ya watu 259 walijeruhiwa.
Katika mwaka huu wa 2015 kwenye kipindi
kama hicho, tayari zimetokea ajali za barabarani 393 Unguja na Pemba ikiwa ni
ziada ya ajali mbili ikilinganishwa na mwaka 2014. Ajali hizo zimesababisha vifo vya watu 91 na watu
450 wamejeruhiwa. Katika kipindi hiki
kwenye Mkoa huu, kumetokea ajali za barabarani 73, zilizosababisha vifo vya
watu 15 na kuwajeruhi watu 123. Ni wazi
kuwa takwimu hizo si za kufurahisha, kwa hivyo jitihada za pamoja zinahitajika
ili kupunguza na hatimae kuliondoa kabisa tatizo la ajali za barabarani kwa
vile asilimia kubwa ya ajali hizi zinasababishwa kwa kutokuzingatiwa kwa sheria
za usalama barabarani na matumizi mazuri ya barabara zetu.
Ndugu
Wananchi,
Kwa mara nyengine napenda nikumbushe
umuhimu wa sisi viongozi wa kisiasa, kijamii na wa madhehebu ya dini
kuwasisitiza wafuasi wetu umuhimu wa kuilinda amani na kujiepusha na vitendo
vyote vinavyoweza kutuondolea amani na utulivu tuliokuwa nao. Nimekuwa nikisema mara kadhaa kuwa amani
haina mbadala. Bila ya amani hatuwezi kupata
maendeleo yoyote. Kutokuwepo kwa amani
kunahatarisha uhai wa watu na ni sababu ya kuharibu miundombinu ya aina mbali
mbali na kuzua fadhaa katika jamii. Ni
dhahiri kuwa kutoweka kwa amani huwaondolea wasaa hata waumini katika kutekeleza
ibada za kumuwabudu Mola wao. Katika aya
ya 112 ya Suratun Nahl, Mwenyezi Mungu anatutanabahisha kwa kutupa mfano wa
waliopewa neema ya amani na utulivu wakashindwa kuitunza kwa kusema:
“Na Mwenyezi Mungu
anakupeni mfano wa mji uliokuwa na amani na utulivu, riziki yake ikiujia kwa
wingi kutoka kila mahali. Lakini
ukazikufuru neema za Mwenyezi Mungu, kwa hivyo Mwenyezi Mungu akauvika vazi la
njaa na khofu kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyafanya”.
Tumuombe
Mwenyezi Mungu atuepushe na mtihani huo.
Napenda nikuhakikishieni kuwa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitaendelea kukabiliana na wale wote watakaofanya vitendo
vinavyoashiria kutaka kuvunja amani ya nchi yetu wakati wote na katika kipindi
hiki cha Kampeni za Uchaguzi Mkuu, wakati wa uchaguzi na baada ya
uchaguzi. Hakuna atakayeonewa au
kudhulumiwa kwa njia yoyote ile lakini Serikali ina wajibu wa kikatiba wa
kuwalinda watu wote na mali zao pamoja na wageni wanaoitembelea nchi yetu.
Ndugu Wananchi,
Hivi sasa tumo katika kusherehekea sikukuu,
lakini kama tunavyofahamu baada ya siku chache zijazo tunatarajia kuanza kupata
baraka za mvua za Vuli. Mvua ni neema
kubwa kwetu hasa kwa kuendeleza shughuli za kilimo na upatikanaji wa maji
nchini. Kwa hivyo, ni vyema tukaanza maandalizi ya kilimo cha mazao na matunda
mbali mbali yanayostawi na kunawiri katika msimu wa Vuli.
Kwa upande mwengine, ni muhimu
tukazingatia kwamba baadhi ya nyakati, Mwenyezi Mungu hutupa neema ya mvua
ambayo vile vile huwa na mitihani ili kuzipima nafsi zetu. Mwenyezi Mungu
ametuambia katika Surat Muhammad aya ya 31 kwamba:
“Nitakufanyieni mitihani
mpaka muwadhihirishe (wajulikane) wale wanaopigania dini miongoni mwenu, na
wanaosubiri nasi tutadhihirisha habari zenu”.
Sote tunakumbuka jinsi baadhi ya
wananchi wenzetu walivyopata mitihani ya mafuriko katika sehemu mbali mbali za
Unguja na Pemba katika msimu wa mvua za Masika uliopita. Tulishuhudia matukio
mengi ya kusikitisha katika maeneo ya Kwahani, Mwanakwerekwe, Tomondo na
kadhalika, katika mwezi Mei, 2015. Mimi
na viongozi wengine tulipata fursa ya kuwatembelea wananchi waliopata maafa kwa
ajili ya kuwafariji.
Napenda niwakumbushe wananchi kwamba
katika nyakati mbali mbali, Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini “Tanzania
Meteorological Agency (TMA)”, imetahadharisha kwamba katika msimu wa mvua
za Vuli, upo uwezekano mkubwa wa kutokea mvua kubwa za “El-Nino” kutokana
na hali ya sasa ya kuongezeka kwa joto katika Bahari ya Pasifiki. Ongezeko
hilo la joto katika bahari hiyo kama litaendelea kuwepo, linaweza kuenea
hadi katika Bahari ya Hindi na kusababisha mvua kubwa za “El-Nino” katika
ukanda wote unaopakana na bahari ya Hindi.
Kwa kawaida mvua kubwa za “El-Nino”
zinapolikumba eneo la nchi husababisha mafuriko na kuacha madhara makubwa
ya uharibifu wa miundombinu na mali za wananchi; hasa nyumba zilizojengwa
katika maeneo ya mabondeni. Wataalamu
wetu wanatufahamisha kwamba kuna viasharia vingi sana vya kuonesha uwezekano wa
mvua za “El Nino” kutokea mwaka huu katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
Huu ni utabiri wa binaadamu lakini
Mwenyezi Mungu ana kudra na shani yake. Utabiri huu unatokana na elimu na
maarifa aliyotupa Subhana Wata’ala, ili kurahisisha maisha yetu. Ni vyema tukaitumia
elimu hii vizuri kwa kuanza kuchukua tahadhari zinazofaa. Nasaha zangu kwenu
wananchi ni kwamba tuzingatie hekima ya ule usemi maarufu kwamba, “Tahadhari kabla ya athari”. Kwa hivyo, taasisi zinazoshugulikia usafi wa
miji ziongeze kasi katika kusafisha misingi ya maji machafu na njia za maji,
usafi wa mazingira yetu ili kuepukana na maradhi. Ninawanasihi wananchi tuache ujenzi katika
sehemu za mabonde na sote tuwe na moyo wa kusaidiana wakati wote, hasa pale
Mwenyezi Mungu anapotupa mitihani mbali mbali.
Ndugu
Wananchi,
Kwa baraka ya siku hii, tuwaombee
mafanikio vijana wetu wa darasa la sita, la saba na Kidato cha Pili waliofanya
mitihani yao hivi karibuni na Mwenyezi Mungu awape matayarisho mema vijana wetu
wanaojiandaa na mitihani ya Taifa Kidatu cha Nne. Awajaalie wote wafaulu katika
mitihani yao. Awape wagonjwa wetu wote
shifaa ya maradhi yao na aijaalie nchi yetu amani, upendo na masikilizano na
mapenzi zaidi baina yetu.
Namalizia hotuba yangu kwa kukuombeeni
nyote kila la kheri katika kuisherehekea sikukuu hii ya Idd-el-Hajj. Tuisherehekee sikukuu hii kwa mambo ya kheri
na kujiepusha na yale yote yanayomchukiza Mwenyezi Mungu. Tumuombe Mwenyezi Mungu azikubali ibada za
mahujaji wetu wote. Tunapowasiliana nao
tuwaombe waiombee nchi yetu iendelee kuwa ya amani na utulivu. Mwenyezi Mungu
awape uwezo wale wote wenye azma ya kuitekeleza ibada ya Hijja waweze kufanya
hivyo kama walivyokusudia na kupata fursa ya kuishi japo kwa siku chache katika
miji mitukufu ya Makka na Madina Yarabbil Allamina
Mwenyezi Mungu awarehemu wazee wetu,
ndugu, jamaa na marafiki zetu wote waliotangulia mbele ya haki. Aijaze neema na
baraka nchi yetu. Atupe uwezo na wepesi wa kuitekeleza mipango yetu ya
maendeleo kama tulivyoipanga. Atujaalie
afya njema na riziki za halali. Mwenyezi Mungu atujaalie sote turudi nyumbani
kwa salama na amani.
Ahsanteni
kwa kunisikiliza.
IDD
MUBARAK
KULLU
AAM WAANTUM BIKHEIR
Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein akipena mkono wa Eid na wananchi mbali mbali katika khafla ya Eid mkokotoni Zanzibar. |
Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed akipena mkono na watoto kutoka sehemu mbalimbali za Zanzibar waliofika Mkokotoni kujumuika pamoja katika Eid . |
Wananchi mbalimbali maelf kwa mael waliomiminika Mkokotoni kuungana na Rais wa Zanzibar kwenye swala ya Eid. |
Rais wa Zanzibar Dr Shein akiwa kwenye mahojiano na watoto kwenye khafla ya Eid Mkokotoni |
Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein akisalimaian na kupeana mkono wa Eid na kinamama waliohudhuria khafla ya Eid Mkokotoni Zanzibar. |
Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein akisherehekea sikukuu ya Eid na wananchi kwa aina yake kwa kucheza bao . Bao ni mchezo wa asili wa utamaduni wa mwahili wa mwambao wa Afrika Mashariki. |
Ahsanteni sana wananchi wa Jimbo la Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini wa Unguja kwa kuja kwa wingi kwenye uwanja wa mpira wa Bungi kumsikiliza mgombea urais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein leo hii 21.Sept 2015.
Balozi Amina Salum Ali akiwahutubia wanachi waliofika kwenye mkutano huo. |
Mgombea Urais Dr Ali Mohamed akiwanadi wagombea udiwani wa CCM katika Jombo hilo |
Ahsanteni sana wananchi wa Jimbo la Micheweni Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa kuja kwa wingi kwenye uwanja wa mpira wa Konde kumsikiliza mgombea urais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein leo hii 19.Sept 2015.
DK.
SHEIN AHUTUBIA MKUTANO WA KAMPENI MICHEWENI NA KUSEMA:
·
Wavuvikaenimkaowakulaneemainakuja
·
Wakulimawamwani
mambo yenubombakabisa
Mgombeanafasiyauraiswa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi
Dk. Ali Mohamed Shein ameahidi ndani ya miaka miwili kukamilisha mpango mkubwa wa kuimarisha sekta ya uvuvi utakaojumuisha kuwapatia wavuvi boti maalum za kufanyia shughuli za uvuvi. Amesema mpango huo ambao matayarisho yake tayari yameanza utashirikisha sekta binafsi ambapo tayari makubaliano ya awaliyamefanyika ambapo katika hatua ya awali boti
20 kumi zikiwa za mita 6 na nyingine 10 za mita 9 zitapewa wavuvi kwa majaribio. Akizugumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kiwanja
cha Shamemata huko Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dk. Shein
alieleza kuwa endapo wavuvi watazikubali boti hizo baada ya majaribio boti nyingine zaidi
zitatengenezwa na kupewa wavuvi.Dk. Shein
alifafanua kuwa baada hatua hiyo kukamilika itafuata hatua nyingine ya ujenzi wa boti za ukubwa wa
zaidi ya mita 18 kwa ajili ya uvuvi wa bahari kuu hivyo kutoa fursa kwa wavuvi wa Zanzibar
kuvuna rasilimali hiyo muhimu kwa uchumi wanchi. “Tunaamini kuwa tunaweza kuwawezesha kuvua samaki eneo
la bahari kuu ndani ya miaka mitano kwa kushirikiana na
kampuni moja kubwa ya kutengeneza boti na meli za uvuvi ya Sri Lanka” Dk. Shein
aliwaambia wananchi hao waliokuwa wakimshangilia kwa nguvu sana.
Mgombea huyo aliwahakikishia wakulima wa mwani kuwa serikali imejidhatiti kuhakikisha kuwa kilimo
cha mwani aina ya ‘cotton’ wenye thamani zaidi
ambao majaribio yake yalifanyika katika baadhi ya vijiji vya wilaya ya Micheweni kinaimarishwa. Aidha Serikali atakayoiunda akichaguliwa tena itawapatia ndani ya miaka mitano kinamama wakulima wa mwani vihori
500 vya kubebea mwani baada ya serikali kuwapatia vihori 100 mwanzo ni mwa mwaka huu. “Nimekamilisha ahadi zangu kwenu kuhusu barabara, maji
na afya na kuhusu hili la uendelezaji wa eneo huru la kiuchumi la
Micheweni limeshafanyiwa usanifu tayari kwa utekelezaji” Dk. Shein alibainisha.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dr ALi Mohamed akisalimiana na maelf ya wananchi waliokuwa na hamu kupoeana mikono na yeye baada ya kumaliza mkutano. |
Ahsanteni sana wananchi wa Jimbo la Konde Wilaya ya Micheweni Mkoa wa
Kaskazini Pemba kwa kuja kwa wingi kwenye uwanja wa mpira wa Konde kumsikiliza mgombea urais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein leo hii 18.Sept 2015.
DK.
SHEIN AWAAMBIA NWANANCHI:NICHAGUENI NIA YANGU NI KUIBADILI ZANZIBAR HATUA KWA
HATUA
MgombeaUraiswa Zanzibar kupitia Chama cha
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
amewataka wananchi kumchangua tena kwa mara ya pili kuongoza Zanzibar ili aweze
kutekeleza dhamira yake ya kuendelea kuibadili Zanzibar hatua kwa hatua.
Akizungumza katika mkutano mkubwa wa kampeni katika
mji mdogo wa Konde katika Wilaya Micheweni,MkoaKaskazini Pemba leo mgombea huyo
amesema “amekusudiakuibadili Zanzibar hatuakwahatua”.
Aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali aliyoiongoza
ambayo ilikuwa chini ya mfumo wa Umoja wa Kitaifa ilifanya kazi nzuri na
kuiwezesha Zanzibar kujenga mazingira mazuri ya kuimarisha uchumi wake.
Katika mkutano huo Dk. Shein ambaye pia Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anaemaliza muda wake alisema akichaguliwa
tena ataheshimu Katiba na Sheria kwa kuunda Serikali iliyo katika Mfumo wa Umoja
wa Kitaifa kama Katiba inavyoelekeza.
Aliahidi wananchi wa Konde kuwa katika kipindi kijacho
pamoja na kuwa kumekuwepo na mafanikio makubwa katika kusambaza huduma za jamii
serikali itaendelea kuimarisha huduma hizo.
Dk. Shein aliwatahadharisha vijana kuhusu kauli rahisi za wanasiasa zinazoeleza
kama kwamba suala la ajira ni jambo jepesi na kuwaeleza kuwa serikali haina uwezo
wa kutoa ajira kwa kila kijana lakini kinachofanyika ni kuweka mazingira mazuri
ili vijana wengi waweze kujiajiri.
Ahsanteni sana ndugu wananchi wa Pemba kwa kuja kwa wingi kwenye uwanja wa Chokocho Black Magic kumsikiliza mgombea urais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein leo hii 17.Sept 2015.
Ahsanteni sana ndugu wananchi wa Pemba kwa kuja kwa wingi kwenye uwanja wa Gombani ya Kale kwenye uzindizi wa kampeni ya mgombea urais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein leo hii 15.Sept 2015. Shein
Mgombea urais wa Zanzibar kwa CHAMA CHA MAPINDUZI dr. Ali Mohamed Shein akizungumza na Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Ng. Vuai Ali mara baada ya kuwasili Uwanja wa Gombani ya Kale leo hii Pemba. |
Mgombea Urais Dr Ali Mohamed Shein akiowaonesha Katiba ya CCM wananchi waliohudhuria kwenye mkutano
MOHAMED ABOUD:WANANCHI
PEMBA WAMEIKUBALI CCM
·
CUFhawaijui mipango ya CCM.
·
Imewakwama ndoano hawatoki
lazima waisome namba.
Mjumbe
wa Kamati ya CCM ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed amesema wananchi wa Pemba wameonesha hamasa mpya
ya kukiunga mkono Chama cha Mapinduzi na hiyo imedhihirisha maneno yaliyokuwa
yakisemwa kwa miaka mingi kuwa Chama cha Wananchi-CUF si chama.
Alisema
mwamko mkubwa waliouonesha wananchi wa Pemba kukiunga mkono Chama cha Mapinduzi
umewatia homa wapinzani na wameanza kutapatapa.
Mheshimiwa
Aboud alihoji umakini waviongozi chama cha CUF wa kumpeleka kiongozi wake wa
ngazi ya juu kwenye chama kingine badala ya kubaki kuongoza na kutumikia chama
chake.
Kwa
hivyo alibainisha kuwa uamuzi wa CUF kumpeleka Makamu Mwenyekiti wake Juma Duni
UKAWA unadhihirisha uvumi kuwa kuna mgogoro katika chama hicho unaohusisha
nafasi ya kugombea urais kupitia chama hicho.
Alifafanua
kuwa minong’ono kuwa Maalim amechokana Juma Duni angalau angeweza kusimama
nafasi ya urais matokeo yake ni kupelekwa rehani Juma Duni huko UKAWA na hiyo
inatosha kuthibitisha kuwa chama hicho ni cha mtu mmoja.
Aidha
alieleza kuwa kilichomfanya Juma Duni kukubali kuwekwa rehani UKAWAni fedha na
uroho wa madaraka na si kitu kingine.
Aliwakosoa
wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Chama hicho kwa kitendo chao cha kukacha
vikao muhimu vya Baraza kitu kilichodhihirisha kuwa chama hicho hakiko kwa
maslahi ya nchi wala hakijali wananchi wanaodai kuwawakilisha.
“Kukacha
kikako cha bajeti kunadhihirisha dhamira mbaya waliyonayo wenzetu wa CUF kwa
wananchi na Zanzibar na kinachodhihiri zaidi choyo chao dhidi ya mafanikio
yaliyoletwa na serikali chini ya uongozi wa Dk. Shein” alieleza Mhe Mohamed
Aboud.
Kutokana
na wananchi wa Pemba kuwabaini CUF kuwa hawana nia njema na wananchi wala
dhamira nzuri kwa nchi yao basi lazima waisome namba.
“CUF
imeshawakwama ndoana hawakujua mipango ya CCM lazima wataisoma namba Oktoba 25”
alisemza Mjumbe huyo na kusisitiza mgombea wa CCM Dk. Ali Mohamed Shein ndio
“jembe la maendeleo Zanzibar.”
Aliwataka
wamchague Dk. Shein na kuwahakikishia wananchi kuwa katika miaka mitano ijayo watashuhudia
Zanzibar mpya kutokana na mipango mizuri iliyopangwa na mazingira bora
yaliyowekwa na serikali ya Dk. Shein.
BALOZI KARUME:
WANANCHI MSIHANGAIKE, RAIS TUNAYE.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Balozi mstaafu Ali Karume amewataka
wananchi wasihangaike kutafuta Rais wa Zanzibar kwa kuwa tayari wanaye.
“Nimesimama
kumuombea kura Dk. Ali Mohamed Shein, uwezo anao na uzoefu anao,tusikae
majukwaani kutafuta Rais wakati Rais yuko tayari” Balozi Karume alisema.
Akizungumza
katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kiwanja cha Gombani ya Kale nje ya
mji wa Chake Chake Balozi Karume alisema katika kuwaangalia wagombea amepima na
kugundua kuwa mpinzani wa Dk. Shein katika nafasi hiyo Maalim Seif hana sifa na
hawezi kulinganishwa nae.
Alibainisha
kuwa mwaka 2011 Maalim Seif alimrai Balozi Karume ajiunge na Chama cha
Wananchi-CUF lakini alimkatalia.
“aliponitaka
nijiunge na CUF nikamwambia kinagaubaga kuwa sijaona kipya kilichofanywa na
chama hicho wala sijaona baya lililofanywa na CCM” Balozi Karume aliueleza
mkutano huo.
Aliongeza
kuwa alimpasulia Maalim kwa kumueleza kuwa wakati wa mkoloni asingepata fursa
ya kugombea urais na kama angethubutu kutamka neno hilo angefungwa jela.
Ni
kutokana naMapinduzi ya mwaka 1964 ndio leo anathubutu kugombea urais hivyo
anapaswa kuheshimu Mapinduzi badala ya kuyabeza na pia kuheshimu na kuenzi
muungano wa Zanzibar na Tanganyika.
“Msikosee
kuwapa madaraka hawa jamaa watatuletea mambo yasiyotarajiwa.Nchi zinazoongoza
kwa maendeleo hivi leo zilipitia kwenye Mapinduzi na baadae kwenda katika
Muungano” Balozi Karume aliwaambia wananchi na kusisitiza kuwa Mapinduzi na Muunganowetu
ni lazima kuuenzi na kuyaendeleza.
Umati wa wanaccm Pemba waliokuja kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya mgombea urais wa Zanzibar. |
Ahsanteni sana ndugu wananchi kwa kuvunja rekodi kwa kujaza mafuriko kwenye uwanja wa Demokrasia na hii ni historia ambayo haijawahi kutokea. maana yake ni Ushindi kwa Dr Shein.
Mgombea Urais wa Zanzibar wa CHAMA CHA MAPINDUZI Dr Ali Mohamed Shein akiwahutubia wananchi waliohudhuria kwa wingi mno katika Uwanja wa Demokrasia katika ufunguzi wa kampeni ya Urais. |
Mwenyekiti wa CHAMA CHA MAPINDUZI . DR JAKAYA KIKWETE akimkabidhi Ilani ya CCM mgombea wa Urais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein katika ufunguzi wa kampeni Uwanja wa Demokrasia . |
Mwenyekiti wa CCM Dr Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi waliohudhuria mkutanoni. |
Makamu wa Rais Dr Mohamed Gharib Bilal akiwahutumia wananchi katika mkutano huo. |
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akiwahutubia wananchi waliofika . |
Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Nd Vuai Ali akiwahutubia wananchi . |
Katibu Mkuu wa CCM Nd. Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi . |
Rais mstaafu Bw. Ali Hassan Mwinyi akiwahutumia wananchi |
MGOMBEA URAIS ZANZIBAR DR ALI MOHAMED SHEIN AKIUNGUMZA NA UMOJA WA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU VYA ZANZIBAR
Sababu 40 za Dk. Ali Mohamed Shein
kugombea tena nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi.
Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein ameamua kugombea tena nafasi ya Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kupitia Chama Cha Mapinduzi. Uamuzi wake huo unatokana na kwanza dhamira yake ya kuwatumikia wananchi wa Zanzibar na pili, kuitikia wito wa wazee wa CCM na wananchi wa Zanzibar. Pamoja na sababu hizo, ziko sababu nyengine 40 kubwa zinazomshawishi kila mtu kukubali kwamba uamuzi wa Dk. Shein ni sahihi. Kwa ujumla sababu hizo na nyenginezo ndizo zilizokipelekea Chama Cha Mapinduzi kumteua kupeperusha bendera yake katika uchaguzi mkuu ujao. Sababu hizo ni:-
1.
Ameonesha
uwezo mkubwa wa kusimamia na kutekeleza Ilani
ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 – 2015 kwa zaidi ya asilimia 90.
2.
Katika
kipindi chake cha uongozi ameimarisha uchumi kutoka asilimia 6.0 mwaka 2010
hadi asilimia 7.4 mwaka 2014 na kuongeza
kasi ya maendeleo.
3.
Ameinua
kiwango cha ukusanyaji wa mapato ya ndani ambayo
yameongezeka kutoka TZS bilioni 181.4 hadi kufikia TZS bilioni 360.4, sawa na
ukuaji wa asilimia 98.7 kwa kipindi cha mwaka 2010/2011 hadi 2014/2015 au
wastani wa asilimia 19.7 kwa kila mwaka.
4.
Amepelekea
kupungua kwa mfumko wa bei kutoka asilimia 14.7 mwaka 2010 hadi asilimia 5.6 mwaka 2014 na kwenda
sambamba na maelekezo ya Ilani ya kutaka kufikia chini ya asilimia 7.
5.
Kwa
kuimarika uchumi, Pato la Taifa kwa mwananchi mmoja, kwa bei
za miaka 2010 – 2014, limekua kutoka TZS 856,000 ($613) mwaka 2010 hadi kufikia
TZS 1,552,000 ($939) kwa mwaka 2014 ikiwa imepita lengo la Ilani la shilingi 884,000 kwa mwaka
2015.
6.
Wakulima
kunufaika na ruzuku za pembejeo za kilimo kulikopelekea kuongezeka kwa mazao
hasa ya mpunga, mboga mboga na mifugo, ambapo zaidi ya wakulima 360,000
wamefaidika.
7.
Kuwaondoshea
kodi wananchi kwa bidhaa muhimu kama vile sukari, mchele na unga wa ngano.
8.
Kuliimarisha
zao la karafuu kwa kulireshea hadhi, heshima na kulipa nafasi yake katika
uchumi wa Zanzibar.
9.
Amewaongezea
uwezo wakulima wa zao la karafuu pamoja na kuongeza bei ya zao hilo kwa
wakulima kutoka shilingi 4,500 mwaka 2010 hadi kufikia shilingi 14,000 mwaka
2014 kwa kilo moja.
10.
Amepindukia
lengo la Ilani ya Uchaguzi katika ujenzi wa barabara kwa kujenga kilomita 431.6
kwa kiwango cha lami badala ya kilomita 356.3 zilizomo kwenye Ilani.
11.
Kwa
kushirikiana na sekta binafsi ameimarisha huduma za usafiri wa baharini pamoja
na kupanua maeneo ya kuhifadhia makontena na zana za kisasa za ukaguzi wa
mizigo.
12.
Amesimamia
ununuzi wa meli mpya ya kisasa ya abiria na mizigo katika kukabiliana na tatizo
la usafiri kati ya Unguja, Pemba na Dar es Salaam.
13.
Amesimamia na kutekeleza kwa ufanisi mkubwa
mpango wa upanuzi na uendelezaji wa kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Abeid
Amani Karume pamoja na kiwanja cha ndege cha Pemba.
14.
Amekamilisha
mradi wa umeme unaopita chini ya bahari kutoka Ras Kiromoni wa Megawati 100,
pamoja na kutekeleza kwa ufanisi mradi wa usambazaji umeme vijijini vikiwemo
baadhi ya visiwa vidogo vidogo.
15.
Amefanikiwa
kuongeza kwa kasi huduma za usambazaji wa maji safi na salama kutoka asilimia 75
mwaka 2010 hadi asilimia 87 kwa maeneo ya mjini na kutoka asilimia 60 mwaka
2010 hadi asilimia 70 kwa upande wa vijijini.
16.
Amewaondoshea
wazee mzigo wa kuchangia ada ya skuli katika ngazi ya elimu ya msingi ili
kuhakikisha kwamba fursa sawa ya elimu inapatikana kwa watoto wote bila ya
kujali kipato chao.
17.
Amesimamia
juhudi za kuongeza ujenzi wa skuli na madarasa kulikopelekea kuongezeka kwa
idadi ya wanafunzi wanaorodheshwa katika ngazi zote za maandalizi, msingi,
sekondari na vyuo vikuu.
18.
Ameweka
mazingira mazuri ya kuweka uwiano wa kijinsia katika utoaji wa elimu kwa ngazi
zote na kutoa fursa zaidi kwa wanawake. Kwa mfano, katika Chuo Kikuu cha Taifa
cha Zanzibar (SUZA) idadi ya wanafunzi wa kike imeongezeka kutoka 853 mwaka
2010 kati ya wanafunzi 1972 hadi wanafunzi
1244 mwaka 2015 kati ya wanafunzi
2078 ikiwa ni zaidi ya wanafunzi wa kiume.
19.
Ameimarisha
miundombinu ya afya ikiwemo majengo, wataalamu na vifaa vya kisasa.
20.
Ameimarisha
huduma za kinga na tiba na huduma ya mama na mwana katika hospitali na vituo
vya afya mijini na vijijini ikiwa ni pamoja na kuondoa malipo kwa akinamama
waja wazito wanaokwenda hospitali kujifungua.
21.
Amesimamia
hadi kukaribia kufikia kiwango cha kimataifa cha daktari mmoja kutibu watu 8000
ambapo kwa Zanzibar daktari mmoja amefikia kutibu watu 9000.
22.
Amewanufaisha
wananchi kwa kuanzisha mpango wa utalii kwa wote na kuimarisha sekta hiyo
kulikopelekea kuongeza idadi ya watalii kutoka 132,836 mwaka 2010 hadi kufikia
311,891 mwaka 2014.
23.
Amefanya
safari za nje zenye tija na maslahi makubwa kwa Wazanzibari ambapo matunda ya
ziara hizo yameongeza kasi ya uwekezaji na kukuza ajira.
24.
Ameiwezesha
Zanzibar kuingia katika ramani ya kimataifa kihabari kwa kuitoa katika mfumo wa
analogia na kuingia katika mfumo wa kisasa wa digitali.
25.
Ameimarisha
miundombinu mbali mbali ya michezo ikiwemo kuifanyia ukarabati mkubwa viwanja
vya michezo vya Amani na Gombani ili iweze kutumika kwa mashindano mbali mbali
ya kimataifa, pamoja na kukijenga upya
Kiwanja cha Mao - Tse Tung.
26.
Amesimamia
kurejeshwa hadhi ya viwanja vya kufurahishia watoto Unguja na Pemba kuvijenga
upya na kuweka vifaa vya kisasa.
27.
Kuinua
viwango vya mishahara ya watumishi wa umma na sekta binafsi pamoja na kuimarisha maslahi yao kwa ujumla.
28.
Msimamo
wake usiyoyumba katika kuimarisha amani, utulivu na maelewano miongoni mwa
Wazanzibari.
29.
Msimamo
wake usiyoyumba wa kuuendeleza na kuudumisha Muungano wa Serikali mbili.
30.
Makini
na hayumbi katika kutetea jambo analoliamini kulingana na katiba na sheria za
nchi.
31.
Ana
uwezo mkubwa wa kufanyakazi bila ya kuchoka na kujali wakati.
32.
Mkweli
na mchapakazi hodari, asiyekubali fitna wala majungu, hana ubinafsi, ana
uchungu wa Zanzibar na watu wake hasa wanyonge.
33.
Ameonesha
umakini na uhodari mkubwa katika kuasisi na kuongoza serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar yenye muundo wa Umoja wa kitaifa.
34.
Kuchukia
viongozi na watumishi wanaokiuka maadili ya uongozi, sheria na kanuni za
utumishi wa umma.
35.
Kukerwa
na vitendo vya rushwa vinavyofanywa na wanaotoa na wanaopokea rushwa na ndio
sababu ya kupitisha sheria ya kupambana na rushwa na uhujumu wa uchumi.
36.
Ameithibitishia
jamii kwamba anachukia vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kwa watoto na watu
wazima.
37.
Ameweka
mkazo
mkubwa katika kukamilisha dhamira ya kuendeleza maeneo huru ya uchumi, mpango
ambao ulibuniwa tokea mwaka 1993.
38.
Juhudi maalum alizozichukua
katika kuzifanyia kazi zile zinazotambuliwa kuwa kero za muungano, ambapo masuala kadhaa yameshatatuliwa kupitia Kamati
inayoongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayowajumuisha
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar.
39.
Amewajali sana wazee kwa kuwahudumia, kuwatunza,
kuyaimarisha makaazi yao, kuwapatia huduma muhimu za kila siku kwa maisha yao
na kuwawekea posho maalum kwa kila
mwezi.
40.
Amekusudia kuibadilisha taswira ya eneo la Fumba baada ya
kukamilika Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Kisasa wa Fumba ambayo
utekelezaji wake unaendelea pamoja na Mradi unaoendelea wa Maendeleo ya Mji wa
Kisasa Kijini – Matemwe katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.
No comments:
Post a Comment