Tuesday, 12 January 2016

SHEREHE ZA MIAKA 52 YA
 MAPINDUZI YA ZANZIBAR.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiteta na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli wakati wa kilele cha sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wananchi walioshiriki  katika   kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium leo akiwa katika gari maalum,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein    katika   kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium zilizofanyika leo. 
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu  alipowasili katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika Kilele cha sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
 
No comments:

Post a Comment